Kuna zaidi ya madaktari 3,000 Tanzania wako mitaani jobless. Kwa miaka 2 sasa hatujaajiri madaktari kwani hatuna uhaba nao, na vyuo vyetu vikuu vinaendelea kufyatua madaktari 2,000 per annum.
Hivyo hiyo ni neema kwao. Usalama wao definately serikali ya Kenya itaulinda. Msiwaogopeshe. It is a good opportunity for them. Acha vijana wetu wakafanye kazi Kenya. Kwanza huo mshahara waliougomea medics wa Kenya ni mara tatu ya mshahara ambao tungewalipa sisi kama tungewaajiri. Na tumeshindwa kuwaajiri kwani nafasi zimejaa na wage bill yetu inatumia almost 55% ya makusanyo ya TRA.
Hata sisi wakati wa mgomo wa akina Dr Ulimboka tulitishia kuwatimua madaktari wote waliokuwa kwenye mgomo na nafasi zao zilikuwa zichukuliwe na madaktari toka China. Tishio hilo ndilo lilimaliza mgomo. Serikali si ya kuchezea. Wakenya wamechelewa sana kuchukua hatua hiyo, hivyo wagonjwa wengi wasio na hatia wamepoteza maisha ambao wangepona kwa kupata huduma za kitabibu. Vijana wetu waende kuokoa maisha ya ndugu zetu Wakenya. Undungu ni kusaidiana kwenye matatizo. Ndiyo ushirikiano wa EAC unaopaswa kuwa. Kwa miezi 4 Wakenya wamekuwa wakipukutika kwa kukosa madaktari wakati sisi tuna ziada ya madaktari wako jobless mitaani. Hii siyo vizuri.