KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Yote hayo aliweza kuyafanya huku aliimba yeye ni rais wa wanyonge!Wana JF tunatafutiana ban za lazima sasa hivi kujifanya hamnazo na kujisahaulisha.
Hakuna kiongozi aliotupa wakati mgumu kimaisha kama John Joseph Pombe Magufuli. Mambo alivyoyavuruta na kutuburuza nayo kama taifa yule mzee hayaelezeki.
Hakubakisha mtu salama, kuanzia Wakulima wa Korosho, Wauza Midosho, Wafanyabiashara, Wastaafu, Walimu, Wafanyakazi wa Umma, Wanafunzi kwenye Riba Za Mikopo, Madereva kwenye Mikeka ya trafic, Wachimbaji Wadogo na Wakubwa wa Madini, Mashirika ya Ndege kama Precison Air + Fast Jet.
Na kuna watu hadi sasa wanamsifu juu ya maneno hayo, hata kama vitendo vilikuwa zero!