Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Usifikiri ni utani.

Leo hii ukipata tu hela nyingi, fikiria mara mbili kabla hujapeleka bank.

Kuna wakati nililkuwa nalipwa mshahara wa dola 9,000 kwa mwezi. Nilikuwa nimeajiriwa nje ya nchi lakini niliomba mshahara wangu ulipwe kwenye akaunti yangu ya nyumbani hapa Tanzania.

Niliporudi likizo, kutaka kuchukua hela, nikaambiwa nikamwone manager wa branch. Baadaye nilifanikiwa lakini baada ya kupeleka documents za mkataba, work permit, nakala ya dicuments za kodi za nchi nilikokuwa nafanya kazi, n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kitu hatari[emoji3061][emoji3061]
 
Sasa hivi kuliko uweke elfu 50 bank ni bora uifiche kwenye kibubu. Wakiiona lazima wakuhoji na kukwambia umekwepa kodi kwa miaka 3 iliyopita.
Uchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.
 
Salaam Wakuu,

Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.

Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.

Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?

1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.

2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chajo
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.

3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk

4. Unalazimishwa uonge nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru

5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.

Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.

Hakika aduni wa Mtanzania ni Mtanzania.

Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.

1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera

2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika

3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN

4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar

5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers

7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili

8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511

9. MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet

10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.

Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.

Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.

Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.

Uchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.
 
Kila la heri.
Sijapata jibu vipi hizi bank za nje mfano exim, barclay,absa,kcb ukiweka huko napo wanazichungulia kisha wanazikwapua au huko ni salama.Maana kuishi kishetani Hali pesa unayo napo yataka moyo.
 
Wazee wa escrow wakubali tu kugawana salio Kama alivyofanya naongea na mwenye mbwa wake Ili wanunue Uhuru wao. Zaidi wategemee ya kina papy kocha
 
Sijapata jibu vipi hizi bank za nje mfano exim, barclay,absa,kcb ukiweka huko napo wanazichungulia kisha wanazikwapua au huko ni salama.Maana kuishi kishetani Hali pesa unayo napo yataka moyo.
Hata Bank za kigeni BOT wanapenya hasa wakiona pesa imetoka nje kuja Tanzania, kwa sasa BOT ndiyo Benk kuu ya ajabu Duniani inazuia pesa kuja Tanzania kuleta maendeleo na hata pesa ikipenya ikafika kwenye hizo Benk napo huizuia mpaka mmiliki wa hiyo pesa atoe Rushwa au vinginevyo watamsumbua miezi kadhaa kabla ya kupewa pesa au kudhulumiwa kabsa kwa kutishiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi anakimbia anaacha pesa wanaipora kihuni kwa njia haramu za kishetani.
 
Watanzania waliopo nje hasa ulaya America Asia wamelazimika kufanya maendeleo huko Huko walipo tofauti na waganda wakenya ambao maendeleo huelekeza kwao kwa kutuma pesa nyingi tokea walipo Duniani kwenda Nchini mwao ambapo hakuna usumbufu kama wa BOT ya Tanzania wala TRA kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetani
 
So wabongo nao wanatumia bashite style Kama fursa kupenyea mle mle Kama walivyofanyiwa wa bureau de change zimepelekwa kwenye uhakiki miaka 3 Sasa
 
Watanzania waliopo nje hasa ulaya America Asia wamelazimika kufanya maendeleo huko Huko walipo tofauti na waganda wakenya ambao maendeleo huelekeza kwao kwa kutuma pesa nyingi tokea walipo Duniani kwenda Nchini mwao ambapo hakuna usumbufu kama wa BOT ya Tanzania wala TRA kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetani

Malaika mkuu toka chattogang ana allergies na matajiri furaha yake ni kuona machozi ya watu.Thus wenzetu masikini, wajamaa ni marufuku kupewa leseni za kuendesha magari makubwa watasababisha ajali kubwa barabarani.Nimewaelewa
 
Uchumi hauruhusu kuweka hela ndani. hela lazima ikae benki ili itumiwe na wengine wakati wewe huzihitaji kuzitumia.
Kuweka ndani ni risk Sana but kuweka bank Zama hizi za ujamaa ni risk zaidi pia.
 
Back
Top Bottom