Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Kauli ya Jaguar kipindi kile ilikuwa bado haijakomaa (ilikuwa njiti). Sasa imekomaa.
haha natamani nitie neno asee

Ila hili jambo linahitajia zaidi busara kuliko jambo jengine lolote lile

sasa sijui sisi watanzakenya tuegemee upande upi asee

ila mhim zaidi busara kuliko jambo jengine lolote lile aseee.....
 
HAHAHAHA, Kelele za chura hiyo. Uganda ama Rwanda zikifunga Kenya inaweza kuumia lakini si Tanzania. KQ na mtoto wake Jambo Jet zinaenda Entebbe na Kigali kushinda Dar na hizo vitu zingine umetaja
Si uandike kwa utuo ueleweke. Mbona Kama tumbo la kuhara limekushika hivi?
 
Mnapenda kujidanganya! Ni kwa sababu Uganda hawana ujinga ya ujamaa na blind nationalism. Makampuni ya Kenya mengi yanapenda kuwekeza Uganda na Rwanda kwa sababu viongozi wa hizo nchi wana akili ya kujua kutofautisha siasa na biashara.
Kwa sahi viwanda vinavyojengwa uganda mingi ni makampuni za kutoka kenya. BUL(Bidco uganda limited) mtoto wa Bidco Kenya, Hoima cement mtoto wa bamburi cement Kenya,Nile breweries mtoto wa Kenya breweries, Lato milk ni mtoto wa wahindi kutoka Kenya na Brookside Kenya.

Hii ndiyo sababu viwanda vya uganda vinakuwa kwa kasi kushinda Tanzania, na sababu ya biashara kati ya Kenya, Uganda na Rwanda kuwa kubwa kuliko Tanzania
Wewe hamsha akili yako na huo ushabiki wako blind. Ni kweli unaujua uhitaji wa Kenya kwa Tanzania kuanzia watu wao mpaka biashara ya bidhaa zao hapa Tz? Hivi mfano, unajua KQ routes kuja Tanzania ni percent ngapi ya route zao zote Duniani? Hii ya mwisho inatosha kabisa kukuzibua brain 🧠.
 
Hata Tanzania pia ina maamuzi yake, Kama Tanzania imeamua kuzuia ndege za Kenya kwa sababu yoyote ile, hilo pia limefanyika kwa maslahi ya Tanzania, Tafadhali heshimu maamuzi ya kila nchi.


Hili swala siyo la kulichukulia kishabiki kama mtu anayeshabikia mchezo wa simba na yanga!
 
Hapana inamaanisha KLM ikitoka Nairobi ikuje Tanzania, isirudi tena nairobi itoke huko ikienda amsterdam kwa vile abiria kutoka Tanzania hawaruhusiwi katika uwanja zetu za ndege. Hata ATCL haijafungiwa ni abiria wa kutoka Tanzania, yani hata ukuwe mtalii unapitia nairobi amabayo ndiyo hub ya east and central africa kutoka Tanzania hauruhusiwi. Hii ndiyo msimamo ya Kenya.
Tatizo wewe uelewa wako ni mdogo Sana katika dunia ya "Aviation". KLM haiwezi kutoka Kanya kuja Tanzania direct, ni lazima irudi Amsterdam.

Hiyo hatua ya Kenya ni husu ndege zenye kibalia cha kutoka Tanzania na kwenda Kanya moja kwa moja ambazo ni KQ, ATCL, Precision Air na Private planes.

Hiyo inamuhusu raia yeyote anayetokea Tanzania direct to Kenya, sio lazima awe mtanzania.
 
Nimefurahishwa na kimalikia safi kimenyoka hatari, hakijapepesa macho. (...on reciprocal basis= jino kwa jino).
 
Wewe sababu tz haitangazi bhasi unaamini hakuna Corona???? Kenya wenyewe wangekuwa hawatangazi hiyo Corona isingekuwepo tatizo Hela za mabeberu walizokulaaa[emoji23][emoji23][emoji23] Corona imeua watu 200 sijui hukp kenya lakini kuna magonjwa yaneua zaidi ya hio idada lakini hakuna anaejali hiloo sababu ya Misaada lakini Kamwe usifikiria tz hakuna Corona juzi tu kuna shangazi yangu tumemzikaa...

Pamaoja.na kwamba corona bado ipo ila kenya wanaifanyia biashara, pia wana ubaguzi na kujisikia saana.
 
Pagumu sana hapa! MKAPA ndio alikuwa anaweza kumshauri Magufuli sasa hayupo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yaani diplomasia ya Kenya na Tz ipo pabaya sana.

