Kwa kweli nimeshutuka sana baada ya kumsikiliza Waziri wa kilimo ndugu Asunga kuwa malipo ya Korosho yalitofanywa na serikali pesa nyingi zimeibiwa.
Yaani pamoja na kufukuzwa kwa yule aliyekuwa mkurugenzi wa bodi ya korosho proffesa, pamoja na kuundwa kwa Kamati ya uhakiki wa malipo bado watu wamepigwa mabilioni ya pesa?
Nina imani kamati za kuhakiki walipwaji ziliundwa kwa kuingiza baadhi ya watumishi wa vitengo vyetu nyeti hivi imekuaje hayo mabilioni tena kuibiwa?
Nimejiuliza sana dhidi ya uhadilifu wa watumishinwa Bodi ya korosho, watumishi wa wizara ya kilimo idara za ushirika na wengine.
Mimi niliwahi kusema kuwa hizi idara zinastaili kufumuliwa ila kwa sbabu tunasemeaga kupitia jf mpka huwe pascally ndio utaheshimika.
Katika hili ningeomba kuwashirikisha jambo ndugu zangu kuwa kuna uwezekano mkubwa kauli nyingi za Mh Rais ambazo huwa zinaruhusu matumizi fulani ya pesa watu wanazitumia sana kupiga pesa.
Kama maamuzi magumu kama yale watu watu wameiba pesa hatua kali zichukuliwe dhidi ya walio hakiki, Kaimu warajisi wa mikoa, na maafisa ushirika wa eneo uska pasipo kusahau watumishi wa bodi ya korosho.