Serikali ya CCM na mwendo wa kula kwa urefu wa kamba zao

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Wananchi tunalalamika na mzigo wa kodi usio wa haki.

Wanaanza kudai kodi ya pango day 1 umepangisha baada ya safari ndefu Isiyowahusu wao ya ujenzi wa nyumba.

https://www.jamiiforums.com/threads/wizi-wa-tra-kupitia-kodi-ya-pango.2058986/

Wao Kodi hawalipi, ila sisi.

Kulikoni bus hili la Namungo kusajiliwa SM? Yaani, pasipo na kulipiwa kodi?

Tunayasikia ya hivi pia kule Nyanyembe Nyota Wakubwa.

Kwamba ni mwendo wa makulaji kwa urefu wa kamba zenu siyo?
 
Hatari sana kwa kweli.
Ina maana timu ya Namungo ni mradi wa Halmashauri ya Ruangwa?
 
Namungo ni timu inayomilikiwa na halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa hivyo mmiliki wa basi hilo si Namungo bali Ruangwa dc na timu ya Ruangwa dc kama ilivyo kwa KMC FC.
 
Namungo ni timu inayomilikiwa na halmashauri ya wilaya ya Ruangwa hivyo mmiliki wa basi hilo si namungo bali ruangwa dc na timu ya ruangwa dc kama ilivyo kwa KMC FC.
Una maana Namungo na KMC ni timu za serikali zenye kuendeshwa kwa kodi za wananchi zikiwemo hizi za majengo wengine tunazozilalamikia? Mwongozo wako tafadhali.
 
Hapa mbuzi amekula kwa urefu wa kamba yake, kaamua kuila na kamba yenyewe, sasa mbuzi wetu mamvi mpaka piko ni mbuzi huru anakula atakavyo na kwa umbali wowote.
 
Una maana Namungo na KMC ni timu za serikali zenye kuendeshwa kwa kodi za wananchi zikiwemo hizi za majengo wengine tunazozilalamikia? Mwongozo wako tafadhali.
hapana timu inaendeshwa kwa ufadhili ila inamilikiwa na halmashauri.hata huko nyuma tulikuwa na timu nyingi zilizokuwa zinamilikiwa na mashirika ya umma,lkn utofauti wake ni kuwa zilikuwa zinatumia fedha za serikali.tulikuwa za timu za ujenzi,afya,magereza,polisi,jkt,ushirika moshi nk.kwa sasa kuna maboresho kidogo,wafadhili pamoja na mapato ya timu ndo yanayoendesha timu.pia hilo basi linatumika kwa shughuri mbalimbali za halmashauri.
 
Namungo ni timu inayomilikiwa na halmashauri ya wilaya ya Ruangwa hivyo mmiliki wa basi hilo si namungo bali ruangwa dc na timu ya ruangwa dc kama ilivyo kwa KMC FC.
Acha uongo wewe
 
Sasa hili bus lililonunuliwa Kwa kodi za wananchi kujikuta na hizo chapa za Azam, NBC, Sport Pesa, Namungo FC nk unaiona imekaa je mkuu? Kwamba hili bus kumbe ni la serikali wala si Namungo?

Hali hii inazo baraka za CAG kweli?
 
Kuna shida sehemu.
 
Namungo ni timu inayomilikiwa na halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa hivyo mmiliki wa basi hilo si Namungo bali Ruangwa dc na timu ya Ruangwa dc kama ilivyo kwa KMC FC.
Unamaanisha hata bus la KMC lina plate number kama za bus la Namungo?
 
Hapa mbuzi amekula kwa urefu wa kamba yake, kaamua kuila na kamba yenyewe, sasa mbuzi wetu mamvi mpaka piko ni mbuzi huru anakula atakavyo na kwa umbali wowote.

Hii ni offside ya wazi isiyohitaji ku consult VAR popote. Walioko nyuma ya hili na walielewe hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…