Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Kwa nchi nyingi za dunia ya 3 ikiwemo Tanzania, kupata nafasi ya utumishi serikalini serikali huwa sio kwenda kuutumikia umma bali ni fursa ya kuiba na kutumbua (kula bata) kwa rasrilimali fedha ya umma huku wanaotakiwa kuhudumiwa na fedha hizo wakiogelea kwenye shida na changamoto kibao...Maswali ni mengi kuliko majibu. Kwa mfano;
1. Ni sekta binafsi gani hiyo inayoweza kupoteza pesa zake ili kugharamia maafisa wa serikali, umma, makada, mahawala na chawa kwenda Dubai?
2. Sekta binafsi ina maslahi gani ya moja kwa moja na mambo ya tabia nchi mpaka iwagharamie watu ovyo ovyo kwenda Dubai kwenye huo mkutano?
3. Tangu lini serikali imeanza utaratibu wa kuruhusu uholela wa watu binafsi kudandia kama wajumbe katika safari za Rais za nje ya nchi hata kama watajigharamia wenyewe? Serikali inajua athari na hatari zake?
4. Kwanini wameshindwa kutoa orodha ya majina na taasisi husika zilizogharamia hao watu kwenda Dubai kama wajumbe ili umma uweze kuamini na kuelewa.
Yaani hiyo taarifa inataka kusema, ujumbe wa Tanzania wa Rais nje ya Tanzania huwa hautegemei mipango, malengo na bajeti ya serikali bali hutegemea mwitikio na uwezo wa sekta binafsi kufadhili hilo. Ni kichaka cha sababu za kijinga na kipuuzi kabisa.
Bahati mbaya sana kuwa hata kiti kikuu cha cha u - Rais na aliyekikalia naye anakabiliwa na roho iyo hiyo ya wiziwizi (ufisadi) na tamaa ya kutumbua. Na kwa kesi hiyo, nani atawasimamia na kukemea walio chini..
Tunapaswa kuhanikiza kufanyika Kwa mabadiliko ya mifumo ya kiutawala haraka sana. Tujenge mifumo imara ya kikatiba na kisheria ya kusimamia na kuwawajibisha viongozi tunaowapa dhamana ya kuongoza...