Ego itaua uhusiano wa hizi nchi mbilii japo wanajidai marafiki kinafiki lakini tushafikaa mbalii aiseee sasa hivi raia wa Tanzania wataanza kutimuliwa Kenya[emoji29][emoji29]

MKAPA majirani wote hawajaja kumzika.
Hatujali as long as wao wanatuhitaji zaidi kuliko sisi tunavyowahitaji wao. Uhusiano wa kinafiki hatuutaki...

Wao lazima waone wivu Mambo yao hayaendi watoto hawasomi shule, uchumi umedorora wananchi wamefungiwa ndani Kama kuku huku kwetu sisi tunatwanga na tunapeta, acha tuonyeshane utemi na tuendelee kupunguza Lile gepu la TZS 21 dhidi ya shilingi yao.

Wakitahamaki mwakani imebaki TZS 15 dhidi ya shilingi ndio watajua Watanzania hatutaki masihara.
 
Niko na wakenya kwa hili nasimama na mutu ya Kenya ,sisi wabongo na ma corona yetu tupigwe tu
 
Je unajua, Uganda iko na professionals na wasomi wengi nchini kenya kuliko Tanzania?
Je unajua, Uganda inakuwa kwa kasi kubwa kiuchumi kushinda Tanzania kwa sababu ya biashara na Kenya?
Je unajua, Mganda hahitaji work permit kufanya kazi Kenya?
Lete ushahidi unaoonyesha kwamba uchumi wa Uganda unakua kwa kasi kuliko Tanzania.
Kasi za kukua kwa uchumi ni
1)Tanzania
2)Rwanda
** Hizi nchi mbili hubadilishana "positions"
3)Kenya
4)Uganda
5)South Sudan
6)Burundi
 
Sema wanawekeza sababu bongo competition ni kubwa na sio sababu za kisiasa, ivi mkuu kwa unavyoona kwa mechi ya Mo na bakresa utakuja kizembe ili kuliteka soko. Kuna kampuni ya maziwa ya Kenya inaitwa Kilimanjaro milk si imekufa japo promo ilikuwa kubwa, ku overcome tanga fresh au Azam milk unahis ni easy. Watu wanafuata unafuu mzee
Mnapenda kujidanganya! Ni kwa sababu Uganda hawana ujinga ya ujamaa na blind nationalism. Makampuni ya Kenya mengi yanapenda kuwekeza Uganda na Rwanda kwa sababu viongozi wa hizo nchi wana akili ya kujua kutofautisha siasa na biashara.
Kwa sahi viwanda vinavyojengwa uganda mingi ni makampuni za kutoka kenya. BUL(Bidco uganda limited) mtoto wa Bidco Kenya, Hoima cement mtoto wa bamburi cement Kenya,Nile breweries mtoto wa Kenya breweries, Lato milk ni mtoto wa wahindi kutoka Kenya na Brookside Kenya.

Hii ndiyo sababu viwanda vya uganda vinakuwa kwa kasi kushinda Tanzania, na sababu ya biashara kati ya Kenya, Uganda na Rwanda kuwa kubwa kuliko Tanzania
 
Ndio maana nakwambia,y'all need to go to the drawing board,uamuzi mliochukua ni uamuzi rahisi sana hata kichaa wa mirembe angeuchukua..

Mzee,huwezi nielekeza cha kuongea humu wala mimi siwezi kuelekeza chochote humu!

Kenya imefungia nchi zaidi ya 250,TZ ni one of them..shida mmepaniki na kuchukulia personal,too bad Nairobi ni regional hub EA hapa, mizigo yote itakwamia hapo,na abiria wote hawawezi enda long route ya Cape Town eti ndio waje TZ.

Jawabu sio rahisi kiivyo kama mlivyotoa, is that economically at your best interest au mmeenda kula pilipili kichaa za Chattle huko?

This is chess and not checkers.
Wacha wakwamie huko mkatalii nao mjini!
Dont start a fire you can't finish...
 
... nullification ni KQ originating from Nairobi to Dar/Kilimanjaro/Zanzibar. So, ikianzia Mombasa, Kisumu, Eldoret (all international airports) or elsewhere apart from Nairobi naona itaruhusiwa. Sijui kwani wasomi wetu hawako makini na vitu vidogo lakini vya msingi kama hivi!
.....mmmmmh mkuu nawe mpana hatari.
 
Halafu hawa jirani zetu wana matatizo kweli wanaanzisha mambo kisha kuanza kulia.

US kafunga ubalozi mdogo wa China in Houston
China kajibu na kufunga ubalozi mdogo wa US in Chengdu.

