Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Kama kuna wakati najisikia raha kuwa Mtanzania hakika ni sasa
Mzee Mwinyi, Magufuli tutampa mitano tena ya Ahsante
Hadi wanyooke hawa wanaotawaliwa na MABEBERU
 
Inabidi serikali iende mbele zaidi kwa kuharamisha takataka zote zinazoingia kutoka Kenya (bidhaa na raia).

Ukikutwa na chochote "made in Kenya" au kimethibitishwa na KEBS ni uhujumu uchumi.

Na hii sheria isiishie tu kipindi hiki cha mpito,[emoji16] Viongozi waape kuilinda kama ilivyo kwenye kuulinda Muungano.

Newton's 3rd Law of motion on a straight line inahitaji amendment, ACTION AND REACTION hazipaswi kuwa equal.
Huu ndio ugoro mkuu wa uzi huu,hongera mkuu
 
Hata huelewi Kagame ali-solve vipi lile tatizo..

Hujui wala huelewi lolote about it....

Leave that alone,ni topic for another day,leo tuongelee hili ya hawa mavilaza kuja na majawabu ya hovyo kwa issue ya Wakenya..

Hiyo ndio topic ya leo!

Kwahiyo unafiiri Kagame ali3nda kumpigia magoti Mseven?

Kwa taarifa yako mpaka nchi jirani ziliingilia kati na kuna nyuzi zake zimo humu zikiongelea jinsi walivyokuwa wanatunishiana misuli!

Walikuwa wanafanya vile siyo kuineshana nani ni mbabe bali kulinda interest za nchi zao! Na kutokana na hilo saa hii wanaheshimiana.
 
Mbona KQ pekee, si mungefungia hata Jambo Jet ambayo ni mtoto 100% wa KQ, pia precision air ambayo ni 50% mtoto wa KQ? Yaani hapo hakuna kazi imefanyika ni vitisho tu. Hata mufungie KQ na Jambo Jet bado KQ itapata pesa kupitia precision air
Mezeni kwanza iyo Doz nyingine inafuata ukisikia kuwashwa juwa bado kidogo tutawabadilishia Doz!
Angalizo fuata maelekezo ya Dr na si kumshauri Dr
 
Huwezi kuuza utu wako kizembe namna hiyo, yeye aingie kwako afu wewe kuingia kwake mwiko “huwajui wakenya vizuri, chukulia mfano sakata la maroli lililotokea hapa majuzi.
 
Sema kujidanganya! Munapenda kujidanganya watanzania. KQ ilikuwa inakuja Dar mara 14 kwa wiki hiyo ni mara mbili kwa siku kuanzia 2015. Linganisha hiyo na KQ mara 5 kwa siku kuenda Entebbe, Jambo Jet mara 3 kwa siku kuenda Entebbe.

Hata kibiashara, Kenya inafanya biashara mingi na uganda na Rwanda kushinda Tanzania. Biashara kati ya Kenya na Uganda ni karibu mara tatu kati ya Kenya na Tanzania.
Kwasababu Uganda ni Landlocked country.
 
Precision Air imezuiwa kuingia Nairobi.
Apana haijazuiwa, ni abiria tu kutoka Tanzania wote hata watalii wanaotaka kupitia nairobi kutoka Tanzania. Precision air iki beba kutoka kigali kuja nairobi direct ita ingia tu!
 
Pagumu sana hapa! MKAPA ndio alikuwa anaweza kumshauri Magufuli sasa hayupo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yaani diplomasia ya Kenya na Tz ipo pabaya sana.

Ego itaua uhusiano wa hizi nchi mbilii japo wanajidai marafiki kinafiki lakini tushafikaa mbalii aiseee sasa hivi raia wa Tanzania wataanza kutimuliwa Kenya[emoji29][emoji29]

MKAPA majirani wote hawajaja kumzika.
Wakitimua wetu tunatimua wao… give and take..
 
Waswahili waliwahi kusema mwanzo wa ngoma ni lele! Hizi si dalili nzuri kwa mustakabali wa jumuiya yetu. Itabidi kifanyike kitu kuokoa jahazi, huku kutunishiana misuli sidhani kama kutakua na suluhisho la kudumu!

