Serikali ya Kenya kuwaajiri madaktari kutoka Tanzania, Uhabeshi na Cuba

usalama kwanza.....sio madaktari wote wa Kenya wanapenda huo mgomo lakini wametishiwa iwapo watalejea kazini peke yao.
 
Wawafukuze, watangaze ajira huko huko kwao anayetaka aombe upya, uone kama hawataomba maana Kuna wengine wamelazimishwa na wenzao kugoma hivyo watakuwa wameonewa nina amini serikali ya Kenya inatambua hilo
 
Wewe Yehoyada nina wasiwasi na upeo wako wa uelewa wa mambo. Yaani wenzako wana negotiate kwa ajili ya maslahi yao halafu wewe ujitie kiherehere kwenda kufifisha juhudi zao halafu wakuangalie tu? Hivi mtu akiwa UVCCM na uwezo wa kufikiri hupotea sio? Wewe unafikiri yanayotokea South Africa ni kwa sababu ya nini? Mojawapo ya sababu ni kwa hao wageni kuwa tayari kuajiriwa kwa malipo kiduchu ambayo wao hawayaafiki na hivyo kuwakosesha ajira wenyeji. Hili nalo unahitaji tuition? Acha kuaibisha walimu waliokufundisha, vinginevyo kama ulifaulu kwa kukariri.
 
Madaktari wa TZ kuweni makini na maisha yenu, msije mkaletewa Mungiki ikala kwenu!
Kuna zaidi ya madaktari 3,000 Tanzania wako mitaani jobless. Kwa miaka 2 sasa hatujaajiri madaktari kwani hatuna uhaba nao, na vyuo vyetu vikuu vinaendelea kufyatua madaktari 2,000 per annum.

Hivyo hiyo ni neema kwao. Usalama wao definately serikali ya Kenya itaulinda. Msiwaogopeshe. It is a good opportunity for them. Acha vijana wetu wakafanye kazi Kenya. Kwanza huo mshahara waliougomea medics wa Kenya ni mara tatu ya mshahara ambao tungewalipa sisi kama tungewaajiri. Na tumeshindwa kuwaajiri kwani nafasi zimejaa na wage bill yetu inatumia almost 55% ya makusanyo ya TRA.

Hata sisi wakati wa mgomo wa akina Dr Ulimboka tulitishia kuwatimua madaktari wote waliokuwa kwenye mgomo na nafasi zao zilikuwa zichukuliwe na madaktari toka China. Tishio hilo ndilo lilimaliza mgomo. Serikali si ya kuchezea. Wakenya wamechelewa sana kuchukua hatua hiyo, hivyo wagonjwa wengi wasio na hatia wamepoteza maisha ambao wangepona kwa kupata huduma za kitabibu. Vijana wetu waende kuokoa maisha ya ndugu zetu Wakenya. Undungu ni kusaidiana kwenye matatizo. Ndiyo ushirikiano wa EAC unaopaswa kuwa. Kwa miezi 4 Wakenya wamekuwa wakipukutika kwa kukosa madaktari wakati sisi tuna ziada ya madaktari wako jobless mitaani. Hii siyo vizuri.
 
Naipongeza hatua hii; watanzania wapate ajira. Pamoja na hayo, vyeti viwekwe mezani vihakikiwe kwanza wasije wakatutia aibu huko. [HASHTAG]#WekaChetiMezani[/HASHTAG]
 
Dakatri mwenye akili hawezi kukubali offer ya aina hiyo maana mbali na kusaliti madaktari wenzake lakini pia anahatarisha maisha yake.
 
Ila hapa naona Tanzania wakifaidi sana iwe kwamba mpango huu utaendelea. Vipi madaktari watz wataajiriwa wote Kenya na Tanzania?? Naona hapa noma sana
Tanzania si wanabana matumiz bado, graduate wanakaa mtaan miaka 2 hafu upate gape nje ujishauri kisa Tanzania hii ya wivu na matamko? Binafsi nashauri waende wakpata nafasi maana hapa kwetu dharau nying sana ktoka kwa wanasiasa! Ifke muda waone muhm wao, hapa kwetu wamekalia uhakiki watumishi hewa mwaka mzma ***** kabsa! Vjana wameumia mpaka basi hafu bado hawajui hatima yao, hawa wanasiasa wamekalia matamko tu! Vjana nendeni aisee! Tz nao watachukua wakenya waliogoma waje wawape mshahara wanaotaka!
 
Wakenya Tanzania kwao ni sebuleni.Mbona wakianzisha vurugu wao ndio watapata hasara? Manake huku Tanzania wamejaa wengi sana na tunaishi kama ndugu!
 
Let me warn the TMA members that the Kenyans are very difficult and dangerous people to work with. You will end up being murdered. So never accept that deal please
Acha kudanganya, mtu Hana ajira aendelee tusubili tu?, acha wakatafute hujui kuna wahitim wengi wapo kitaa na hawana ajira, I Hali Zahanati zetu hazna ma Dr?,eti bado tunakagua vyeti feki, wengine wachukua lkz 2months,
 
tukija kufanya kazi huko mtatupatia ulinzi?
 
So now the government is admitting to spying on Unions ?
 
Tatzo kila kitu watu wanaingza siasa, hakuna kitu kinachonikera kama kuleta ccm na chadema kwenye vitu muhimu vya maisha ya watu, ccm na chadema zkae pemben ktk mambo muhm kama haya, usenge wote unaoendelea chanzo ni kuweka mambo ya ccm vs chadema, ss ni watanzania tunaohtaj mahtaj muhm na sio chama cha siasa!
 
Serikali ya Kenya imesema itawafuta madaktari wote kazi wasio report kazini baada ya masaa 12 ,imesema itaajiri Madaktari kutoka Tanzania nawashairi Madaktari changamkieni ajira
 
Kwa sasa tanzania Kuna madaktari zaidi ya 1500 wako mtaani,toka 2015 hii fursa njema kesho tunasubiri ajira hiyo hao wapumzike tu,it's not ethically patient die in pain while their fellow standing aside and look!!! its brutality,
 
Serikali ya Kenya imesema itawafuta madaktari wote kazi wasio report kazini baada ya masaa 12 ,imesema itaajiri Madaktari kutoka Tanzania nawashairi Madaktari changamkieni ajira
hapo umesema vyema tunahamu kubwa kuwahudumia ndugu zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…