Serikali yabainisha walimu 58 wenye PhD shule za msingi!

Unadhani kwenye Movie ndio hakuna uchakachuaji?
Jaribu utajionea mwenyewe....

Well said, maana hata Phd ya kikwete ni mpango ulioratibiwa na Steven Seagal na wenzake, wakati wao hawana hizo Phd.
5.JPG
 
Mama Mdogo,

Hivi mmiliki wa Shule anaweza kuwa kwenye list ya waajiriwa wa shule "as a member of staff"?

Kwahiyo wakija wakaguzi naye anakaguliwa "Kitabu cha Maadalizi ya somo e.t.c"!

Kweli Tanzania hakuna lisilowezekana!

kwa nini isiwezekane, kamwulize Dr Didas kule Chanika japo yeye yuko secondary school
 
Am i in right forum??
Mtoa hoja upo sahihi au nitafute miwani nisome upya hii kitu??
 
USTAADH hebu tufafanulie hizo PhD zinazofundisha Shule za msingi wakati baadhi ya Universities wanatafuta

Mkuu, tatizo ninaloliona hapo ni kwamba, Wizara ya elimu hawa-update (samahani kwa kiswanglishi) rekodi zao mara kwa mara. Ninachofahamu ni kuwa kuna walimu wa shule za msingi ambao wamejiendeleza mpaka kufikia level ya PhD. Namfahamu mtu mmoja ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na hivi sasa ni anamalizia PhD yake na tayari alishaajiriwa na UDSM na huyu huenda akawa mojawapo wa hao wanaotajwa na wizara ya elimu.
 
Hiyo ndio shida ya kukaa bongo bila kutembea na kufunguka macho. Huku US mbona watu wana PhD na Masters na wanafundisha middle schools na high schools.
Cha ajabu ni kipi?
Kama Obama alimaliza Masters (LLM) tena pale Harvard Law na akaenda kuwa Community Organizer sasa ajabu iko wapi?
Tembeeni mjionee
 
Bongo zipo hizi jamani, mnasahau Open university wanatoa PhD! Hizi ndo PhD za hawa walimu wa primary. I am sure if they are confident enough that they hold PhD, they would not continue to be where they are.

Tufafanunulie mashaka yako dhidi open university,manake hueleweki.
 
PhD..............!!!!!!!!!!! .............Primary................!!!!!!!!!!!!!! there must be a typing error somewhere............

inawezekana tena sana 2 kwakuwa mtu kujiendeleza kimasomo ni moja ya maendeleo na inaruhusiwa tatizo ni kwamba serikari yetu haina takwimu zakuwatumia hawa watu so hawana idadi ya watu wanaojiendeleza mili wakimaliza wawahamishe level za juu.
 
PhD..............!!!!!!!!!!! .............Primary................!!!!!!!!!!!!!! there must be a typing error somewhere............

Not a typing error, I know someone for sure, to be exact, my Aunt. She holds a PhD from Missouri University. Her last five years before here retirement she took a job and worked as a primary school teacher (Bukoba Vijijini). Her case could be different though because it was more circumstantially driven. She had to move to the country (Kijijini) to join her husband who had retired.
 
Hiyo ndio shida ya kukaa bongo bila kutembea na kufunguka macho. Huku US mbona watu wana PhD na Masters na wanafundisha middle schools na high schools.
Cha ajabu ni kipi?
Kama Obama alimaliza Masters (LLM) tena pale Harvard Law na akaenda kuwa Community Organizer sasa ajabu iko wapi?
Tembeeni mjionee

Marekani usiilinganishe na Tanzania. Katika hali ambayo shule za kata zinafundishwa na form six wa kujitolea, itakuwa ni ajabu kusikia kuwa kuna mwalimu wa shule ya msingi mwenye PhD. Linganisha vinavyokaribiana. Uganda na Tanzania, Tanzania na Rwanda, n.k

Hata hivyo, tunakupongeza kaka yetu kwa kutembea; wewe sio mbumbumbu kama sisi.
 
N-handsome;1245411]What is the difference between Harvard PhD and Open University PhD? especially when the OUT PhD is not honorary one like Boyz II Men ones :lalala::lalala:

Wala usiulize kabisa tofauti ya PhD ya mtu aliyemaliza Harvard na hizo za Open University, tusingekuwa tuna fanya ranking za vyuo kama vyuo vyote vinatowa elimu sawa mkuu. Labda hapa kwetu bongo lakini kwa wenzetu walioendelea chuo ulichosoma kina matter zaidi, huwezi toka na PhD yako ya UDSM Ukafundishe Harvard, siyo kuwa hujui mambo wanakuchukulia kuwa quality ya elimu/PhD yako haikidhi mahitaji ya Chuo.

