Tanzania imekuwa ni nchi iliojaa vituko toka kwa viongozi wasio na maono chanya yenye kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Sera nyingi zimekuwa zikikinzana na kuzua mijadala juu ya malengo yetu kama nchi ni yapi.
Serikali kupitia wizara ya kilimo ilisema itanunua mahindi kutoka kwa wakulima kwa Tsh 500 kwa kilo moja, wakati huo huo serikali imeingia mkataba wa kuizia mahindi nchi ya Zambia kwa Tsh 1000 kwa kilo. Huu ni utapeli na unyonyaji uliokithiri. Tulitegemea mkulima ndio awe mnufaika mkubwa kwenye hii biashara ila cha kushangaza dalali (serikali) anakula sahani moja na mkulima (aibu kubwa sana).
Kama ilivyo kawaida yao baada ya wakulima kupinga bei zao za kitapeli, kiongozi mkuu kaibuka na kauli ya bei elekezi (Tsh 700 kwa kilo) na kibaya zaidi wengi bado wanapumbazwa na utamaduni huu ambao umekuwa ndio desturi ya CCM kuhadaa wananchi na kuishia kusifia na kushangilia ujinga. Hapa kwa wenye uelewa wa uongozi dhamira na nia ya kwanza ndio hasa lilikuwa lengo la hawa madalali kwamba wanunue kilo moja kwa Tsh 490 mpaka 500.
Ilitakiwa bei iwe Tsh 800 au 900 ili kuhamasisha shughuri za kilimo kwa Watanzania na hii itaongeza uzalishaji na hivyo kuchochea kuongezeka kwa viwanda, hivyo ajira za kutosha zitapatikana na maisha ya watanzania yataboreka kwa kiwango kikubwa. Sio mnakuja na sera za maisha bora kwa kila Mtanzania huku mkiendelea kunyonya mkulima. Acheni utapeli wenu na mjikite kutumikia nchi kwa misingi na utawala bora na sio kuwa madalali na matapeli kwa raia.
Pia, soma: Kuelekea 2025 - Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa mia 700 kwa kilo