Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
July 04, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan alisema serikali ya CCM itanunua vichwa na mabehewa vilivyotumika (mtumba) na vyenye hali nzuri watavitengeneza.Mradi mkubwa wa thamani ya Sh16 trilioni kutumia mabehewa na vichwa (used), hii sasa ndiyo hujuma yenyewe. Hata hakuna ambaye anahujumu mradi.
HUJUMA kwa SGR ni kununua madude yaliyotumika wakati wa ‘Escape from Sobibor’ mwaka 1943. Unatia nakshi. Unanunua mabehewa na vichwa used.Kuendesha mradi wenye thamani ya trilioni 16 kwa treni ambayo siyo high performance locomotive na haina Auxiliary Power Unit (APU) hii ndiyo HUJUMA.Dunia sasa inatengeneza sera za viwanda na kuzuia uagizaji wa vifaa vya mitumba (used), serikali ya CCM kupitia waziri wake wa fedha, ipo tofauti na Dunia.Mwigulu Nchemba na bunge la CCM wamepitisha sheria ya manunuzi kuhalalisha ununuzi wa mitumba (chakavu) katika ndege, meli, vichwa vya treni, mabehewa.Kwa mantiki hiyo, mradi wa SGR umehujumiwa na SERIKALI na siyo kama ambavyo tunataka kuaminishwa sasa. Msiwasingize kunguru au nyaya kukatwa.Sheria ya manunuzi ya umma 2011 s.66(2) inaruhusu Serikali kununua mitambo chakavu (used), lakini kwa DHARURA na waziri LAZIMA atengeneze kanuni!Sheria ya Manunuzi ya Umma inataka waziri kuunda kamati maalum ya ushauri kiufundi inayojumuisha watu wenye taaluma, maarifa, uzoefu masuala ya ununuzi. Tufahamishwe kundi lililompa ushauri waziri wa uchukuzi kununua mabehewa na vichwa vya treni vya MTUMBA kwa DHARURA. Hao ndiyo WAHUJUMU.NB; Kila mwaka Serikali ya CCM inatumia Sh558 bilioni kununua magari mapya (VX V8) ‘shangingi’. Vitu vipya kwa watawala, vyuma chakavu kwa walipa kodi?