Serikali yaagiza wanaotoza fedha za nguzo za umeme kwa wananchi wakamatwe

Serikali yaagiza wanaotoza fedha za nguzo za umeme kwa wananchi wakamatwe

Hiyo ni kwa ajili ya ule umeme unaosambazwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) au ule wa kawaida unaoshughulikiwa na TANESCO moja kwa moja? Na pia kwa nini waziri katumia neno "wanaolazimisha" ina maana kuna nafasi ya "kuwaomba" wananchi kulipia hizo nguzo na wakilipia kwa hiari inakuwa siyo tatizo? Kama hilo la kuwaomba lipo na linaruhusiwa basi kuna uwezekano wa mameneja kulazimisha kwa kutumia lugha ya kuwaomba kulipia kama njia ya kujenga mazingira ya rushwa.

REA

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nipo umbali wa kilomita 4 kutoka kwenye centre yenye umeme ninahitaji kuunganishiwa umeme na mimi napaswa kupatiwa nguzo bure mpaka sehemu ya makazi yangu ??
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Medard Kalemani ameagiza makandarasi au mameneja wanaolazimisha wananchi kulipia nguzo za umeme ili kuunganishiwa nishati hiyo kukamatwa.

Amesema watu hao wanapuuza agizo la Serikali inayotaka nguzo hizo kutolewa bure.

Ametoa ufafanuzi huo Februari 15, 2020 baada ya kupokea malalamiko ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo katika hafla ya ufunguzi wa ofisi ya CCM Mkoa wa Geita.

Yakobo amesema licha ya Serikali kutangaza mara kwa mara kuwa nguzo za umeme ni bure wapo makandarasi wanaoendelea kukaidi agizo hilo na kuwatoza wananchi fedha.

Kalemani amewataka wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia agizo hilo na kuwakamata watakaotoza fedha.

Amebainisha kuwa Serikali inatoa nguzo za umeme bure na wananchi wanapaswa kuchangia Sh27,000 pekee kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana nyakati zingine wasomi hawataki kabisa kufanya kazi serikalini. Kazi na wanasiasa ni jukumu gumu na la kipuuzi mno wakati mwingine. Anakukabidhi jukumu la kugawa mkate kwa watu wake halafu hakupi mikata ya kuwagawia. Usipowagawia anakuwajibisha kwa kosa lake la kutoleta mikate.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo umbali wa kilomita 4 kutoka kwenye centre yenye umeme ninahitaji kuunganishiwa umeme na mimi napaswa kupatiwa nguzo bure mpaka sehemu ya makazi yangu ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawawezi kukujibu ndugu yangu hili suala nimewauliza sana hawatoa majibu maana mimi kutoka kwenye source ya umeme niko umbali wa Km 1.5 hivi but wako kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nimeomba umeme wa njia 3 katika kuunga juhudi za muheshimiwa raisi Tanzania ya viwanda tanesco wameniandikie bili ya 92100au nitoe 300000 nipewe ya ml 1.6

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwinge savei anatengeneza mazingira ya pesa ananambia tuinane nduo anuandikie bili kwahiyo anakaribisha maUngumzoo mie ndio wamenichoshaa kweli tanesco na njaa zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukienda tanesco kuwaeleza hili jambo watakujibu halijapitishwa bungeni 😁😁

Kuvutiwa umeme single phase 321,000/= 3phase 912.000 😁😁 wangepatikana wapinzani kama makampuni ya simu wasingethubutu kutupandilia vichwani
 
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Medard Kalemani ameagiza makandarasi au mameneja wanaolazimisha wananchi kulipia nguzo za umeme ili kuunganishiwa nishati hiyo kukamatwa.

Amesema watu hao wanapuuza agizo la Serikali inayotaka nguzo hizo kutolewa bure.

Ametoa ufafanuzi huo Februari 15, 2020 baada ya kupokea malalamiko ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo katika hafla ya ufunguzi wa ofisi ya CCM Mkoa wa Geita.

Yakobo amesema licha ya Serikali kutangaza mara kwa mara kuwa nguzo za umeme ni bure wapo makandarasi wanaoendelea kukaidi agizo hilo na kuwatoza wananchi fedha.

Kalemani amewataka wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia agizo hilo na kuwakamata watakaotoza fedha.

Amebainisha kuwa Serikali inatoa nguzo za umeme bure na wananchi wanapaswa kuchangia Sh27,000 pekee kwa ajili ya kuunganishiwa umeme.
Kasi ya rais Magufuli ni kubwa kuliko watukanaji wake.
IMG-20200215-WA0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukienda tanesco kuwaeleza hili jambo watakujibu halijapitishwa bungeni [emoji16][emoji16]

Kuvutiwa umeme single phase 321,000/= 3phase 1,912.000 [emoji16][emoji16] wangepatikana wapinzani kama makampuni ya simu wasingethubutu kutupandilia vichwani
Naomba ufafanuzi tofauti ya single phase na 3phase.na namna ya kuzitumia.nipo gizani kidogo hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ufafanuzi tofauti ya single phase na 3phase.na namna ya kuzitumia.nipo gizani kidogo hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kifaa kinachotumia umeme wa kawaida mfano majumbani kuna taa, friza, fridge, pasi n.k, hapo sio lazima utumie 3phase. Only single phase.

Kifaa kinachotumia umeme mkubwa mathalan kiwanda cha tofali, ginnery, plant za dhahabu, almasi n.k, hapo yakupasa uwekewe 3phase, umeme wenye uwezo wa kuendesha kiwanda chako.
 
Back
Top Bottom