Serikali yabaini ubadhirifu mabilioni ya fedha za malipo ya korosho. Wakulima wasiolipwa watakiwa kujitokeza na CAG kuikagua bodi ya Korosho

Serikali yabaini ubadhirifu mabilioni ya fedha za malipo ya korosho. Wakulima wasiolipwa watakiwa kujitokeza na CAG kuikagua bodi ya Korosho

Nani alikuambia? Wizi na ufisadi hauwezi kuisha. Upo hata zile nchi ambazo zina kiwango kidogo cha ufisadi. Kinachotakiwa ni viongozi wenye nia na kiu ya kuuchukulia hatua kama ilivyoibuliwa hapa.

Haaaa haaaa acha nicheke tu, viongozi wenye nia ndio hao wanaingia madarakani kwa kubaka box la kura! Pale muhalifu anapoenda kupambana ili kumaliza uhalifu!
 
Huyu CAG anaitendea haki nafasi yake
Tunakuona mwishimiwa juhudi zako. Unadandia kila kitu, usije dandia rungu uta .....
IMG-20191117-WA0001.jpeg
 
Waziri wa kilimo mh Hasunga amesema mabilioni ya fedha za korosho yameliwa na wajanja hivyo ameunda tume ya uchunguzi kufuatilia ubadhirifu huo.

Pia mh Hasunga amemtaka CAG kuikagua bodi ya korosho kwani kuna kiasi cha zaidi ya sh bilioni 55 hazijulikani ziliko.

Kadhalika Waziri amewataka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wajitokeze wakiwa na vielelezo vyao.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Yuko wapi CAG wa kukagua wizi wa Korosho? CAG wa kiukweli Prof Mussa Assad ameondoka, huyu Kicheere atakuja kufanya maigizo kwa kuchukua maelekezo toka kwa Jiwe. Usanii mtupu!!
 
Yuko wapi CAG wa kukagua wizi wa Korosho? CAG wa kiukweli Prof Mussa Assad ameondoka, huyu Kicheere atakuja kufanya maigizo kwa kuchukua maelekezo toka kwa Jiwe. Usanii mtupu!!
CAG ni taasisi!
 
JAMAA hawa ni waongo Duh

Unaunda tume afu unamtaka CAG akague ni upotevu wa pesa kwanini Tume na wakati huohuo CAG KATUMWA NIMATUMIZI MABAYA YA FEDHA ni shida SANA
Waziri wa kilimo mh Hasunga amesema mabilioni ya fedha za korosho yameliwa na wajanja hivyo ameunda tume ya uchunguzi kufuatilia ubadhirifu huo.

Pia mh Hasunga amemtaka CAG kuikagua bodi ya korosho kwani kuna kiasi cha zaidi ya sh bilioni 55 hazijulikani ziliko.

Kadhalika Waziri amewataka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wajitokeze wakiwa na vielelezo vyao.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Mtabakia kulilialia tu
Zao la korosho mshaliuaaaaa

Ova
 
Hizi ni siasa tena siasa uchwara, malipo yanalipwa kwa njia ya benki. Na utaratibu uulikua kila mkulima analipwa kupitia akaunti yake na serikali ilikua inamuingizia mkulima moja kwa moja bila kupitia chama kikuu au chama cha msingi (Amcos). Sasa hizo fedha zipotee zinapotea kwa njia ipi.

Serikali ilkili adharani tu kwamba haitoweza kumalizia madeni sababu ilipata hasara!.
Korosho ilizoutangazia umma kwamba imenunua kwa tsh 3,300/-wamekuja kuuza 2700 hadi tsh 2000/-. na hadi sasa bado hazijaisha!.

Lakini hizi siasa za kuamisha goli ili kutafuta huruma ya wananchi ni kutuona wakulima wa korosho ni mazumbukuku.
Akili yako ya ajabu sana yaani kama wamelipwa kupitia BANK hakuwezi kuwa na ubadhirifu wowote?
 
Hii nchi inaendeshwa kigangster ni kukurupuka full. Watu wanapenda sana sifa na wamezidi ushamba
 
Waziri wa kilimo mh Hasunga amesema mabilioni ya fedha za korosho yameliwa na wajanja hivyo ameunda tume ya uchunguzi kufuatilia ubadhirifu huo.

Pia mh Hasunga amemtaka CAG kuikagua bodi ya korosho kwani kuna kiasi cha zaidi ya sh bilioni 55 hazijulikani ziliko.

Kadhalika Waziri amewataka wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa wajitokeze wakiwa na vielelezo vyao.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Hawana hela za kuwalipa wakulima waache ubabaishaji, Jiwe si alikuwepo huko Mtwara alijidai hela zipo?
 
Back
Top Bottom