Serikali ya Tanzania yatoa msaada Uturuki

Serikali ya Tanzania yatoa msaada Uturuki

Donor country imetia hongera JPM.
Kweli ndoto ya JPM ya Tanzania kuwa Donor Country, Dr Salmia ameifanikisha. Hongera sana mama. USD 1,000,000 ni sawa na TZS 3 billion.

Huko Malawi thamani ya chakula tulicho wasaidia ni zaidi ya hiyo. Huo ni mwanzo tu. Tumeanza kuwapelekea jirani zetu gesi ya bei nafuu ili kuwapunguzia makali ya maisha ili waachane na maandamano yasiyokuwa na kikomo.

Tumewadhamini jirani zetu baada ya benki kuu yao kuishiwa dollars za kununulia mafuta ya petroli na dizeli ili kuwaepusha na janga la nchi kukosa nishati hiyo.
 
Unajua hata tusingetoa hao wenyewe wangetuelewa tu maana wanajua hali yetu.
Hapana.
Hawa wasingejua hali yetu ya umaskini, ila ninayo hakika wanajua hali yetu ya upumbavu wa nchi yenye neema kubwa kabisa kuwa na viongozi wasiojuwa kuwaongoza wananchi wao wautumie utajiri wao mkubwa kuondoa umaskini wa kutupwa.

Wanajuwa vizuri sana, tulivyo na viongozi wanaofuja mali za wananchi.

Kwa hiyo, wao kupewa dola milioni moja haiwastuwi hata kidogo, kwani wanajua vilevile, hata wakiikataa hela hiyo itaishia kwenye kufujwa tu haitafanya kazi yoyote ya maana kuwasaidia wananchi.

Nitakubaliana nawe, kama utashauri wachukue hiyo hela, halafu wao waje watujengee vsima vya maji huko vijijini kwa kuitumia hela hiyo hiyo.
 
Kule US kuna homeless kubao, yaani masikini hana hata uhakika wa sehemu ya kulala, btw huu msaada si ni kutokana na majanga? Kuna ubaya gani? Yaani mnaongea utafikili umetolewa msaada wa kuwajengea shule?
Utakuwa ni mmoja wa wasioweza kutofautisha hao maskini wa Marekani na maskini tulio nao hapa Tanzania.
Labda panatakiwa itolewe elimu kuhusu hili jambo hapa JF ili muweze kuwa na uelewa huo.

Utajiri ilionao serikali ya Marekani unaweza kumhudumia wote hao 'homeless kibao' unaowazungumzia wewe.
Serikali ya Tanzania leo hii hata itake, haina uwezo wa kumfanya kila mTanzania awe na sehemu ya kulala! Hili liko wazi.

Hao unaowaita 'homeless kibao' Marekani, wengi wao kwa sababu mbalimbali wanaamua wenyewe kuwa na maisha hayo, pengine hata kwa kutotaka tu masharti yanayotolewa na serikali kuwa na mahali pa kulala. Mahali pa kulala papo, lakini walengwa hawataki masharti yanayoendana na kupewa makazi hayo. Baadhi ya hawa watu ni wagonjwa wa akili au waathirika wa madawa ya kulevya.
Hapa Tanzania, tunao maskini wengi, ambao umaskini wao unatokana na ufinyo wa fursa za kuwaondolea umaskini wao. Hawataki kuwa maskini, lakini inawalazimu kuwa na hali hiyo kwa kukosa fursa.

Tafadhali, naomba unielewe vizuri, sijasema kuwa Tanzania ikiwa na utajiri ilionao Marekani hapatakuwepo na 'Homeless kibao". Hilo litategemeana na sera za nchi husika jinsi ya kuwahudumia wananchi wake wote, na pengine utamaduni wa nchi husika.

Ngoja niulize swali, kwa sababu sijui jibu lake: Hivi Saudi Arabia kuna 'homeless'? Hivi Sweden, Austria, Norway kuna 'homeles' na maskini wa kutupwa kama Tanzania?

Nchi zote hizi nilizozitaja hazina utajiri kumzidi Marekani, kwa hiyo, swali langu lina aina ya jibu kuonyesha kwamba maskini wa Tanzania, kamwe huwezi kumlinganisha na maskini wa Marekani.

Kama bado hujanielewa, ningeomba labda umwite pia rafiki yangu ninayemheshimu sana, mkuu 'zitto jr', ambaye naona kakubaliana na hoja yako hapo juu kwa kukupa 'like'.

Tafadhali, mwite zitto jr aje asaidie.
 
Kweli ndoto ya JPM ya Tanzania kuwa Donor Country, Dr Salmia ameifanikisha. Hongera sana mama. USD 1,000,000 ni sawa na TZS 3 billion.

