Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora"
Pia alisema " Pesa si msingi wa maendeleo bali ni matokeo yake"
Hawa wachumi wanaposema tukusanye pesa zaidi je wanaijua falsafa ya Mwalimu.
Ardhi tuliyonayo ni kwa ajili ya kulima na viwanda ni matokeo ya kufanikiwa kwa kilimo.
Kilimo kitaleta fedha za kigeni lakini ukusanyaji wa kodi za ndani hauongezi fedha za kigeni moja kwa moja.
Ili tufanikiwe tuitumie ardhi yetu kikamilifu kwa kuwekeza zaidi kwenye Kilimo kuliko kitu chochote kile.
Uwekezaji tunaoufanya sasa ni mzuri sana lakini unatakiwa ufanywe baada ya kilimo kufanikiwa na kuwa kilimo cha kimataifa na si cha jembe la mkono.
Tukiendelea kutoimarisha kilimo chetu, ukuaji wa uchumi wetu utakuwa si endelevu na tutaendelea kuwa na vijana wengi mitaani walio na elimu ya juu na wasio na elimu kabisa wakizurura mitaani.
Sasa hivi mazao ya wakulima pamoja na kuwa ni machache lakini yanakosa soko na pengine kwa sababu hayako kwenye ubora unaotakiwa kimatifa au Serikali imeweka urasimi katika watu kujitafutia masoko wenyewe.
Bado kilimo ni uti wa mgongo wa Uchumi wetu lakini hatuutendei haki kwa kuutangaza kama tunavyofanya katika kutangaza ukusanyaji wa kodi, viwanda, elimu, afya, ndege, barabara, madaraja nk.