Serikali ya Ujerumani kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 56 za Kitanzania zitakazotumika kwa ajili ya miradi ya mikubwa ya shughuli za Uhifadhi nchi

Serikali ya Ujerumani kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 56 za Kitanzania zitakazotumika kwa ajili ya miradi ya mikubwa ya shughuli za Uhifadhi nchi

Je, huu ni msaada au mkopo? Tungekuwa tunapata ufafanuzi kidogo ili sisi walipa kodi tujue, endapo tumeongezewa deni jingine la kulipa au tumepewa bureee
 
This is good news ila hizo pesa ni peanut compared to what German looted Tanzania, hivyo ni sehemu tuu ya CSR. Sasa its high time Tanzania sio tupewe viji misaada mbuzi as favours, bali tupewe haki yetu na mapato stahili ya mali kale zetu zilizoko Ujerumani. Sio vibaya tukiwakumbusha Ujerumani kurudisha fuvu la Mkwawa shujaa, na wale mashujaa wote waliowanyonga, kisha kuwachinja na kuchukua vichwa vyao na kuvipeleka Ujerumani. 2. Warudishe malikale zote walizo loot from German East Africa. 3. Wagharimie kutujengea uwezo wa uhifadhi, ili waturudishie ile skeleton ya dinasauria wetu wa Tendaguru ambeye ndie anayevunja gueness book of records ya dinasauria mkubwa duniani, ambaye anawaingizia Ujerumani bilions of money kupitia utalii. Watujengee uwezo, waturudishie dinasauria wetu, watu waje Tanzania na sio Ujerumani.
P
Mzee Pascal je unaweza kuamua unapenda kudai nini? Unaanza warudishe walichopora, ila baada hutaji walichopora unjadili mifupa isiyo na thamani yoyote ya kifedha;
(mafuvu hukaa kwenye ghala za makumbusho yao, hakuna anayetaka kuziona; mifupa ya dinosauri inapendeza lakini jinsi ilivyo haileti faida, makumbusho yao yanahitaji pesa kutoka serikali kwa sababu kiingilio hakitoshi kulipa gharama; juzi tu walifanya ukarabati wa kiunzi kwa milioni nyingi...)
 
Cha msingi hizo ela zisije zikaingia kwenye mikono ya wajanja wachache.
 
Mkipewa hizo pesa zote msinyanyue tena mdomo kudai mabaki ya limjusi lenu
 
Enzi za Kayafa fedha kama hizi zingetengwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ili kulazimisha CCM ishinde.
 
Back
Top Bottom