Papy ndombe
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 3,761
- 4,535
Tajiri anaonekana Kama nyara haramuSasa tajiri anaishi kwa wasiwasi kuliko masikini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tajiri anaonekana Kama nyara haramuSasa tajiri anaishi kwa wasiwasi kuliko masikini
Ubepari uleta ajira, ukuza uchumi, ujamaa uleta umasikini na udikteta ktk nchiHuo sasa ndo unaitwa ubepari na ndo tunaupiga vita,ubepari ni unyama
Vibali ununue ukaweke ndani? We haujipendi. Hiyo ni sawa kuwa na kibali cha kuhifadhi meno ya temboUnatafuta vibali
BalaaMatajiri sita Kwa mpigo ndani ya miaka miwiliView attachment 1652731
Hii kitu hatari[emoji3061][emoji3061]Usifikiri ni utani.
Leo hii ukipata tu hela nyingi, fikiria mara mbili kabla hujapeleka bank.
Kuna wakati nililkuwa nalipwa mshahara wa dola 9,000 kwa mwezi. Nilikuwa nimeajiriwa nje ya nchi lakini niliomba mshahara wangu ulipwe kwenye akaunti yangu ya nyumbani hapa Tanzania.
Niliporudi likizo, kutaka kuchukua hela, nikaambiwa nikamwone manager wa branch. Baadaye nilifanikiwa lakini baada ya kupeleka documents za mkataba, work permit, nakala ya dicuments za kodi za nchi nilikokuwa nafanya kazi, n.k.
Sent using Jamii Forums mobile app
Uchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.Sasa hivi kuliko uweke elfu 50 bank ni bora uifiche kwenye kibubu. Wakiiona lazima wakuhoji na kukwambia umekwepa kodi kwa miaka 3 iliyopita.
Uchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.Salaam Wakuu,
Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.
Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.
Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?
1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.
2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.
3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk
4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru
5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.
Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.
Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.
Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.
1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera
2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika
3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN
4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar
5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura
6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers
7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili
8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511
9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet
10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.
Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.
Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.
Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.
Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE UTANGULIZII 1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi...www.jamiiforums.com
Ukiweka ndani si Siri yako ukichimbia chiniVibali ununue ukaweke ndani? We haujipendi. Hiyo ni sawa kuwa na kibali cha kuhifadhi meno ya tembo
Kila la heri.Ukiweka ndani si Siri yako ukichimbia chini
Sijapata jibu vipi hizi bank za nje mfano exim, barclay,absa,kcb ukiweka huko napo wanazichungulia kisha wanazikwapua au huko ni salama.Maana kuishi kishetani Hali pesa unayo napo yataka moyo.Kila la heri.
Watu wataenda kuweka pesa zao nje au watazichukua kujenga nyumba kuweka wapangaji na malipi ya kodi za nyumba yanakuwa cash mkononiUchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.
Hata Bank za kigeni BOT wanapenya hasa wakiona pesa imetoka nje kuja Tanzania, kwa sasa BOT ndiyo Benk kuu ya ajabu Duniani inazuia pesa kuja Tanzania kuleta maendeleo na hata pesa ikipenya ikafika kwenye hizo Benk napo huizuia mpaka mmiliki wa hiyo pesa atoe Rushwa au vinginevyo watamsumbua miezi kadhaa kabla ya kupewa pesa au kudhulumiwa kabsa kwa kutishiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi anakimbia anaacha pesa wanaipora kihuni kwa njia haramu za kishetani.Sijapata jibu vipi hizi bank za nje mfano exim, barclay,absa,kcb ukiweka huko napo wanazichungulia kisha wanazikwapua au huko ni salama.Maana kuishi kishetani Hali pesa unayo napo yataka moyo.
Muhimu ni kununua US Dollar tuTatizo hapa serikali ikishtuka watu hawapeleki hela bank Watakuja na mbinu ya kubadirisha pesa, hapo ndio kimbembe utazipeleka vp bank
Hata Bank za kigeni BOT wanapenya hasa wakiona pesa imetoka nje kuja Tanzania, kwa sasa BOT ndiyo Benk kuu ya ajabu Duniani inazuia pesa kuja Tanzania kuleta maendeleo na hata pesa ikipenya ikafika kwenye hizo Benk napo huizuia mpaka mmiliki wa hiyo pesa atoe Rushwa au vinginevyo watamsumbua miezi kadhaa kabla ya kupewa pesa au kudhulumiwa kabsa kwa kutishiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi anakimbia anaacha pesa wanaipora kihuni kwa njia haramu za kishetani.
Watanzania waliopo nje hasa ulaya America Asia wamelazimika kufanya maendeleo huko Huko walipo tofauti na waganda wakenya ambao maendeleo huelekeza kwao kwa kutuma pesa nyingi tokea walipo Duniani kwenda Nchini mwao ambapo hakuna usumbufu kama wa BOT ya Tanzania wala TRA kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetani
Kuweka ndani ni risk Sana but kuweka bank Zama hizi za ujamaa ni risk zaidi pia.Uchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.