Huko Malawi thamani ya chakula tulicho wasaidia ni zaidi ya hiyo. Huo ni mwanzo tu. Tumeanza kuwapelekea jirani zetu gesi ya bei nafuu ili kuwapunguzia makali ya maisha ili waachane na maandamano yasiyokuwa na kikomo.

Tumewadhamini jirani zetu baada ya benki kuu yao kuishiwa dollars za kununulia mafuta ya petroli na dizeli ili kuwaepusha na janga la nchi kukosa nishati hiyo.
Dah!

Naomba hii aione mhusika.

Lakini fahamu kwamba hii nchi sasa milango yake yote na madirisha, na hata kupitia darini,"IPO WAZI"!
 
Tanzania yatoa msaada wa Dola za Marekani 1,000,000 kwa Uturuki kufuatia madhara ambayo nchi hiyo inepata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Februari mwaka huu.

Hii ni mara ya pili Tanzania kufanya hivyo baada ya majuzi kuwasaidia marafiki zetu wa Malawi [emoji1156] waliokumbwa na Kimbunga kilichosababisha maafa.

Tanzania inarejea enzi za Mwalimu Nyerere ilipokuwa mstari wa mbele kulikomboa Bara la Afrika.
Nchi yetu ni tajili
 
..mbona jamaa wa Kituruki aliyepokea hundi anaonekana msela-msela?

..tuna uhakika huo msaada umewasilishwa mahali panapohusika?
 
Dah!

Naomba hii aione mhusika.

Lakini fahamu kwamba hii nchi sasa milango yake yote na madirisha, na hata kupitia darini,"IPO WAZI"!
Na mahindi, mchele na maharage yetu tumekuwa tukiwauzia majirani zetu hao kwa bei ndogo hadi kupelekea bidhaa hizi kuwa za aghali zaidi kuliko za huko kwao. Tulipositisha wakaanza maandamano ya kupinga bidhaa hizi kupanda zaidi bei.
 
Wanabodi habari zenu!!

Moja KWA moja niende kwenye mjadala, kuna habari za uhakika kuwa sasa Tanzania imerejea rasmi katika nafasi yake kwenye uwanja wa kimataifa.

Na hii inachagizwa baada ya Rais SAMIA SULUHU Hassan kuridhia Msaada wa Kifedha kuwasaidia wananchi wa UTURUKI kutokana na tetemeko la ardhi lililowakumba.

Katika diplomasia,daima kuna mahusiano ya nchi na nchi katika ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali.

Moja ya nyanja hizo ni katika maafa na vita on reciprocal basis.Uturuki imepata maafa na serikali imeamua kutoa Msaada.

Pamoja na kwamba inazo changamoto nyingi za ndani ikiwemo mfumuko wa bei ya bidhaa bado serikali imeona vyema kushirikiana na wenzetu katika nyakati ngumu.

Msaada wa zaidi ya bil 2 za kitanzania ni sehemu tu ya moyo wa upendo wa nchi yetu KWA waturuki.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amebainisha hayo.Jambo hili ni jema mbele za Tanzania,UTURUKI na mbele za Mungu.

Kwa hapo acha tuseme Rais wetu Dr SAMIA SULUHU Hassan ameupiga mwingi.

Nasemaje mnyonge mnyonge Iakini haki yake mpeni.

Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki UTURUKI

Nawasilisha
 
Tanzania yatoa msaada wa Dola za Marekani 1,000,000 kwa Uturuki kufuatia madhara ambayo nchi hiyo inepata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Februari mwaka huu.

Hii ni mara ya pili Tanzania kufanya hivyo baada ya majuzi kuwasaidia marafiki zetu wa Malawi [emoji1156] waliokumbwa na Kimbunga kilichosababisha maafa.

Tanzania inarejea enzi za Mwalimu Nyerere ilipokuwa mstari wa mbele kulikomboa Bara la Afrika.
"Hii nchi ni tajiri" in magufuli's voice
 
Watu kama sisi tunaojua Ulaya, Tanzania ina uwezo mkubwa wa kusaidia. Wewe fikiria pesa za humo halmashauri zinavyopotea, pesa zinavuja kila kona. Ndiyo maana serikali inaleta mifumo ya kisasa ili kuziba au kuondoa kabisa mifumo ya karatasi mkononi. Imeletwa control namba n.k lakini bado upotevu ni mwingi. Serikali inabidi kuwekeza kwenye mifumo ya ulipaji wa kisasa. Hapo mbele tutaweza kuingia kweye G20
 
Naunga mkono kutoa msaada ni kuimarisha diplomasia pia.
 
Back
Top Bottom