Nani alianza........?......sisi tumeshawahi kumzuia mtu kuja kwetu.....?....walitumia hiyo kujiona wapo sawa wao kuja bwerere......
Saa zingine kuna yule jirani ambae......from nowhere anajisikia tu kukupanda kichwani......sasa huyo inabidi udeal nae perpendicularly ili mwende sawa.......
Tutaelewana tu....Wacha kwanza tuoneshane makali.......
 
Hamna kitu, watapanda Ethiopia airlines, KLM na ndege zingine, watapita Kenya na watakuja bongo.
Narudia tena wewe una akili nyingi sana. Uwezo wako wa kuona mbali ni mkubwa sana. You truly deserve to be in this forum
 
Serikali ya Tanzania yaipiga KQ Airways kutua nchini

"Wakimwaga ugali tunamwaga mboga"
"Magufuli baba lao"View attachment 1523058View attachment 1523059
Huu ni upuuzi mkubwa sana,
Kwanza kabisa tunapaswa kuelewa sababu za wao kukataa ndege zetu kutua kwao-Hatua tunazochukua dhidi ya COVID 19 ambazo binafsi hata mimi naziona zina kasoro nyingi,haziko organised,hatutoi status updates na mbaya zaidi tunataka kila nchi ifanye hivo

Sijaona sababu ya TCAA kufanya hivyo katika msingi wa Reciprocal kwa sababu inaonesha kwamba uwezo wet wa kufikiri ni mdogo sana.

Maoni yangu ni kwamba kama taifa lazima tuweke mipango madhubuti ya kuzuia usambaaji wa COVID na kuweka takwimu sahihi kuhusu hali ya ugonjwa huo.
 
Kwasababu Uganda ni Landlocked country.
Mnapenda kujidanganya! Ni kwa sababu Uganda hawana ujinga ya ujamaa na blind nationalism. Makampuni ya Kenya mengi yanapenda kuwekeza Uganda na Rwanda kwa sababu viongozi wa hizo nchi wana akili ya kujua kutofautisha siasa na biashara.
Kwa sahi viwanda vinavyojengwa uganda mingi ni makampuni za kutoka kenya. BUL(Bidco uganda limited) mtoto wa Bidco Kenya, Hoima cement mtoto wa bamburi cement Kenya,Nile breweries mtoto wa Kenya breweries, Lato milk ni mtoto wa wahindi kutoka Kenya na Brookside Kenya.

Hii ndiyo sababu viwanda vya uganda vinakuwa kwa kasi kushinda Tanzania, na sababu ya biashara kati ya Kenya, Uganda na Rwanda kuwa kubwa kuliko Tanzania
 
... nullification ni KQ originating from Nairobi to Dar/Kilimanjaro/Zanzibar. So, ikianzia Mombasa, Kisumu, Eldoret (all international airports) or elsewhere apart from Nairobi naona itaruhusiwa. Sijui kwani wasomi wetu hawako makini na vitu vidogo lakini vya msingi kama hivi!

Kuna KQ inayotoka Mombasa na viwanja vingine imesajiliwa kutua TZ? Au unafikiri ndege inapaa kutoka popote na kutua kwenye kiwanja chochote bila utaratibu?
 
Wanafikiri wao ni nani kwa mfano? Wakwendee huko, wapambane na stress zao za covid.

Tanzania tupo shwari
Mhandisi hii kitu inabidi tufanye kikao cha dharura nipe coordinate 🥂🍾
 
Yanini kumlaumu mkwezi wakati nazi imeliwa na mwezi?!

Kuna watu walishatabiri Haya yote ya kufungiwa na nchi mbalimbali pale mipaka itakapofunguliwa baada ya kupata ahueni ya ugonjwa wa Corona.

Athari za kutotangaza takwimu juu ya ugonjwa wa Corona ndiyo hizi!

Imeonekana kutotangaza kana kwamba imechukuliwa nchi imekuwa na high risk profile!

Sasa ingekuwa vyema mjadala na hoja ikaanzia hapo badala ya kumhukumu mkwezi.

Nazani kama sijakosea Lema alisema kuhusu athari ya kutotangaza takwimu za ugonjwa wa Corona.

Nabii Lema yametimia kuhusu hili la Corona
 
Back
Top Bottom