Ni kweli tuna deni lakini siyo kweli kwamba hatukopesheki kwa sababu ya deni kubwa. Tanzania ina kiwango kidogo sana cha Debt to GDP katika EAC ukilinganisha na nchi zingine.
Kenya 59%
Rwanda 42%
Uganda 40%
Tanzania ni 37%
Kiwango ambacho watoa mkopo kama huanza kuogopa kutoa mikopo ni pale kinapofikia 50% debt to GDP ratio.
Kenya juzi wamepata mkopo pamoja na kwamba wana 59 Debt to GDP. Hata Ethiopia ambao wako kwenye 61% debt to DGP ratio wanaendelea kupata mikopo.
Tanzania hatupati mikopo kwa sababu ya masharti ambayo yanakuja na string attached ambazo either hatuzikubali au hatuzitimizi lakini sio kwamba eti tuna deni kubwa.
Hata hizo takwimu za GDP ya Tanzania usiziamini. Katika awamu hii, takwimu nyingi ni za uwongo, ni za kupikwa.
Hiyo GDP ndiyo utajiri wenyewe. Kama tunawadanganya watu kuwa sisi ni matajiri, tunawadanganya kuwa uchumi unakua kwa 7.1% wakati ni 5% or less, ina maana hata GDP yetu inakuwa ni ya uwongo.
Kama GDP yetu ni ya uwongo, ina maana hata hiyo asilimia ya deni letu ni ya uwongo pia.
Usiulinganishe uchumi wa Kenya na Tanzania. Uchumi wa Kenya una predictability, wakati uchumi wa Tanzania hauna predictability. Haieleweki kwa namna tunavyoenda, tutaishia wapi. Unaweza kumkopesha mwenye deni ambaye unaelewa ana uhakika na anachofanya, kuliko asiye na deni ambaye haijulikani anafanya nini kwaajili ya kufika wapi.
Utawala huu umekosa maono. Wanadhani wakiwanyima watu uhuru wa kujua, watafanikiwa kwa kila jambo wanalolipanga. Ukweli ni kinyume. Anayekukopesha ili awe na uhakika, kuna wakati anahitaji taarifa toka kwa watu na taasisi huru. Kama wewe hutaki taasisi huru ziwe huru kufanya kazi, hata kama taarifa zako zitakuwa za kweli, wakati wote zitatiliwa mashaka.
Nilishangaa nilipokuwa ASEX (Australian Stock Exchange), Sydney; kuona Tanzania imekuwa listed kwenye nchi hatari kwa mitaji ya nje. Leo huwezi kupata fedha kwaajili ya kuja kuwekeza Tanzania.
Ni uwongo mkubwa kueleza kuwa tunashindwa kupata mikopo kwa sababu inakuwa na masharti tunayoyakataa. Ukiacha pesa MCC, ambaye ilihitaji kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na uhuru wa watu, hakuna msaada tuliowahi kuukataa kwa sababu ya masharti. Hata pesa ya MCC, hatukuikataa bali walitukatia watoaji baada kumnyang'anya ushindi wa wazi Maalim Seif kule Zanzibar.