Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Serikali ya CCM haifurahi ukiwa na kiasi kikubwa cha fedha benki, unafilisiwa kwa kupewa kesi ya Uhujumu Uchumi

Why uweke pesa nyingi bank kwann usiziweke kwenye uzalishaji?
Sijaona mtu mjinga kama wewe, kwa hiyo pesa nikiweka benki inakuwa unakaa tu..Sasa zinazokopeshwa na mabenk unajua zinatoka wapi kama sio za watu waliozihifadhi.
 
Hawajawahi shindwa bambika kesi unaweza ambiwa unamiliki gego la fungo au fisi pori.
 
Duu mkuu kama ingeshindikana na umevuja jasho sana huko nje unakubali kunyanyaswa bado ukute kuwa hakuna Hela si ndo MTU unakufa mkuu.
Usifikiri ni utani.

Leo hii ukipata tu hela nyingi, fikiria mara mbili kabla hujapeleka bank.

Kuna wakati nililkuwa nalipwa mshahara wa dola 9,000 kwa mwezi. Nilikuwa nimeajiriwa nje ya nchi lakini niliomba mshahara wangu ulipwe kwenye akaunti yangu ya nyumbani hapa Tanzania.

Niliporudi likizo, kutaka kuchukua hela, nikaambiwa nikamwone manager wa branch. Baadaye nilifanikiwa lakini baada ya kupeleka documents za mkataba, work permit, nakala ya dicuments za kodi za nchi nilikokuwa nafanya kazi, n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaona mtu mjinga kama wewe, kwa hiyo pesa nikiweka benki inakuwa unakaa tu..Sasa zinazokopeshwa na mabenk unajua zinatoka wapi kama sio za watu waliozihifadhi.
So niache kuzizungusha kuinvest kwenye real asset nk niweke tu zikae huku nakatwa gharama za kuzihifadhi.
 
Salaam Wakuu,

Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.

Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.

Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?

1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.

2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chako
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.

3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana;;Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk

4. Unalazimishwa uongee nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru

5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.

Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.

Hakika adui wa Mtanzania ni Mtanzania.

Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.

1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera

2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika

3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN

4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar

5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers

7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili

8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511

9. Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet

10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.

Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.

Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.

Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.

Safi sana. Tano tena
 
Umasikini wa afrika umefanywa makusudi na Hawa wakoloni weusi jiwetype wenye allergies na matajiri.
Miaka 60 ya Uhuru bado wanategemea misaada.
JE HOTUBA ALIYOITOA RAISI TRUMP SEPTEMBER 2018 JUU YA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA NI MATUSI AU NDO UKWELI?

Haya ni mambo yaliyonukuliwa katika hotuba ya Raisi Trump akiongelea bara la Afrika. Naomba usome na utoe maoni yako. Akiwa anawasuta viongozi wa Afrika, Trump anahoji kwamba:
  • lkiwa sasa imefika miaka 50 ya uhuru na bado viongozi wengi wa Afrika wameshindwa kuwa na miundo mbinu thatbiti kwa ajili ya watu wao, je hao viongozi ni binadamu kweli?
  • Anaendelea kusema kuwa ikiwa ninyi viongozi mnakalia dhahabu, almasi, mafuta na uranium na watu wenu wanakosa chakula, je ninyi viongozi wa afrika ni watu kweli?
  • Kama mnakaa kwenye madaraka na kununua silaha kutoka kwa wageni na kuua watu wenu, je ninyi ni binadamu kweli?
  • Kama mnawaza kukaa madarakani mpaka mwisho wa maisha yetu, je ninyi ni binadamu kweli?
  • Ikiwa mnatumia maliasili ya nchi zenu kwa maendeleo ya familia zenu, je ninyi ni watu kweli?
  • lwapo hamjali kuweka miundo mbinu ya afya za watu wenu na badala yake mkiugua mnaenda kutibiwa nchi za nje, Je ninyi ni binadanu kweli?
  • Mtaheshimikaje katika mataifa yenu wakati mnapiga risasi raia wenu kama vile ni mchezo?
*Amemalizia kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika wataendelea kuwa kama wanyama hadi watakapo badili mtazamo wao na kuheshimu watu wanaowaongoza.

NB: Hadi kufikia hapo, unadhani Raisi Trump inatakiwa alaumie kutokana na tabia zake za kutukana waafrika, au labda anachosema ni kweli tukubaliane na yeye?
Una maoni gani kutokana na hotuba aliyoitoa huko kwenye kikao cha umoja wa mataifa? Hizi ni dharau za wazungu au kuna ukweli ndani yake?
Hitimisho Hawa wakoloni weusi kwao ni salama zaidi kuwatawala masikini na futereless people ( wanyonge).
Kumbuka v8 moja ni sawa na matreka 6 horse power 75 brand new na vilimio vyake.
So kipi v8 au trekta? Tuendelee kuaminisha tu mabeberu awapendi tuendelee.
 
Najua kesi ya jamaa yangu wa karibu kabisa aliyepigwa zaidi ya mil 90. Kashindwa kutoa hela, kaenda kuuliza anaambiwa nenda makao makuu ya Benki, huko wakamwabia serikali inasema kuna mashaka na hela yako... kabanwa mbavu aeleze amezipataje. Bahati mbaya jamaa biashara zake hazikuwa rasmi (kilimo), akakosa vithibitisho. Wakataifisha.
Duuuh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Najua kesi ya jamaa yangu wa karibu kabisa aliyepigwa zaidi ya mil 90. Kashindwa kutoa hela, kaenda kuuliza anaambiwa nenda makao makuu ya Benki, huko wakamwabia serikali inasema kuna mashaka na hela yako... kabanwa mbavu aeleze amezipataje. Bahati mbaya jamaa biashara zake hazikuwa rasmi (kilimo), akakosa vithibitisho. Wakataifisha.
Daa na hii mkuu mie nilichezwa na machale Nilikuwa na vimilioni kadhaa ni chini ya miamoja ikabidi ninunue nyumba fasta mana kwanza nadaiwa na Heslb yaani wangezibana kiukweli ningekufa. Mateso niliyopitia adi kuzipata najua mie na Aliye mbinguni.

Yaani nikiwa na dola Milioni moja hapa home sikai.
Kwanza kuna apartment ama hotel room unanunua huko Dubai ama New York wewe unaipangisha ukiwa hapa hapa
 
Muda wowote miswada itakwenda bungeni kuwazuia watu kununua dhahabu na hizo bitcoin maana kwa aina ya mtu aliyeko Ikulu

Ila kwetu sisi wazee wa kucross borders bila passport hawatatuweza watawabana misukule yao ya kijani
Mkuu gold unanunua digitally Uko dunia gani kuna kitu kinaitwa risk aversion or safe heaven.
Watu utajiri wao wanauweka sehemu salama hata kuinunua Franc ya kiswisi Iko strong sana haiyumbiyumbi ovyo ovyo
 
Back
Top Bottom