Serikali ya mtaa imenilima faini ya elf 50, kisa sijafanya usafi

Usafi ni ustaarabu wa Maisha, umekushinda wewe basi waelimishe wapangaji wako....

Alafu kesi ikiisha wafukuze usiendelee kuwa karibu na watu wasio wastaarabu na wachafu
Maeneo gani hayo
Mkuu watimue tu wape notice

Ova
mikataba yao haijaisha, naomba solution la hii pesa mkuu nadaiwa 50k
 
Waambie mkamalizane mahakamani uonyeshe hapo kwenye mkataba ulipoandika mpangaji atahusika na usafi wa kufyeka nyasi kuzunguka ntumba...
 
Tena wakuongeze
 
nikushauri...........
Je,kuna mkataba wa upangishaji unaoeleza masharti ya nyumba hio,je unapatikana?,Ikiwa mkataba upo, tafadhali hakikisha unajumuisha kipengele cha usafi wa majani na maeneo ya nyumba ambayo wapangaji wanapaswa kuyahudumia. Kipengele hiki ni muhimu ili kuepuka matatizo ya usafi yanayoweza kuathiri mazingira na kuleta malalamiko kutoka kwa mamlaka za manispaa.

KAMA IPO ... FANYA HIVII...
Ikiwa wapangaji Hawataki kutekeleza wajibu wao wa usafi, hakikisha unatoa notisi rasmi ya kuondoka kulingana na masharti ya mkataba na sheria za manispaa. kuhusu usafi, vinginevyo kosa ni lako huwajibiki kutunza mazingira lipa hio pesa ,ongeza sheria hio ya usafi kwenye mikataba yao ya pango
 
Leo tutagombana sana mkuu na wapangaji sababu ni wabishi kulipa pesa hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…