Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,683
- 14,060
Ili kuepukana na gharama za ununuzi wa magari ya ghali kila mwaka kwa ajili tu ya kusafirishia viongozi mbalimbali ni vyema sasa serikali ikaja na utaratibu mpya.
Nina shauri serikali kuanza kununua minbuses maalumu kwa ajili ya kubebea viongozi katika safari kama ziara mbalimbali ili kuepuka utitri wa magari katika misafara na gharama za ununuzi wa magari ya kifahari.
Serikali ya Uchina wamekuwa na utaratibu huu wa kusafirisha wajumbe wa bunge la watu wa China katika vikao vyao pia katika ziara mbalimbali za katibu wa chama cha kikomunisti cha Uchina na Rais wa nchi hiyo Xi jinping ameonekana mara kwa mara akitumia usafiri huu katika nchi ya China.
Huyu ni katibu wa chama cha kikomunisti cha China na Rais wa China Xi jinping akitumia Minbus katika moja wapo wa ziara ndani ya China pamoja na viongozi wenzake.
Ni vyema sasa serikali ikatazama suala hili kwa namna ya pekee ili kuepukana na hali kama hii