Mim najiuza unataka nimweke mwanangu mazingira haya?
Twajua yapasa tuishi na watoto wetu ila kuna mazingira hapana kwa kweli
Uko sahihi
Kuna mazingira hatarishi kwa malezimya mtoto
Bweni ndio solution
Familia nyingi zins changamoto za mazingira ikiwemo mfano kipato
Familia haina kipato cha uhakika cha kuhakikisha mtoto kala kila siku sababu ni wanachofanya wanakopa wanapeleka mtoto Bweni ambako atakuwa na uhakika wa kila siku kupata mlo tena cheap kuliko angekuwa nyumbani wao wanabaki na njaa zao na kuhangaikia kulipa deni
Pili kuna familia baba na mama wako nyumba moja lakini kutwa hawaivi kutwangana mingumi na kutukanana kila siku .Wazazi wansojielewa hupeleka mtoto bweni wabaki na matatizo yao mtoto aondoke maeneo hatarishi kwa makuzi.
Kuna mitaa hatarishi kwa watoto mtoto kubakwa nje nje kumejaa mateja kila kona na wavuta bangi hatari kwa watoto nk
Wazazi waamua kupeleka watoto bweni wadogo inatakiwa ufuatilie reason sio tu kuwaona wajinga
Tembelea environment za wazazi wenye watoto bweni angalia majukumu yaio yakoje kikazi chukulia natoa mfano tu mdogo ni mfano sio kitu halisi mfano mlinzi wa mama Samia raisi ni single mother kutwa yuko naye safarini huyo mwanaye shule ya day haiwezi kumfaa.Bweni ndio saizi yake.Sababu nchi inamhitaji mama yake sana kwa kazi nzito
Kuna single mothers ambao wana watoto na majukumu ya kutwa kutafuta riziki.Soo kila mtoto ana baba na mama yake
Huyu single mother hustler mhangaiksko.mtafuta riziki hadi usiku wa manane unapotaka mwanawe asome day school akili kichwani zitakuwa hazimo
Kwa sasa hivi single mothers ni wengi mno wako hadi wabunge mawaziri,majaji, maproffessor, wenye vyeo vikubwa serikalini kibao
Kwa kazi zao kukataza bweni ni kutowatendea haki single mothers