Serikali ya Mbeya ituambie kuhusu uwepo wa Kipindupindu maeneo ya Itumbi - Chunya inadaiwa Watu wanapoteza maisha

Serikali ya Mbeya ituambie kuhusu uwepo wa Kipindupindu maeneo ya Itumbi - Chunya inadaiwa Watu wanapoteza maisha

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Ndugu zangu kama una rafiki au ndugu maeneo ya Itumbi Wilayani Chunya hapa kwetu Mbeya jaribu kumjulia hali mara kwa mara sababu mji umevamiwa na Kipindupindu.

Taarifa zilizopo japokuwa Mamlaka haijaweka wazi ni kuwa kuna zaidi ya Watu 10 wahofiwa kupoteza maisha kwa ugonjwa huo katika Mji wa Matundasi na Itumbi hapo Chunya.

Nimefuatilia na kubaini kuwa changamoto kubwa ni uchafu wa mazingira, wachimbaji wengi madini wanajisaidia vichakani kutokana na kukosekana kwa vyoo katika mazingira yao ya uchimbaji.

Mtu anatoka zake kwenye mgodi anashusha mzigo wa kinyesi kichakani na haya masika yaliyoanza hivyo kinyesi kinatapakaa kwenye makambi yao na kusababisha mlipuko wa magonjwa.

Serikali lioneni hili siyo mnakumbuka kuwapa leseni tu za uchimbaji bila kuangalia vitu muhimu kama vyoo maeneo yao ya kazi.
 
Ila kwa uchafu ule wa Mbeya na ustaarabu wa kishamba lazima kipindupindu kisiishe
 
Wachimbaji wote wawe na kikoleo cha kuchimbia "choo."

1730725142821.jpeg
 
Nadhani mwenye Jukumu la kutangaza kuwepo ama kutokuwepo Kwa huo mlipuko ni RC Kwa level ya Mkoa ama DC baada ya kushauriana na Kamati yake ya Usalama.

Ila nafikiri Kuna haja Wananchi kuendelea kuhamasishwa kuhusu Matumizi bora ya Choo pamoja na usafi wa mazingira.

Maana kiuhalisia, Ugonjwa wa Kipindupindu unatokana na Uchafu.

Sasa Sina hakika kama suala la vyoo bora pamoja na usafi wa mazingira vinapewa kipaumbele na wale wachimbaji wa Madini kule Itumbi hadi kule Makongolosi
 
Kabisa
 
Back
Top Bottom