Serikali ya Zimbabwe inazidi kugonga vichwa vya Habari kufuatia ukiukaji wa haki za binadamu

Serikali ya Zimbabwe inazidi kugonga vichwa vya Habari kufuatia ukiukaji wa haki za binadamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Zimbabwe inazidi kugonga vichwa vya Habari kufuatia ukiukaji wa haki za binadamu. Ni kulingana na ripoti ya HRW

Wanaharakati Zimbabwe wanaishutumu serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa kwa kutumia suala la janga la corona kuwakandamiza wapinzani.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch jana Alhamisi, Zimbabwe ni kati ya nchi 23 za Afrika ambazo zinatumia janga la corona kuminya haki za raia.

Mwandishi wa habari Frank Chikowore, ni miongoni mwawaandishi wa habari waliokamatwa mwaka jana kwa kumhoji mwanasiasa wa upinzani na pia mwanaharakati ambaye alidaiwa kuteswa na maafisa wa usalama wakati wa vikwazo vya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.
 
Back
Top Bottom