ROSTAM AZIZ, Mweka Hazina Mstaafu wa CCM, anasema alipoanza mishe zake chamani, alikuta fomu za CCM hazina mahala pa kujaza MFANYABIASHARA.
Chama kiliundwa kwa raison detre (SABABU YA UWEPO) ya kupigania wanyonge, masikini wa kutupwa, wakulima na wafanyakazi.
Yeye anasema akasukuma mabadiliko makubwa ya kualika Watanzania wenye background zozote. Wakasema utajiri si dhambi, na umaskini si sifa. Vizuri.
Lakini je, baada ya kualika kila mja ajaye, chama kilichukua hatua gani kudhibiti pitfalls zinazokuja kwa kujumuisha kila aina ya watu ?
Hakuna!
Walichapa fomu mpya tu. Kwenye Ukulima na Ufanyakazi wakaongeza Mpiga mishe.
Ndio wakaja maharamia wa kila aina chamani.
Tarehe 29 Oct 2025 tuliona bendera za Chama Cha Mwalimu zinachomwa moto. Ofisi za chama zinachomwa moto.
Ofisi za TANU, ofisi za CCM, zamani zilikuwa mahala takatifu. Hata mgomvi wako ulikuwa unamwambia ee bwana nitakupeleka CCM! Una kagari huna egesho ulikuwa unaenda kulilaza CCM. Palikuwa sehemu salama na kimbilio la wanyonge.
Leo Serikali ya CCM, Chama Cha Ukombozi wa Afrika, imeshtakiwa kwenye mahakama ya jinai za dunia kwa makosa ya kuua raia wake wenyewe. Kufukuza raia wake kwenye ardhi zao na kuwauzia Waarabu. Kuteka na Kufira raia.
CHAMA CHA MAPINDUZI kinanuka damu. Kinanuka dhulma. Kinanuka mavi. Kwa sababu vyombo vyake vya usalama vimejisifia kwamba vikikuchukua vinakutesa na vinakufira. Kinanuka uhaini wa kupindua matakwa ya wananchi kwenye sanduku la kura.
Leo Mwalimu amebiringika kaburini. Chama chake cha ukombozi kina tuhuma nzito za dhulma, kwa uhabithi, ujahili, na ujaalaana. Dhidi ya watu wake yenyewe. Watu wa CCM leo ni matapishi ya dunia. Jakaya Mrisho Kikwete, umeshika remote kwa pembeni, utakwepa hukumu, lakini wale uliowaingiza mkenge wakaenda kumwaga damu za wananchi ili familia zenu tatu tano ziendelee kutawala tunaomba dunia iwanyonge mpaka kufa.