sawima
JF-Expert Member
- Jul 9, 2019
- 5,496
- 8,491
[emoji3]Kuingia road kutafuata baada ya hali kuwa ngumu sana maana wanakoenda watakusanya mpaka kodi ya wafuga majini na misukule
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji3]Kuingia road kutafuata baada ya hali kuwa ngumu sana maana wanakoenda watakusanya mpaka kodi ya wafuga majini na misukule
Sababu ya roho ya uovu iliyopandikizwa rohoni mwao upelekea wao kufanya uovuVisasi ni vya Mungu mkuu japo huwa inauma sana mpaka kupelekea watu kufanya maamuzi ya kutoa roho za watu
Sijaona mtu mjinga kama wewe, kwa hiyo pesa nikiweka benki inakuwa unakaa tu..Sasa zinazokopeshwa na mabenk unajua zinatoka wapi kama sio za watu waliozihifadhi.Why uweke pesa nyingi bank kwann usiziweke kwenye uzalishaji?
Usifikiri ni utani.
Leo hii ukipata tu hela nyingi, fikiria mara mbili kabla hujapeleka bank.
Kuna wakati nililkuwa nalipwa mshahara wa dola 9,000 kwa mwezi. Nilikuwa nimeajiriwa nje ya nchi lakini niliomba mshahara wangu ulipwe kwenye akaunti yangu ya nyumbani hapa Tanzania.
Niliporudi likizo, kutaka kuchukua hela, nikaambiwa nikamwone manager wa branch. Baadaye nilifanikiwa lakini baada ya kupeleka documents za mkataba, work permit, nakala ya dicuments za kodi za nchi nilikokuwa nafanya kazi, n.k.
Sent using Jamii Forums mobile app
So niache kuzizungusha kuinvest kwenye real asset nk niweke tu zikae huku nakatwa gharama za kuzihifadhi.Sijaona mtu mjinga kama wewe, kwa hiyo pesa nikiweka benki inakuwa unakaa tu..Sasa zinazokopeshwa na mabenk unajua zinatoka wapi kama sio za watu waliozihifadhi.
Safi sana. Tano tenaSalaam Wakuu,
Nmeanza kuelewa kwanini Matajiri wengi wa Tanzania wanaficha fedha zao nje ya Nchi. Siwalaumu tena. Na kama hii hali ikiendelea, Benki nyingi zitatikisika kiuchumi kwani watu watasusa kupeleka hela.
Zamani Watanzania wengi walikuwa hawapeleki fedha zao benki. Walikuwa wanazichimbia mashambani na wengine kuzilalia kwenye Vitanda vya Kamba. Hii walikuwa wanafanya kwa kuhofia kunyang'anywa fedha zao na Serikali. Mabenki yalifanya Kampeni kubwa kuwabembeleza watu wapeleke fedha benki na Wakafanikiwa.
Hii hali sasa imerudi kwa kasi hivi Karibuni. Nini kinafanyika?
1. Wanafuatilia benki una kiasi gani, Wakikuta hela ni nyingi Wanazizuia, Ukienda kutoa hazitoki wanakuambia zinafanyiwa Uchunguzi.
2. Wanabuni mbinu watazipataje hizo hela, hivyo ramani inachorwa ya kuzipata kwa kuangalia makando kando yako. eidha unaweza ambiwa:
i) Unamiliki fedha zisizoendana na Kipato chako
ii) Hujalipia kodi, au umepata kwa Udanganyifu.
3. Utakamatwa na kufunguliwa kesi isiyo na dhamana;;Uhujumu Uchumi.
i) Utakatishaji fedha
ii) Kuongoza genge la Uharifu
iii) Kukwepa kodi nk
4. Unalazimishwa uongee nao mfanye Makubaliano ni kiasi gani cha fedha utawapa ili Uachiliwe huru
5. Unalazimishwa ukiri kosa halafu Unapigwa faini na fedha zako zinachukuliwa. Faini haizidi fedha ulizo nazo, wanazijua hivyo wanajua utalipa tu.
