Toyota ndio the best seller, is No 1 worldwide for more than 20 years; unafananisha na gari za Iran ambazo hata hatujui ni aina gani?
Mkuu Iran sio watu wa kubahatisha.
Sawa gari zao hazijajulikana kwasababu ya vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa.
Ila mind you Iran ingekua imeachiwa huru aisee watu wangepiga sana nduru.
Mfano mdogo tu,umeona hii reli yetu ya SGR?
Mie nina wazee TRC,walinipa fununu kuwa ilikua bado kidogo wajenge Iran,na Iran wako na teknolojia nzuri sana ya reli,ila ubahili wa 10% ukawafanya wakose tenda na kupewa mzabuni Yepi Merkezi.
Iran ni watu ambao huwa wakifanya kitu wanajizatiti na hawabahatishi.
USA na washirika wake kumuwekea vikwazo hawajakurupuka,wanajua uwezo wake mkuu.
Wewe fikiria taifa lina vikwazo takriban miaka 40+ ila ipo uchumi wa kati wa juu,imeendelea kiteknolojia sio tu ya silaha bali hata ya nuclear,madawa(waliunda chanjo yao ya corona),reli n.k n.k.
Jiulize wangekua huru kama Tanzania tu wangelikua wapi!??
Na hizo gari zinakuwa manufactured from scrap to a whole thing.