Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga mkono hoja yako kwa 100%Hivi nyie mlikuwa mnaweka pesa zenu nyingi Benki? Benki huwekwa pesa ndogo ndogo tu, kama 1milioni mpaka 50 milioni. Zaidi ya hapo tafuta pahala pengine pa kuweka.
Benk siyo mahala salama pa kuweka pesa kwani zinawindwa na TRA vinara wa Rushwa wafunge account huku vyombo vingine vikiwinda wakubambikie kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi wapate kukupora hizo fedhaUkqeli mtupu huu, yajayo yanaogopesha.
Account ya viongozi wa umma hata ikiwa na trilion 10 hawasumbukia nayo, wabebakia kupora Account za wafanyabiashara wa kawaida kwa uonevu manyanyaso makubwa kwenye Nchi yaoInatia hasira sana hii,ma DC, RC ,wakurugenzi,mawaziri nk wao ruksa kufanya chochote,ila wavuja jasho ambao hata hawajui mitaji wameipataje wanahenyeshwa sana
Ile ahadi ndiyo inatekelezwa sasaAhadi ya "kuishi" kama shetani iliyotolewa haijawahi tenguliwa!
Huu ndiyo upumbavu unaleta Athari za Benk kukosa wateje , kwani kuwa na pesa nyingi lazima ziwe zimepatikana sasa? Watu wana akiba zao za kipindi kirefu na bado zinaporwa kienyeji kwa njia haramu za kishetani, watu wanauza nyumba mashamba mazao madini na vinginevyo waache kuweka pesa Benk kisa wewe una wivu na hao TRA vinara wa kufunga Account nao wana njaa ya Rushwa? Acha wivu tafuta pesa zako Wivu utakuua ukiwa masikini mkubwa.Na kweli katika kipindi hiki kigumu inakuwaje unapata hela kuliko sisi?
HaswaaaaahBenk siyo mahala salama pa kuweka pesa kwani zinawindwa na TRA vinara wa Rushwa wafunge account huku vyombo vingine vikiwinda wakubambikie kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi wapate kukupora hizo fedha
Tatizo Bank wakigoma BOT wanaweza kuwafutia leseni....Nchi inaongozwa na washamba!! Hawaangalii impact itakayosababishwa na uhuni wao.Mabenk yasipozinduka na kukataa ujinga wa Account za wateja wao kufungwa hovyo hovyo na TRA wajiandae kufirisika kwa kukosa wateja baada ya imani na mabenk kuendelea kushuka zaidi
Siku Benk zikianza kufa ndipo BOT watajutia ujinga wao ambao Uganda Zambia kenya wametumia fursa hizo kuwaalika wafanyabiashara kwenda kuweka fedha zao huko kusiko na usumbufu wowote, mmiliki wa pesa yupo huru na pesa yake.Tatizo Bank wakigoma BOT wanaweza kuwafutia leseni....Nchi inaongozwa na washamba!! Hawaangalii impact itakayosababishwa na uhuni wao.
Wazazi wako wamepata hasaraNimesoma comment nyingi na inaonekana mleta thread hii kafanikiwa kuwafanya wachungaji kuwa emotional.
Je tunafurahia watu wanaomiliki pesa bila takwimu sahii za mapato na Kodi?
Unatoa wapi pesa kihalali ili zijae tu banki? Acheni ujinga lipa Kodi
Wengi wanaolialia ni wezi , matepeli n wizi wakubwa. Fuateni njia halali na muwe bold kujustfy utajiri wenu
Salaam Wakuu,
Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.
Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.
Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?
1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.
2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.
3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk
4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru
5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.
Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.
Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.
Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.
1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera
2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika
3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN
4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar
5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura
6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers
7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili
8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511
9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet
10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.
Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.
Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.
Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.
Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE UTANGULIZII 1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi...www.jamiiforums.com
Hizo dollar nazo zina mchezo wa expire date, unalijuwa hilo?
Mbona mimi ni tajiri sina wasiwasi,,biashara yangu ya kiosk inaendelea vizuri haisumbuliwi....Sasa tajiri anaishi kwa wasiwasi kuliko masikini
Huo sasa ndo unaitwa ubepari na ndo tunaupiga vita,ubepari ni unyamaNa kweli katika kipindi hiki kigumu inakuwaje unapata hela kuliko sisi?
Wewe hata uwezo wa kununua computer ya laki 4 huna sishangai unachukia wenye hela, utashangaa wamekuja kumuoa mama yako.Na kweli katika kipindi hiki kigumu inakuwaje unapata hela kuliko sisi?