Baada ya hapo Wanakuachia huru unaendelea na kazi zako. Unaanza upya kujitafutia kipato, kikiongezeka Mzunguko unaanza tena hapo kwenye maelezo namba moja.
Hakika adui wa Mtanzania ni Mtanzania.
Hapa chini naweka Mifano Michache ya Watu waliochezewa hii style ya kunyang'anya watu fedha zao ukiachilia mbali Tariq Machibya maarufu Mr Kuku.
1. Mwandishi wa Habari za kiuchunguzi Ndugu Erick Kabendera
2. Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika
3. Wafanyabiashara saba wa mafuta wakiwemo Wakurugenzi wa Kampuni ya SHIN UP Tanzania limited Zhang Zhi XIN, LINCOLN
4. Mkurugenzi mkuu wa Benki M Tanzania, Sanjeev Kumar
5. Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura
6. Astery Ndege aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers
7. Mfanyabiashara Daniel Chizua aliyedaiwa kukutwa na Kobe Wawili
8. Raia wa China, Liang Hu aliyedaiwa kuua Tembo 511
9. Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet
10. Wafanyabiashara Noah Mmasanga, Richard Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo na wengine wengi.
Vilevile kuna hukumu zinatolewa bila hata ya Kwenda Mahakamani. Mfano TCRA iliwapiga faini Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni.
Je, ni lini Tutapata Mabilionea Wapya sababu Waliopo Wanazidi kuaga dunia.
Nashauri wachunguzi wa mambo wafanyie kazi Vifo vya hawa Matajiri wa Kitanzania ambao wamekufa kwa kufuatana . Isijekuwa ni hela zao zimewatoa roho. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi Subhash Patel, Mr Reginald Mengi, Dr Rajni Kanabar, Ali Mufuruki, Salim Hassan Turky, Mr Salum Shamte nk.
Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE UTANGULIZII 1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi...www.jamiiforums.com
Duuuh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Najua kesi ya jamaa yangu wa karibu kabisa aliyepigwa zaidi ya mil 90. Kashindwa kutoa hela, kaenda kuuliza anaambiwa nenda makao makuu ya Benki, huko wakamwabia serikali inasema kuna mashaka na hela yako... kabanwa mbavu aeleze amezipataje. Bahati mbaya jamaa biashara zake hazikuwa rasmi (kilimo), akakosa vithibitisho. Wakataifisha.
Albadili zinachelewa.mfano ya issue ya Lisu aijajibu tangu iliposomwaDawa yao vinara wa kufungia watu Account zao ni kuwasomea Albadiri tu
Daa na hii mkuu mie nilichezwa na machale Nilikuwa na vimilioni kadhaa ni chini ya miamoja ikabidi ninunue nyumba fasta mana kwanza nadaiwa na Heslb yaani wangezibana kiukweli ningekufa. Mateso niliyopitia adi kuzipata najua mie na Aliye mbinguni.Najua kesi ya jamaa yangu wa karibu kabisa aliyepigwa zaidi ya mil 90. Kashindwa kutoa hela, kaenda kuuliza anaambiwa nenda makao makuu ya Benki, huko wakamwabia serikali inasema kuna mashaka na hela yako... kabanwa mbavu aeleze amezipataje. Bahati mbaya jamaa biashara zake hazikuwa rasmi (kilimo), akakosa vithibitisho. Wakataifisha.
Mkuu gold unanunua digitally Uko dunia gani kuna kitu kinaitwa risk aversion or safe heaven.Muda wowote miswada itakwenda bungeni kuwazuia watu kununua dhahabu na hizo bitcoin maana kwa aina ya mtu aliyeko Ikulu
Ila kwetu sisi wazee wa kucross borders bila passport hawatatuweza watawabana misukule yao ya kijani