Serikali ya CCM imegeuka kuwa madalali wa wakulima wa mahindi, badala ya kuwasaidia kupata bei nzuri sasa inawanyonya

Nyasi-Man

Senior Member
Joined
Sep 3, 2023
Posts
171
Reaction score
351
Tanzania imekuwa ni nchi iliojaa vituko toka kwa viongozi wasio na maono chanya yenye kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Sera nyingi zimekuwa zikikinzana na kuzua mijadala juu ya malengo yetu kama nchi ni yapi.

Serikali kupitia wizara ya kilimo ilisema itanunua mahindi kutoka kwa wakulima kwa Tsh 500 kwa kilo moja, wakati huo huo serikali imeingia mkataba wa kuizia mahindi nchi ya Zambia kwa Tsh 1000 kwa kilo. Huu ni utapeli na unyonyaji uliokithiri. Tulitegemea mkulima ndio awe mnufaika mkubwa kwenye hii biashara ila cha kushangaza dalali (serikali) anakula sahani moja na mkulima (aibu kubwa sana).

WhatsApp Image 2024-07-17 at 9.02.01 PM.jpeg

Kama ilivyo kawaida yao baada ya wakulima kupinga bei zao za kitapeli, kiongozi mkuu kaibuka na kauli ya bei elekezi (Tsh 700 kwa kilo) na kibaya zaidi wengi bado wanapumbazwa na utamaduni huu ambao umekuwa ndio desturi ya CCM kuhadaa wananchi na kuishia kusifia na kushangilia ujinga. Hapa kwa wenye uelewa wa uongozi dhamira na nia ya kwanza ndio hasa lilikuwa lengo la hawa madalali kwamba wanunue kilo moja kwa Tsh 490 mpaka 500.

WhatsApp Image 2024-07-17 at 8.38.49 PM.jpeg

Ilitakiwa bei iwe Tsh 800 au 900 ili kuhamasisha shughuri za kilimo kwa Watanzania na hii itaongeza uzalishaji na hivyo kuchochea kuongezeka kwa viwanda, hivyo ajira za kutosha zitapatikana na maisha ya watanzania yataboreka kwa kiwango kikubwa. Sio mnakuja na sera za maisha bora kwa kila Mtanzania huku mkiendelea kunyonya mkulima. Acheni utapeli wenu na mjikite kutumikia nchi kwa misingi na utawala bora na sio kuwa madalali na matapeli kwa raia.

Pia, soma: Kuelekea 2025 - Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa mia 700 kwa kilo
 
Cha ajabu matajiri wengi hawataki kununua Kwa hiyo 700 wanataka 450
Kwahiyo mkulima mwenye shida Hana namna
Huu ujinga aisee, mi nimeyahifadhi siuzi Kwa bei ya kipuuzi,Sina njaa acha yakae😄
 
Cha ajabu matajiri wengi hawataki kununua Kwa hiyo 700 wanataka 450
Kwahiyo mkulima mwenye shida Hana namna
Huu ujinga aisee, mi nimeyahifadhi suzi Kwa bei ya kipuuzi
Kweli brother kuliko kujaza matumbo ya walafi sikilizia kwanza, viongozi wengi ni greedy and selfish........unadhani motivation ya wakulima kulima zaidi itatoka wapi kama serikali haiwatengenezei mazingira bora ya bidhaa zao.....tabu tupu
 
Ni tabu sana brother kuwa na viongozi wasiosaidia wakulima wao kunufaika lakini pia kuwatia moyo ili waongeze zaidi shughuri za kilimo.....ila wao wanataka kugawana 50/50 wakati hawajachangia chochote
Wamemzuia mkulima kuuza kwenye soko atakapo yeye lakini hawana cash ya kumlipa

Wanachagua quality ya mahindi wanayo itaka wao wasiyo itaka Wana mludishia mkulima na wakati huo huo wamemzuia asiuze kokote Ila wao

Wametoa Bei elekezi lakini Bei zilizopo mitaani nitofauti kabisa na zilizo tangazwa

Waziri husika ni mfanya biashara kwahiyo sizani Kama mkulima atakuwa sarama
 
Viongozi wengi wa ccm ni walafi na wabinafsi wasio na utu.
Ni bora wakulima mkaangalia mfumo thabiti wa kuuza mazao yenu kuliko kupitia kwa hawa watu.
Tatizo nikwamba mkulima haruhusiwi kutafuta soko lingine kufanya hiyo nikosa kubwa kwa serikali yetu tukufu

Huku mipakani wame tusambazia maaskali na patrol nikubwa kwelikweli Ila tunaishi nao
 
Tanzania imekuwa ni nchi iliojaa vituko toka kwa viongozi wasio na maono chanya yenye kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Sera nyingi zimekuwa zikikinzana na kuzua mijadala juu ya malengo yetu kama nchi ni yapi.

