Mbelajr2023
Member
- Nov 23, 2022
- 54
- 115
Nasemaje Tanzania inarudi katika medani za siasa za kimataifa,mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Ahsanteni KWA comment zenu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wahenga walisema kutoa ni moyo si utajiri
Kabisa. Wasindwe na walegeeWanaopinga ni wachoyo! Wapo radhi kuchachiwa na chakula na jirani alale njaa.
Nchi ipo na makuta mingi kila goli milioni 5 wacha tuwape msaada tu!Wanabodi habari zenu!!
Moja KWA moja niende kwenye mjadala, kuna habari za uhakika kuwa sasa Tanzania imerejea rasmi katika nafasi yake kwenye uwanja wa kimataifa.
Na hii inachagizwa baada ya Rais SAMIA SULUHU Hassan kuridhia Msaada wa Kifedha kuwasaidia wananchi wa UTURUKI kutokana na tetemeko la ardhi lililowakumba.
Katika diplomasia,daima kuna mahusiano ya nchi na nchi katika ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali.
Moja ya nyanja hizo ni katika maafa na vita on reciprocal basis.Uturuki imepata maafa na serikali imeamua kutoa Msaada.
Pamoja na kwamba inazo changamoto nyingi za ndani ikiwemo mfumuko wa bei ya bidhaa bado serikali imeona vyema kushirikiana na wenzetu katika nyakati ngumu.
Msaada wa zaidi ya bil 2 za kitanzania ni sehemu tu ya moyo wa upendo wa nchi yetu KWA waturuki.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amebainisha hayo.Jambo hili ni jema mbele za Tanzania,UTURUKI na mbele za Mungu.
Kwa hapo acha tuseme Rais wetu Dr SAMIA SULUHU Hassan ameupiga mwingi.
Nasemaje mnyonge mnyonge Iakini haki yake mpeni.
Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki UTURUKI
Nawasilisha
Gori moja m 5, hii ndio tanga na nyika.Tanzania karibia wote ni maskini.
Ukiangalia orodha ya matajiri wote ni Raia wa nje.
Hakuna mzawa.
Sasa kama spidi ndio hii ya kumwaga tu mahela kila mahali halafu baadae tunakopa kujengea vyoo hiyo sio sawa.
Halafu bajeti ya nchi zaidi ya asilimia 30 ni fedha za mikopo tu.Gori moja m 5, hii ndio tanga na nyika.
Mimi naona tupeleke petition ubalozi wa uturuki ili wa diverge hiyo pesa kwenye visima na zahanati kule vijijini kwetu.Hapana.
Hawa wasingejua hali yetu ya umaskini, ila ninayo hakika wanajua hali yetu ya upumbavu wa nchi yenye neema kubwa kabisa kuwa na viongozi wasiojuwa kuwaongoza wananchi wao wautumie utajiri wao mkubwa kuondoa umaskini wa kutupwa.
Wanajuwa vizuri sana, tulivyo na viongozi wanaofuja mali za wananchi.
Kwa hiyo, wao kupewa dola milioni moja haiwastuwi hata kidogo, kwani wanajua vilevile, hata wakiikataa hela hiyo itaishia kwenye kufujwa tu haitafanya kazi yoyote ya maana kuwasaidia wananchi.
Nitakubaliana nawe, kama utashauri wachukue hiyo hela, halafu wao waje watujengee vsima vya maji huko vijijini kwa kuitumia hela hiyo hiyo.
Mkuu, huu ni mwanzo mzuri wa mchango wa mawazo.Mimi naona tupeleke petition ubalozi wa uturuki ili wa diverge hiyo pesa kwenye visima na zahanati kule vijijini kwetu.
Tunaendelea kujenga matundu ya choo Kwa zile tulizopokea mwaka Jana!Duu hata Malawi juzi wamekula bonge la msaada aisee inaeelekea naishi kwenye nchi TAJIRI ila sijijui
Mama yangu akiwa na pesa utamjua tu huwa hajifichi watoto huwa tunatumwa sana dukani.. ila sikiisha makasiriko bila sababu mtajua hujui..
Tanzania yatoa msaada wa Dola za Marekani 1,000,000 kwa Uturuki kufuatia madhara ambayo nchi hiyo inepata kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Februari mwaka huu.
Hii ni mara ya pili Tanzania kufanya hivyo baada ya majuzi kuwasaidia marafiki zetu wa Malawi [emoji1156] waliokumbwa na Kimbunga kilichosababisha maafa.
Tanzania inarejea enzi za Mwalimu Nyerere ilipokuwa mstari wa mbele kulikomboa Bara la Afrika.