DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
"Waacheni wananchi watoe yaliyomo vifuani mwao kwa uhuru. Kwa kufanya hivyo itatusaidia sisi kama Serikali kwa namna mbili; Kwanza, tutajua wananchi wetu wanafikiria nini kuhusu jambo fulani. Pili, itatusaidia sisi kama Serikali iwapo tumekosea tuweze kujisahihisha na kuendelea kuwakelea maendeleo wananchi wetu" Mhe RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, Agosti 12, 2021.
Usuli
Ijumaa, Aprili 10, 2026, Mhe Paul Christian Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliusimamisha Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) uliokuwa umepangwa kufanyika Aprili 12, 2026, akausimamisha Uongozi wa sasa wa TOC kisha akaunda Interim Committee kwa maelezo kuwa kuna wagombea hawakutendewa haki kwenye mchakato wa Uchaguzi wa TOC.
Maswali chechefu:
1. Je, kwanini Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) umekuwa ukipigwa danadana mara kwa mara ?
1.1 Uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika Desemba 2024 lakini haukufanyika kisha ukatakiwa kufanyika Oktoba 4, 2025 lakini pia haukufanyika na ukapangwa kufanyika Aprili 12, 2026 lakini umepigwa pini tena.
2. Je, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo haioni kuwa kwa kusimamisha uchaguzi huo inakuwa imeiingilia TOC, kitu ambacho kinakatazwa na IOC Charter ?
2.1 Kifungu cha 27.9 cha IOC Charter kinakataza Serikali kuingilia mambo ya National Olympics Committees (NOC). Aidha, Sera ya IOC ni kuwa hizi NOC ziwe huru (autonomous) na kufanya chaguzi zake bila kuingiliwa:
"The Olympic Charter states that National Olympic Committees shall enjoy the right of elections free from any outside influence".
3. Je, Serikali haioni kuwa kwa uamuzi wake huo, ambao ni dhahir shahir umeiingilia TOC, kuna hatari ya TOC kufungiwa na IOC ?
4. Je, Serikali haijui kuwa kuna mataifa mengi yamelia na kusaga meno kutokana na Serikali kuzingilia NOC ? Mifano ipo bwerere, itoshe kutaja michache:
4.1 POC ya Panama ilisimamishwa na IOC baada ya Serikali ya Panama kuiingilia POC mwaka 2007;
4.2 KOC ya Kuwait ilifungiwa mara mbili na IOC (2010 & 2015) baada ya Serikali kuingilia KOC;
4.2 OIC iliisimamisha India mwaka 2012 baada ya Serikali ya India kuingilia uchaguzi wa India Olympic Association (IOA) na kuidharau OIC Charter.
4.3 Mwaka 2011, OIC iliisimamisha GOC ya Ghana baada ya Serikali ya Ghana kuingilia autonomy ya GOC.
4.4 Mwaka 2022, OIC iliisimamisha National Olympic Committee (NOC) ya Guatemala kwa kuingilia uchaguzi wa NOC.
4.5 Mwaka 2008, IOC iliisimamisha National Olympic Committee ya Iraq baada ya Serikali ya Iraq kuingilia kati na kuivunjilia mbali National Olympic Committee na kuiinjika Kamati ya muda (Interim Committee). IOC ilisema kitendo hicho ni kinyume na IOC Rules on autonomy zinazotiwa mkazo na IOC Charter. Serikali ya Tanzania ilichokifanya jana kinashabihiana na kilichofanywa na Serikali ya Iraq mwaka 2008.
5. Je, Serikali haijui kuwa IOC ni kama FIFA na vyombo hivi havinaga msalie- mtume Serikali zinapoingilia vyama vya michezo vilivyo chini yao ?
5.1 Oktoba 27, 2000, FIFA iliisimamisha Football Association of Tanzania (FAT) baada ya Serikali kuyatimba. Julai 2000, Serikali iliun'goa Uongozi wa FAT chini ya Mwenyekiti wa FAT Muhidini Ndolanga na Katibu Mkuu Ismael Aden Rage kwa madai ya ubadhilifu na uchaguzi ukaitishwa.
Agosti 2000, FIFA ilieleza kuwa kitendo hicho ni haram kwani kinaingilia autonomy ya FAT na ikagoma kuutambua uchaguzi wa viongozi wa FAT uliofanyika Agosti 6, 2000 Idodomia na ikataka uchaguzi mpya ufanyike na normalization committe iundwe na iwe chini ya Mhe Ndolanga ili kuongoza michezo badala ya viongozi wapya. Serikali, kupitia Jenerali Ulimwengu, aliyekuwa Mwenyekiti wa BMT, ikaona huu sasa utani, ikadinda ndipo FIFA ikaisimamisha FAT.
5.2 Rais Benjamin Mkapa alilazimika kuunda timu ya Mawaziri 3 (Prof Philemon Sarungi, Prof Juma Kapuya & Mhe Anna Abdallah) ili kuangalia namna ya kufanya ili FIFA iondoe kusimamishwa kwa FAT. Kamati hiyo ikachutama mbele ya Mhe Ndolanga na wakayajenga kwa msingi wa Let the bygones be bygones.
