Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Ndugu zangu kama una rafiki au ndugu maeneo ya Itumbi Wilayani Chunya hapa kwetu Mbeya jaribu kumjulia hali mara kwa mara sababu mji umevamiwa na Kipindupindu.
Taarifa zilizopo japokuwa Mamlaka haijaweka wazi ni kuwa kuna zaidi ya Watu 10 wahofiwa kupoteza maisha kwa ugonjwa huo katika Mji wa Matundasi na Itumbi hapo Chunya.
Nimefuatilia na kubaini kuwa changamoto kubwa ni uchafu wa mazingira, wachimbaji wengi madini wanajisaidia vichakani kutokana na kukosekana kwa vyoo katika mazingira yao ya uchimbaji.
Mtu anatoka zake kwenye mgodi anashusha mzigo wa kinyesi kichakani na haya masika yaliyoanza hivyo kinyesi kinatapakaa kwenye makambi yao na kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Serikali lioneni hili siyo mnakumbuka kuwapa leseni tu za uchimbaji bila kuangalia vitu muhimu kama vyoo maeneo yao ya kazi.