What is the difference between Harvard PhD and Open University PhD? especially when the OUT PhD is not honorary one like Boyz II Men ones :lalala::lalala:

nadhani jamaa hajui maana ya Phd. Ndo maana analeta dharau kwa OUT. Amelogwa na UDSM
 
Bongo zipo hizi jamani, mnasahau Open university wanatoa PhD! Hizi ndo PhD za hawa walimu wa primary. I am sure if they are confident enough that they hold PhD, they would not continue to be where they are.

Kwani PhD za Open University ni tofauti na zingine?[/QUOTE]

KAMA NIMEKUELEWA VIZURI UNA MAANA KUWA PhD ZA OPEN UNIVERSITY ZINA UTATA
 
Kwani PhD za Open University ni tofauti na zingine?

KAMA NIMEKUELEWA VIZURI UNA MAANA KUWA PhD ZA OPEN UNIVERSITY ZINA UTATA[/QUOTE]

... labda nifafanue, PhD meaning Doctor of Philosophy na SIO Pull him/her Down....kwi kwi kwi!!!
 
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imebainisha kuwa hadi kufikia Juni mwaka huu, shule za msingi zilikuwa na walimu wapatao 58 wenye Shahada ya Udakatari wa Falsafa (PhD) wakati walio na Shahada ya Uzamili ni 75, Shahada ya Kwanza 1,099 na Stashahada ya Ualimu ni walimu 6,512.

Hata hivyo, pamoja na makundi hayo matatu, pia imeonesha kuwa idadi ya walimu wa Daraja la Tatu A ni 148,986 na wa Daraja B na C idadi yao ni 9, 123 sawa na asilimia 5.8 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Taasisi ya BEST 2006-2010.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ualimu katika Wizara hiyo, Rose Massenga, alibainisha hayo Novemba 8 wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Jumanne Sagini, kufungua mkutano wa wakuu wa vyuo vya ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali mjini hapa.

Kwa mujibu wa Masenga, upande wa walimu wa shule za sekondari wanaofundisha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, wenye Shahada ni 9,910, Stashahada 22,171, wenye leseni ni 3,997 sawa na asilimia 12.46 na wengine 4, 439 sawa na asilimia 13.84.

Hata hivyo, alisema mahitaji ya walimu wa elimu ya awali na msingi kwa mujibu wa PEDP katika mwaka 2010 hadi 2011, wanahitajika walimu 18, 783 kati ya hao 15, 783 ni wa msingi na 3,000 wa elimu ya awali, ambapo elimu ya sekondari kwa kipindi hicho wanahitajika walimu 30,075.

Alisema mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya msingi na ule wa elimu ya sekondari, imesababisha ujenzi wa shule nyingi za msingi na sekondari uliambatana na uandikishaji wa wanafunzi wengi kwenye ngazi hizo na matokeo yake kusababisha mahitaji makubwa ya walimu.

Hivyo alisema ni vyema ieleweka kuwa msimamizi wa utoaji wa mafunzo ya ualimu unazingatia mambo mengi vikiwemo sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayoelezeka katika viwango vya kitaifa na kimataifa.

Naye mgeni rasmi, Sagini alisema shule za msingi zina uhaba wa walimu wasiopungua 45,000, wakati upungufu ni mkubwa zaidi kwa sekondari katika masomo ya sayansi.

Hata hivyo, alisema ngazi ya elimu ya msingi idadi ya wanafunzi imeongezeka maradufu kutoka milioni nne mwaka 2001 hadi milioni 8.4 mwaka 2010, ambapo shule za sekondari idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka chini ya 300,000 mwaka 2001 hadi milioni 1.6 mwaka 2010.

Sagini alisema wakati idadi ya wanafunzi ikiongezeka kwa kiwango hicho kikubwa, idadi ya walimu imekuwa ikiongezeka kwa kiasi kidogo ambacho hakitoshelezi mahitaji ya ngazi ya msingi na sekondari.

Pamoja na hayo, amekipongeza Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa kupendekeza na kukubaliana kutafakari hoja ya kuimarisha mafunzo ya ualimu na kupata utaratibu wa mafunzo ya ualimu ulio bora zaidi utakaowezesha kufanikisha malengo ya elimu kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vya ualimu na vyuo vikuu.

Mama Salma yuko kwenye kundi gani? Au naye ana title kama ya mumewe?
 
Na ukiona wa PhD anafundisha primary.............nina wasi wasi na hiyo PhD inayozungumziwa
 
Back
Top Bottom