Serikali ya Tanzania yatoa msaada Uturuki

Serikali ya Tanzania yatoa msaada Uturuki

Write your reply...VIZURI KUTOA SI UTAJIRI BALI NI MOYO.
 
Mkuu 'Icebreaker', huu mfano siyo sahihi hata kidogo

Hao maskini wa huko ni tofauti sana na wa huku kwetu. Unalinganisha hali mbili tofauti kabisa na katika mazingira ambayo hayafanani kabisa. Mlinganisho huu hauwezekani.
Kule US kuna homeless kubao, yaani masikini hana hata uhakika wa sehemu ya kulala, btw huu msaada si ni kutokana na majanga? Kuna ubaya gani? Yaani mnaongea utafikili umetolewa msaada wa kuwajengea shule?
 
Kama wadau wanavyosema kutoa Ni moyo ila kwakweli kabla ya kutoa tujitafakari,kuna wakati tunasema tunaviongozi wa hili taifa Ni Wa hovyo wafuasi wao wanakasirika.
Juzi tu hapa tumepewa mikopo,juzi mama kapewa msahada wa dola 30000 za kujenga vyooo na madarasa,akasema anaomba wadau wamsahidie pia kuchanga ili kufanikisha zoezi hili,leo nao wanatoa msahada wa dola "1000,000"?
 
Huo ni upendo mshumaa.

Kujitutumua tu wakati uwezo huo hatuna.

Si juzi tu hapo tumekopa ili tujenge vyoo.
Hii ni diplomasia, siku uki negotiate ufutiwe tariffs za billions unashangaa wanalainika na kukubali!! That's diplomacy.
 
Kama wadau wanavyosema kutoa Ni moyo ila kwakweli kabla ya kutoa tujitafakari,kuna wakati tunasema tunaviongozi wa hili taifa Ni Wa hovyo wafuasi wao wanakasirika.
Juzi tu hapa tumepewa mikopo,juzi mama kapewa msahada wa dola 30000 za kujenga vyooo na madarasa,akasema anaomba wadau wamsahidie pia kuchanga ili kufanikisha zoezi hili,leo nao wanatoa msahada wa dola "1000,000"?
Ugiriki mpaka ikabidi iokolewe na wenzie maana nchi ilitaka kupigwa mnada kabisa!! Ila Bado Wanatoa misaada Kila mwezi huku Africa.

Ile ni diplomasia, Ili siku ukihitaji favor basi utapewa first priority.

Mimi binafsi nliwahi samehe Hela Fulani nikiwa chuo Sasa Kuna siku nikakwama ada, yule jamaa alinipa mara mbili ya Ile pesa nikamalizia ada. So Kuna wakati favors zinaweza kukuokoa huko mbele hata kama hauna Hela.
 
Ajabu ni kwamba hata sisi bado tunaomba misaad kila siku halafu tukija huku tunajifanya dona kantree, hiyo hela tungetumia kupunguza deni la Taifa aisee badala ya kujivimbisha kutoa misaada

Tanzania haijatoa msaada ili ijionyesha imetoa kama sehemu ya kuwashika pole marafiki zetu wa Uturuki, Tanzania haijaanza leo kutoa msaada.

Rais Mkapa aliwahi kufanya hivyo kwa Burundi pia hii ni Diplomasia.

Haimaanishi ukiomba msaada huwezi kusaidia wengine.!
 
Duu hata Malawi juzi wamekula bonge la msaada aisee inaeelekea naishi kwenye nchi TAJIRI ila sijijui
Hutasikia wametoa msaada ndani humu hata bima ya afya bure inawezekana ila hawataki
 
EeenHeee!

Kama "kutembea"kwako matokeo yake ndiyo haya unayoandika hapa, ya kupotosha watu; mimi sihitaji kutembea kwa namna hiyo.

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Safiii tena tuwaongezee jamani wamewachongeshea dadazetu matako yaukweli sana ukitizama mguu mdogo unatetema kimayele dah.

Uturuki wanaakili na teknolojia nzuri hata biblia inawatambua,tuwaweke karibu watatufaa kuliko matajiri wasiotaka tuendelee.

Pia tukumbuke bilioni tano nipesa ya mboga kutoa rambirambi ni ustaarabu!! Jiwe asingewaza hili HEKO MAMA NAKULAVU SANA
 
Tanzania yatoa msaada wa Dola za Marekani 1,000,000 kwa Uturuki kufuatia madhara ambayo nchi hiyo inepata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Februari mwaka huu...
Heee! Bilioni mbili na ushehe, mmepata wapi hizo hela za kuwapa hao matajiri wakubwa. Si ndio hao wanaojenga reli ya SGR kwa matrilioni mengi na upigaji mwingi tu?! Je, watoto wetu wote wama madawati?...
 
Ugiriki mpaka ikabidi iokolewe na wenzie maana nchi ilitaka kupigwa mnada kabisa!! Ila Bado Wanatoa misaada Kila mwezi huku Africa...
Mzee tunaitaji pesa ya kumalizia miradi,Mambo hayaendi ugumu na mfumuko wa vitu uko juu,Mama anatoa pesa anagawa kweli?
 
Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, msemaji wa serikali ameandika:

"Tanzania yatoa msaada wa Dola za Marekani 1,000,000 kwa Uturuki kufuatia madhara ambayo nchi hiyo inepata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Februari mwaka huu."
Gerson Msigwa.


20230324_131333.jpg
 
Maisha kusaidiana sio mbaya, Leo wao kesho sisi.
 
Na sisi pia tumepewa msaada wa kujenga barabara na Mzungu...so who are we
 
Back
Top Bottom