Serikali kupitia wizara ya kilimo ilisema itanunua mahindi kutoka kwa wakulima kwa Tsh 500 kwa kilo moja, wakati huo huo serikali imeingia mkataba wa kuizia mahindi nchi ya Zambia kwa Tsh 1000 kwa kilo. Huu ni utapeli na unyonyaji uliokithiri. Tulitegemea mkulima ndio awe mnufaika mkubwa kwenye hii biashara ila cha kushangaza dalali (serikali) anakula sahani moja na mkulima (aibu kubwa sana).

Kama ilivyo kawaida yao baada ya wakulima kupinga bei zao za kitapeli, kiongozi mkuu kaibuka na kauli ya bei elekezi (Tsh 700 kwa kilo) na kibaya zaidi wengi bado wanapumbazwa na utamaduni huu ambao umekuwa ndio desturi ya CCM kuhadaa wananchi na kuishia kusifia na kushangilia ujinga. Hapa kwa wenye uelewa wa uongozi dhamira na nia ya kwanza ndio hasa lilikuwa lengo la hawa madalali kwamba wanunue kilo moja kwa Tsh 490 mpaka 500.

Ilitakiwa bei iwe Tsh 800 au 900 ili kuhamasisha shughuri za kilimo kwa Watanzania na hii itaongeza uzalishaji na hivyo kuchochea kuongezeka kwa viwanda, hivyo ajira za kutosha zitapatikana na maisha ya watanzania yataboreka kwa kiwango kikubwa. Sio mnakuja na sera za maisha bora kwa kila Mtanzania huku mkiendelea kunyonya mkulima. Acheni utapeli wenu na mjikite kutumikia nchi kwa misingi na utawala bora na sio kuwa madalali na matapeli kwa raia.

Pia, soma: Kuelekea 2025 - Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa mia 700 kwa kilo
KAMA ULIKUWAGA HUJASHTUKIA HIYO ISHU POLE SANA HASA MIKOA YA NYANDA ZAJUU KUSINI NDO WAHANGA WAKUBWA SABABU WENGI WAO HAWAPATI TARIFA SAHIHI LA SOKO KWA WAKATI
 
kiongozi mkuu kaibuka na kauli ya bei elekezi (Tsh 700 kwa kilo) na kiba
Hata bei hii ni msumari wa moto kwa mkulima. Ekari moja inatoka magunia 13 ya kilo 100 kama imetunzwa kwa viwango stahiki (japo wengi huishia kupata magunia 8) ambapo kwa bei hiyo mkulima atapata 910k.

Nb gharama za mbolea ni mifuko 5 kwa ekari 140k (sawa na sh 540k). Ukiongeza na gharama za kulimia, kupandia, kupalilia, kuvuna na kuhifadhia nafaka , hakuna kitu mkulima anapata kwa bei hiyo.

Nchi hii, bora kuuza makopo kuliko kulima.
 
B

🤔🤔NI unyonyaji wa kutisha
 
Wamemzuia mkulima kuuza kwenye soko atakapo yeye lakini hawana cash ya kumlipa

Wanachagua quality ya mahindi wanayo itaka wao wasiyo itaka Wana mludishia mkulima na wakati huo huo wamemzuia asiuze kokote Ila wao

Wametoa Bei elekezi lakini Bei zilizopo mitaani nitofauti kabisa na zilizo tangazwa
Kwann wanatia bei elekezi kwenye kitu ambacho hawakuhusika kukizalisha? Kwani walimsaidia mkulima kwa chochote? Mbona mishahara yao wanapenda kuitumia Dubai na kwingineko?
 
Hapo ndipo utagundua kwanini kiongozi frani wa East Africa aliwai kumwambia nyelele Ana ongoza maiti sio watu

Hapo hakuna kingine zaidi ya Bashe na mama kushilikiana kutu nyonya wakulima
 
Hata bei hii ni msumari wa moto kwa mkulima. Ekari moja inatoka magunia 13 ya kilo 100 kama imetunzwa kwa viwango stahiki (japo wengi huishia kupata magunia 8) ambapo kwa bei hiyo mkulima atapata 910k.

Nb gharama za mbolea ni mifuko 5 kwa ekari 140k (sawa na sh 540k). Ukiongeza na gharama za kulimia, kupandia, kupalilia, kuvuna na kuhifadhia nafaka , hakuna kitu mkulima anapata kwa bei hiyo.

Nchi hii, bora kuuza makopo kuliko kulima.
Well said mkuu, kwa mchanganuo huo mkulima hawezi toboa na atazidiwa kwa mbali na muuza makopo
 
KAMA ULIKUWAGA HUJASHTUKIA HIYO ISHU POLE SANA HASA MIKOA YA NYANDA ZAJUU KUSINI NDO WAHANGA WAKUBWA SABABU WENGI WAO HAWAPATI TARIFA SAHIHI LA SOKO KWA WAKATI
Mkulima wa Tanzania kujikomboa ni kazi sana .....vikwazo ni vingi mno
 
Back
Top Bottom