Life goes on, wao wanafanya mambo wakipewa retaliation wanaanza ohoo sijui mbona nani anafanya hivi sisi na Uganda tupo vizuri, sijui KLM, EU etc with nonsense; unajiuliza what is Kenya relation with Uganda got to do with Tanzania.

Hapa hakuna third party; ukifanya ‘A’ when the gesture is reciprocated live with it sio kuanza lia lia; that’s how diplomacy works.

Tanzania will never be a pushover
 
Wewe ni jirani, ndugu gan ambae unamfahamu amefariki kwa Corona, njia mathubuti kwa kitu ambacho ni invisible au naweza kusema weak
Mkuu,so wewe unasubiri mpaka afe ndugu yako?Kwamba wakifa wengine haikuhusu?Wakiugua wengine hata wasipokufa haikuhusu?Wakiugua wengine ilia wasipimwa haikuhusu?Kwamba tukae na wagonjwa kimya kimya bila kupima,kufuatilia na kujua hali halisi?Watakao kufa wafe na watakaopona wapone?je hio ndo imani yako?

Kwa mtazamo huo nafikiri ni sawa kabisa wakatuzuia,Tulivowakatalia tumewasaidia sana maana......That is too selfish.
 
Acha upumbavu
Na wewe acha umatakor!

Hupendi hoja yangu ruka nenda kwa unazopenda,otherwise comfortable with my own post..

Ushauri tu,post ya mtu ni upumbavu basi weka yako wewe yenye akili,yanini kupoteza your time na watu wapumbavu wenye post za upumbavu?

What a whimp!
 
Hakuna shirika la ndege la nchi nyingine inayoweza kuruka toka nchi nyingine ambayo sio nchi yake na kutua nchi ambayo sio nchi yake.

Kwa mfano, KLM haiwezi kutoka Nairobi kuja Dar, lazima iende Amsterdam ndio ije Dar. Labda useme raia wa Kanya wasiruhusiwe kuingia Tanzania
Hapana! KWa masoko madogo ya Afrika wanatua tu! Ndo maana KQ inakwenda Zambia kupitia Harare na Maputo. Kuna KLM inayopitia Nairobi kuja Dar.

Tatizo la Wakenya hawataki kukubali kwamba wana tatizo ambalo kiasi fulani TZ halijatupiga sana, COVID-19. KIla wakati hawaoni sababu ya TZ kuwa na hali nzuri. Wanaelewa tuko 60 mil. na hawataki kuiona size ya nchi kwamba ktk EAC TZ ni Anchor ya kuwafanya wasiyumbe, hata kiuchumi. Kila wakati wanasababu za kitoto badala ya diplomasia. Lakini ni wanyonge sana kwa nchi za ulaya au wazungu. Yoote waliyoyafanya na lockdown yao ni kama kuigiza ulaya wanavyofanya. Tutaelewana tu!
 
MIMI NINA OBSERVATION TOFAUTI;

1. Huu mgogoro wa Kenya na Tanzania ni ishara ya ku fail kwa diplomasia ya kimataifa chini ya utawala wa Magufuli....

2. Mgogoro huu ni ishara (signal) tu kuwa lipo tatizo kubwa zaidi ambalo halisemwi wazi na viongozi wa nchi hizi mbili na ambalo kwa kweli ndilo chanzo cha mgogoro huu....

Haiwezekani ishu iwe ni korona wakati vikao na vikao kati ya viongozi wa nchi hizi mbili vimekaa kutafuta ufumbuzi, lakini bado hawakubaliani tu ili kumaliza mgogoro na badala yake unazidi kukua tu....!

3. Mgogoro huu hauwaumizi watawala wa serikali ya CCM bali wananchi wa kawaida kabisa wa itikadi za kisiasa zote ambao maisha yao yanategemea mahusiano mema kati ya nchi hizi mbili. Wananchi tukatae uhuni huu na interests za watu binafsi (watawala) kutuumiza sisi....

2. Aidha, mimi nilidhani pia wangepiga marufuku kila ndege inayopitia Kenya kuja Tanzania ya shirika la ndege lolote like. Lakini kuilenga KQ tu inadhihirisha kabisa liko jambo jingine lililo chanzo cha mgogoro huu na siyo virusi vya Corona kamwe...
 
Hivi unajua kwamba Wakenya wengi wapo Tz
Huyo jamaa anaamini Rwanda ambayo ni landlocked country size ya mkoa wa Tz ina-influence kubwa kiuchumi kwa Kenya kuliko Tanzania. Sasa akili au mbolea hiyo?!?
 
Back
Top Bottom