Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
Ila akili za watu wengine we ushaona sehemu ina vita unaenda kufanya nini rudi kwenu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nachojua Documents za mahakama zilizopo mtandaoni hazidanganyi hata kwa kutumia google translate utaona jinsi kesi yake ilivyokuwa ikipigwa tarehe na yeye kubaki rumande.Unataka sema tumedanganywa na MFA au wao ndo wamedanganywa na RF?
Magufuli aliwato...mba sana kwa dole gumba,sio gubu hiloSerikali bado ina roho ya Umagufuli, kwa sababu aligombea ubunge kupitia chadema ndio maana imekuwa kimya. Kidiplomasia tumefeli
Mbowe kuachiwa ile kesi ya Ugaidi na wale makomandoo wa JWTZ serikali ilikuwa sahihiPia, Nemes Tarimo alikuwa mwana CHADEMA na aligombea ubunge 2020 kupitia kwenye Jimbo la Ubungo.
Mungu amweke mahali pema peponi lakini Jambo hili CHADEMA walitakiwa watoe maelezo ya kutosha kilichopelekea mwanachama wao akafungwa miaka 7
Haliyofanya-aliyofanyaFamilie mkadai malipo ya kazi haliyofanya..
NonsenseSerikali bado ina roho ya Umagufuli, kwa sababu aligombea ubunge kupitia chadema ndio maana imekuwa kimya. Kidiplomasia tumefeli
Wakati wa vita kuna fursa piaIla akili za watu wengine we ushaona sehemu ina vita unaenda kufanya nini rudi kwenu.
Na wengi wanaotafuta maisha nje ata akikutana na changamoto hawezi kuwaambia anajua atawatia stress ikiwa uwezo wa kumfikia au kumsaidia haupo, ni hilo limejulikana baada ya kifo chake lakini wapambanaji wanapitia mengi sana.Ina weze kana waliongea nae ktk salamu za mwaka mpya january, na march akakutana na kadhia hiyo
Yes wanaitwa mercenary, yaani askari wa kukodi wanapigana kwaajili ya mpunga changamoto wanakua hawako patriotic na nchi, kama unajiweza kwenye medani rusia inaonekana anahiyo fursa.Wakati wa vita kuna fursa pia
Vita ni biashara pia...moja ya utafutaji pia huko
Ova
Rip Nemes.....kwenda Urusi wakati huu ni hatari mno.Kulingana na ushahidi wa nyaraka za mahakama ya Urusi ambazo jarida la “The Chanzo” imeweka wazi mtandaoni, marehemu hakuwahi kuhukumiwa bali kesi yake ilikuwa ikisogezwa na yeye kubaki jela hadi alipojiunga na kundu la Wagner. Hicho kifungo cha miaka 7 alichohukumiwa mwezi March 2022 si kweli kulingana na documents za mahakama zilizopo mtandaoni.
StupidNonsense
Na yeye analipa kwenye moto wa mileleMagufuli aliwato...mba sana kwa dole gumba,sio gubu hilo
Naunga mkono hoja hii...alichofanyiwa Nemes na wafungwa wengine na kundi la Wagner ni ukatiliifike kipindi Watanzania tuone kuwa Urusi haina maana kwetu, kwanza haitusaidii na kitendo cha kutaka wafungwa waende vitani ni cha kikatili sana. uhai wa Mtanzania mmoja unatakiwa kuthaminiwa na serikali ionyeshe msimao katika hili.
ukiangalia hata hivyo, hata kama wamgaribi wana mambo ya dhambi na ujinga mwingi, ila wana faida zaidi kwetu kuliko urusi, wanatoa misaada mingi kuliko urusi. hivi ukiuliza hapa bongo mrusi amefanya nini kwa Tanzania, utataja nini? au tunawaweka kama reserve tukihitaji silaha watuuzie? au nini yaani faida yao kwetu? imagine mtu yupo gerezani, wanamwambia aende vitani, unyama gani huo? hata wamagaribi hawawezi kufanya icho kitu. ina maana urusi ana wanajeshi wachache kiasi gani hadi ahitaji mamluki wa aina hiyo? ana uhitaji wa wanajeshi sana kumbe? si walikuwa wanajifanya taifa imara? mbona sasa linafanya vita za kishamba sana.Naunga mkono hoja hii...alichofanyiwa Nemes na wafungwa wengine na kundi la Wagner ni ukatili
Sawa kufa ukiwa una jaribu si vibayaWaziri wa Mambo ya Nje, Stergomena Tax amesema Mtanzania aliyefariki Dunia Nchini Urusi, Nemes Tarimo alikuwepo nchini humo kwa ajili ya masomo na alijiunga na Chuo cha Moscow Technology Pro mwaka 2020 kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya 'Business Informatics'.
Waziri amesema taarifa ambazo Serikali imezipokea ni kuwa mwezi Machi 2022, Mtanzania huyo alikuhumiwa kifungo cha miaka saba gerezani kwa mujibu wa Sheria za Urusi kutokana vitendo vya uhalifu.
Ameongeza kuwa akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi kilichopo nchini humo kinachofahamika kama Wagner akihadiwa kulipwa fedha lakini pia kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita ambapo inadai kuwa alikubali kujiunga na kikundi hicho.
Ikumbukwe kauli ya Waziri siku chache baada ya kuibuka taarifa zilizodai uwepo wa Mtanzania aliyefia Nchini Urusi akihusishwa katika mapigano ya vita vya baina ya Urusi na Ukraine ambavyo vimedumu kwa muda.
Familia ya Nemes Tarimo ilithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa wanasubiri mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya maziko.
Aidha, kwa mujibu wa familia hiyo alifariki mwishoni mwa mwezi Oktoba 2022 na kwamba taarifa ya kwanza walipatiwa na marafiki wa karibu mwishoni mwa mwezi Desemba 2022 kuwa kijana wao amefariki lakini baadae walidai kupata taarifa rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, Urusi.
Pia soma:
Safari ya kuusafirisha mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo kutoka Urusi hadi Tanzania inaanza 24 Januari, 2023
Tarimo Nemes, anayedaiwa alifariki akiwa vitani Ukraine, aligombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA