Serikali yaagiza wanaotoza fedha za nguzo za umeme kwa wananchi wakamatwe

Serikali yaagiza wanaotoza fedha za nguzo za umeme kwa wananchi wakamatwe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Medard Kalemani ameagiza makandarasi au mameneja wanaolazimisha wananchi kulipia nguzo za umeme ili kuunganishiwa nishati hiyo kukamatwa.

Amesema watu hao wanapuuza agizo la Serikali inayotaka nguzo hizo kutolewa bure.

Ametoa ufafanuzi huo Februari 15, 2020 baada ya kupokea malalamiko ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo katika hafla ya ufunguzi wa ofisi ya CCM Mkoa wa Geita.

Yakobo amesema licha ya Serikali kutangaza mara kwa mara kuwa nguzo za umeme ni bure wapo makandarasi wanaoendelea kukaidi agizo hilo na kuwatoza wananchi fedha.

Kalemani amewataka wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia agizo hilo na kuwakamata watakaotoza fedha.

Amebainisha kuwa Serikali inatoa nguzo za umeme bure na wananchi wanapaswa kuchangia Sh27,000 pekee kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.
 
Hiyo ni kwa ajili ya ule umeme unaosambazwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) au ule wa kawaida unaoshughulikiwa na TANESCO moja kwa moja? Na pia kwa nini waziri katumia neno "wanaolazimisha" ina maana kuna nafasi ya "kuwaomba" wananchi kulipia hizo nguzo na wakilipia kwa hiari inakuwa siyo tatizo? Kama hilo la kuwaomba lipo na linaruhusiwa basi kuna uwezekano wa mameneja kulazimisha kwa kutumia lugha ya kuwaomba kulipia kama njia ya kujenga mazingira ya rushwa.
 
tunachangamoto kwenye kila nyanja kiuhalusia. haijulikani kipi ni kipi.

anyway nshanunua nguzo hpo mwaka jana, wakifikia kauli ya ku refund ntarud tena.
 
Ukienda Tanesco wanakwambia hakuna nguzo, Serikali haijaleta nguzo kwaiyo subiri hadi zitakapo kuja. Toeni utaratibu mzuri wengine hela tunazo za kulipia tunahitaji utaratibu tu, hao wa bure waendelee kusubir

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua siasa kwenye utendaji ni ngumu. Mimi nimelipia nguzo kwa sharti la kuandika na kupitisha kwa mtendaji wa mtaa. TANESCO wanasema hawajapewa mwongozo wa utekelezaji wa agizo la Waziri tangu alipolitoa wanakwambia kama unataka subili hadi mwongozo ufike au andika barua wakuunganishe kwa gharama za awali.
 
Hiyo ni kwa ajili ya ule umeme unaosambazwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) au ule wa kawaida unaoshughulikiwa na TANESCO moja kwa moja? Na pia kwa nini waziri katumia neno "wanaolazimisha" ina maana kuna nafasi ya "kuwaomba" wananchi kulipia hizo nguzo na wakilipia kwa hiari inakuwa siyo tatizo? Kama hilo la kuwaomba lipo na linaruhusiwa basi kuna uwezekano wa mameneja kulazimisha kwa kutumia lugha ya kuwaomba kulipia kama njia ya kujenga mazingira ya rushwa.
Mkuu unachoongea ni sahihi wanachokwambia andika barua ili wakuunganishe au subili nguzo/ mwongozo wa namna ya utekelezaji wa agizo.
 
Ukienda Tanesco wanakwambia hakuna nguzo, Serikali haijaleta nguzo kwaiyo subiri hadi zitakapo kuja. Toeni utaratibu mzuri wengine hela tunazo za kulipia tunahitaji utaratibu tu, hao wa bure waendelee kusubir

Sent using Jamii Forums mobile app
afadhali yahioooo mbayaa Nyumba ya NNE anajenga anakukuta akamaliza aNAPATA UMEME WEWE UNASUBIRIA NGUZO YEYE SIJUI NGUZO KAINUNUA MBEYA AMA WAPI HILI SHIRIKAA LINANUKA KABISA RUSHWA NENDEN KMR M WISHOO
 
Back
Top Bottom