Serikali ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ijiuzulu kwa kushindwa kutumia rasilimali za nchi hii kwa maendeleo ya watu wote

Serikali ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ijiuzulu kwa kushindwa kutumia rasilimali za nchi hii kwa maendeleo ya watu wote

Inaumiza sana
Mpaka unajiuliza hivi hawa vihongozi wetu zipo kweli kichwani.
Haiwezekani mtu mmoja atembelee V8 ya 400 millions huku watu 40000 wakinywa maji na mbwa pamoja na ng'ombe kisa tu pump ya million 100 imekosekana
Wapo kwa ajili ya maslai yao,
 
Habari!
Huu uzi ninauandika nikiwa na jazba na ghazabu.
Nimefanya kazi mgodi wa GGM(GEITA GOLD MINE), kisha nikafanya Mgodi wa Bulyanhulu uliokuwa ukimilikiwa na Barrick kisha Acacia.

Ardhi yetu imemeza matrilioni ya fedha.
Nimefanya kazi kwenye hifadhi ya Serengeti kwenye hoteli ya kitalii FOUR seasons na kuizungukia hifadhi kwa umakini siku za off. Ni utajiri mtupu.
Ukianzia Tanga mpaka Mtwara kuna bahari, kuna maziwa, kuna hifadhi nyingi, kuna mapori mengi.

Tuna madini ya chuma, gesi, makaa ya mawe, ardhi inayosapoti kila aina ya mazao. Kama zao hili halikubali Mbeya basi Morogoro linakubali, kama Lindi halikubali Njombe linakubali n.k, n.k
Sasa mpaka leo serikali imeshindwa kutoa mkopo kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu,
Serikali imeshindwa kutoa huduma za afya bure.
Serikali imeshindwa kuondoa nyumba za manyasi na udongo kwa kuboresha sekta ya kilimo na ufugaji.

Je, si wakati sasa serikalini kujiuzulu?

View attachment 2073871hii ni shule ya serikali jamani sio kilinge cha mganga wa kienyeji.
Maendeleo ya kitaifa huanzia kichwani kwa mtu mmoja mmoja. Kama unao ubunifu hujakatazwa kuutumia kwa faida ya jamii inayokuzunguka.

Ni mtazamo wa kizamani kuendelea kulialia wakati tumezungukwa na rasilimali za kila aina. Kulaumu serikali kwa kushindwa kuleta maendeleo wakati wewe ni mtanzania ni aibu kwako pia.

Kutumia picha za kudhalilisha kuonyesha umaskini wakati na wewe unayo passport ya Tanzania ni kuendelea kujidhalilisha pia.
 
Mkuregenzi ananuliwa v8 la milioni 400 la kumpeleka kazini na kupeleka watoto wake shule ndio Kazi kubwa ya haya ma v8 Ili ailinde tu ccm
CCM ya sasa ni Zimwi katika uhalisia wake.Wanaifyonza nchi hii kuliko Kupe au Ruba,na ndiyo maana wakuhisi tu unatishia,unanyemelea au kutamani kuwaondoa katika utawala wao hata kwa njia halali kama uchaguzi huru ama Katiba/sheria mpya, lazima wakuangamize kisiasa,kiuchumi,kijamii na hata jela/kifo kabisa.
They have turned into Vampires!
 
True ni kikundi cha wapigaji wachache wa kunufaika na kodi zetu
 
Back
Top Bottom