Kule US kuna homeless kubao, yaani masikini hana hata uhakika wa sehemu ya kulala, btw huu msaada si ni kutokana na majanga? Kuna ubaya gani? Yaani mnaongea utafikili umetolewa msaada wa kuwajengea shule?
Utakuwa ni mmoja wa wasioweza kutofautisha hao maskini wa Marekani na maskini tulio nao hapa Tanzania.
Labda panatakiwa itolewe elimu kuhusu hili jambo hapa JF ili muweze kuwa na uelewa huo.
Utajiri ilionao serikali ya Marekani unaweza kumhudumia wote hao 'homeless kibao' unaowazungumzia wewe.
Serikali ya Tanzania leo hii hata itake, haina uwezo wa kumfanya kila mTanzania awe na sehemu ya kulala! Hili liko wazi.
Hao unaowaita 'homeless kibao' Marekani, wengi wao kwa sababu mbalimbali wanaamua wenyewe kuwa na maisha hayo, pengine hata kwa kutotaka tu masharti yanayotolewa na serikali kuwa na mahali pa kulala. Mahali pa kulala papo, lakini walengwa hawataki masharti yanayoendana na kupewa makazi hayo. Baadhi ya hawa watu ni wagonjwa wa akili au waathirika wa madawa ya kulevya.
Hapa Tanzania, tunao maskini wengi, ambao umaskini wao unatokana na ufinyo wa fursa za kuwaondolea umaskini wao. Hawataki kuwa maskini, lakini inawalazimu kuwa na hali hiyo kwa kukosa fursa.
Tafadhali, naomba unielewe vizuri, sijasema kuwa Tanzania ikiwa na utajiri ilionao Marekani hapatakuwepo na 'Homeless kibao". Hilo litategemeana na sera za nchi husika jinsi ya kuwahudumia wananchi wake wote, na pengine utamaduni wa nchi husika.
Ngoja niulize swali, kwa sababu sijui jibu lake: Hivi Saudi Arabia kuna 'homeless'? Hivi Sweden, Austria, Norway kuna 'homeles' na maskini wa kutupwa kama Tanzania?
Nchi zote hizi nilizozitaja hazina utajiri kumzidi Marekani, kwa hiyo, swali langu lina aina ya jibu kuonyesha kwamba maskini wa Tanzania, kamwe huwezi kumlinganisha na maskini wa Marekani.
Kama bado hujanielewa, ningeomba labda umwite pia rafiki yangu ninayemheshimu sana, mkuu 'zitto jr', ambaye naona kakubaliana na hoja yako hapo juu kwa kukupa 'like'.
Tafadhali, mwite zitto jr aje asaidie.