Serikali ya Haiti yatangaza hali ya Hatari na Marufuku ya Kutoka Nje Usiku

Serikali ya Haiti yatangaza hali ya Hatari na Marufuku ya Kutoka Nje Usiku

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Serikali imetangaza hali ya dharura na amri ya kukaa ndani (kuanzia Saa 12 Jioni - 11 Asubuhi) hadi Machi 6, 2024 kwa Wakazi wa eneo la Ouest linalojumuisha Mji Mkuu katika jitihada za kukabiliana vurugu kwenye Magereza Mawili zilizowawezesha Maelfu ya wafungwa kutoroka Machi 3, 2024

Vurugu hizo zilizosababisha Vifo vya takriban watu 12 huku Wafungwa zaidi ya 4,000 wakitoroka, zimesababishwa na magenge ya Uhalifu yanayoongozwa na Askari wa Zamani (Jimmy Cherizier) wanaomshinikiza Waziri Mkuu, Ariel Henry kutoka Madarakani

Ikumbukwe, Wiki iliyopita Ariel Henry alikuwa Kenya wiki kusaini makubaliano ya kutuma Polisi kuongoza jukumu la kurejesha Sheria na Utaratibu kwa msaada wa Umoja wa Mataifa katika taifa hilo lililoathiriwa na Magenge ya Uhalifu

..........

Sources : Aljazeera : Haiti declares curfew after 4,000 inmates escape jail amid rising violence

Citizen Digital : https://www.citizen.digital/news/haiti-govt-declares-state-of-emergency-curfew-n337809
 
Religion in Haiti according to the World Religions Database (2020)[2]

Catholicism (65.9%)
Protestantism (19%)
Other Christian (9%)
No religion (2.75%)
Spiritist (2.7%)
Other religion (0.65%)

Serikali imetangaza hali ya dharura na amri ya kukaa ndani (kuanzia Saa 12 Jioni - 11 Asubuhi) hadi Machi 6, 2024 kwa Wakazi wa eneo la Ouest linalojumuisha Mji Mkuu katika jitihada za kukabiliana vurugu kwenye Magereza Mawili zilizowawezesha Maelfu ya wafungwa kutoroka Machi 3, 2024

Vurugu hizo zilizosababisha Vifo vya takriban watu 12 huku Wafungwa zaidi ya 4,000 wakitoroka, zimesababishwa na magenge ya Uhalifu yanayoongozwa na Askari wa Zamani (Jimmy Cherizier) wanaomshinikiza Waziri Mkuu, Ariel Henry kutoka Madarakani

Ikumbukwe, Wiki iliyopita Ariel Henry alikuwa Kenya wiki kusaini makubaliano ya kutuma Polisi kuongoza jukumu la kurejesha Sheria na Utaratibu kwa msaada wa Umoja wa Mataifa katika taifa hilo lililoathiriwa na Magenge ya Uhalifu

..........

Sources : Aljazeera : Haiti declares curfew after 4,000 inmates escape jail amid rising violence

Citizen Digital : https://www.citizen.digital/news/haiti-govt-declares-state-of-emergency-curfew-n337809
 
Nimeona BBC news raisi Ruto ametoa ahadi ya kupeleka polisi 1000 Haiti, alivyo kiherehere. Hayo maandamano ya Kenya watu hawana silaha polisi wanakimbizwa seuse Haiti iliyojaa gangsters wanaotembea semi automatic guns mchana kweupe.

Bado culture difference ya Caribbeans na EA sijui watafanya kazi vipi na hao polisi wa Haiti, nchi za jirani na Haiti zimekaa kimya Ruto yeye anajifanya mjuaji; ngoja hao polisi wake waanze kurudishwa kwenye masanduku.
 
Si ndio hawa badala ya kuokoa watu wakaanza kuiba juisi, makabichi ,hoho, biskuti na kashata kwenye lile shambulio la mall? Basi huko Haiti wanaenda kuongeza vikundi vya wahalifu
 
View: https://m.youtube.com/watch?v=5Zlx3fnPCXo
Mamlaka za Haiti yatangaza hali ya hatari ya saa 72 pamoja na amri ya kutotoka nje usiku baada ya magenge yenye silaha kuvamia magereza mawili makubwa zaidi nchini humo na kuwaachilia maelfu ya wafungwa. Jela kuvunjwa yanakuja huku taifa likikabiliana na ghasia zisizokoma zinazoendeshwa na magenge zaidi ya 80 ambao pia walijaribu kuvamia uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo mji mkuu wa Port-au-Prince .

Source : NBC News

HISTORIA YA MIAKA 220 YA UHURU WA NCHI YA HAITI
Taifa hili la weusi lililojikomboa kupitia mapambano yaliyoanza mwaka 1791 na January 1, 1804 kufanikiwa kuwa hurt kutoka kwa ukoloni wa Wafaransa.

Miaka 220 tangu ipate uhuru Haiti tungetegemea ingekuwa mbali sana. Lakini miaka kibao ya vikwazo vya kiuchumi kutoka mataifa ya ulaya kama Hispania, France vinadaiwa kukikwamisha nchi hiyo Kisiwa cha Haiti kupata maendeleo.

Pia hata baada ya vikwazo hivyo vya nchi za ulaya kuisha, kuanzia mwaka 1900 utawala wa kidikteta, mapinduzi, kukosakana utawala bora na wa kidemokrasia Haiti imezidi kukosa maendeleo na utawala wa sheria kushindikana na tunaona Leo miaka 220 baada ya kupata uhuru wake kwa njia ya damu bado nchi hiyo inajitafuta kujiweka sawa kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Rais wengi wa Haiti waliamua kuhama nchi na hadi leo mamia ya waHaiti wanajiweka katika hali ya hatari kupitia Darién Gap msitu mnene katika mpaka baina ya Colombia na Panama wakijaribu kutafuta maisha bora kama wakimbizi wa kiuchumi wanaosafiri kwa njia za panya kufika nchi za Marekani ya Kaskazini yaani USA na Canada.

Soma zaidi : Wahamiaji toka Congo, Haiti, Cuba, Venezuela n.k katika safari yao ya miguu :
1709682389371.png

Kenya wanaenda fanya nini huko, hizi kazi waachiwe wagner, vita na gangstars sio mchezo.
 
Back
Top Bottom