Msafara mzito ukatinga FIFA HQ Zurich, Switzerland. Msafara huo uliongozwa na Prof Kapuya . Wengine walikuwa ni Henry Ramadhan, Leodgar Tenga, Idd Kipingu na Mohammed Misanga. Prof Kapuya, ambaye mwaka 2000 aliipiga mkwara FIFA kuwa "Tanzania ni nchi huru ambayo ina "Sovereignty" yake na yenye mamlaka ya kuhakikisha mambo ya Michezo yanaenda vizuri bila kuingiliwa na FIFA" na ambaye Novemba 27, 2000 alichimba tena mkwara kuwa "Tanzania haitageuka jiwe, tutajitoa FIFA", akawa mdogo hata piriton ikasome !
Akaieleza FIFA kuwa Tanzania iko tayari kutekeleza maagizo ya FIFA. FIFA ikaifungulia FAT toka Lupango Machi 2001 na ikaagiza uchaguzi mpya. Uchaguzi ukarudiwa Novemba 2001 kama FIFA ilivyoagiza na Mzee-Mzima Ndolanga returned to the Federation as the Chairman- home and dry !
6. Je, Mhe Waziri hajabaini kuwa amekinzana na Sera ya Maendeleo ya Michezo 1995 na Sheria ya Baraza la Michezo Sura ya 49 RE 2023 zinazomtaka kuhakikisha Taasisi zote zilizo chini ya Sekta ya Michezo zinafuata Sheria ? Au kwa maneno mengine; Kwakuwa Mhe Waziri ameeleza kwamba imebidi aingilie kati kwavile kuna wanachama wamelalamika wameenguliwa na kunyimwa haki za msingi, je, Sheria inampa mamlaka Mhe Waziri kuingilia au kuna hatua ya Kisheria wagombea hao walipaswa kuifuata ?
6.1 Sheria inawaruhusu wagombea waonao wameenguliwa kimagumashi kama vile wakinyimwa haki ya kusikilizwa kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa. Na wagombea hao walitumia fursa hiyo ambapo walikata rufaa na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa, Bw Richard Sinamtwa, alitupilia mbali rufaa yao Aprili 6, 2026.
6.2 Kwa akili zangu ndogo za kuungaunga kwa gundi ya Cellotape, naamini hatua waliyopaswa kuchukua baada ya rufaa yao kutupwa, ni kwenda Court of Arbitration for Sport (CAS) na si kulalamika kwa Waziri. Aidha, Waziri hana mamlakana ya kuingilia kati na kuunyofoa uongozi uliopo na kuuinjika mwingine wa muda. Hatua muafaka ni CAS. Ni sawa na Simba ikikosa kuridhishwa na Kamati ya TFF kuhusu suala la Msukuma Mohammed Damaro Camara iende kwa Waziri wa Habari nae aunyofoe Uongozi wa Kamati hiyo na kuweka mwingine badala ya Simba kwenda CAS !
7. Je, Serikali inaamini kuwa kwavile Kifungu cha 27 cha Sheria ya BMT kinasema uamuzi wa Waziri ni wa mwisho maana yake ni kuwa IOC haiwezi kuingilia na kuupiga chini ?
7.1 TOC iko chini ya IOC hivyo hakuna kifungu chochote kiwezacho kuizuia IOC kuingilia TOC iwapo itahisi kuna madudu yamefanyika.
8. Je, iweje, hata kama ni kuunda Kamati (kitu ambacho so sahihi), Mhe Waziri aunde Kamati iliyo ya Wanasoka mf Ismael Aden Rage, Jemedari Saidi? Mbona Taifa letu lina Wabobevu wengi wa Riadha ambao wangefaa ? Cha ajabu, Bw Ismael Aden Rage aliyekuwepo kwenye Msala wa FIFA 2000, ndiye Mwenyekiti wa Kamati hii !
9. Je, Serikali haioni iko hatari nchi yetu ikakosa michuano ya Commonwealth Julai 23, 2026- August 2, 2026 iwapo IOC itatufungia ?
10. Je, Serikali haioni kuwa hata wanariadha wetu hawatashiriki michuano yoyote ya Kimataifa tukifungiwa?
11. Je, Serikali haijui kuwa kuna Mjumbe wa IOC ambaye anafika leo kwaajili ya Uchaguzi uliokuwa ufanyike kesho (as an observer)? Je, Serikali inaamini kabisa IOC itatuchekea tu kwa hiki kilichofanyika ? Je, Serikali haijui kuwa Uongozi ulioondolewa utaijulisha IOC kuwa "Tumeliwa Vichwa kavukavu bila maji" ?
11. Je, tunazingatia kuwa IOC imekuwa ikifuatilia sana suala la Uchaguzi wetu huu ?
12. Tamati
Kwa Heshima na Taadhima, napenda kutoa Rai kwa Mhe Waziri wa Michezo kuwa ikimpendeza atafakari upya na kwa makini uamuzi wake kwa kuzingatia maelezo niliyoyatoa hapo juu. Uamuzi huu wa kuuondoa Uongozi wa TOC na kuuinjika mwingine ni sawa na Waziri auondoe Uongozi TFF afu auinjike mwingine, ni lazma FIFA wataingia fronti na kutufungia !
Nimelazimika kufanya hivi kutokana na Uzalendo kwa nchi yangu kwani nahofia kinachoweza kutukuta toka IOC.
Hata hivyo, uamuzi ni wa Mhe Waziri iwapo afuate ushauri huu au abaki na uamuzi wake lakini mimi nina amani moyoni kwani nimetekeleza jukumu langu la Kizalendo kwa nchi yangu.
"Mzee wa Atikali" ✍️✍️✍️
Jumamosi, Aprili 11, 2026
0754 744 557
CC: AG