Tetesi: Serikali yadaiwa kumvua uraia Padri wa Kanisa Katoliki

Kisheria, ni nini wanadai kime justify kushuku uraia wake?

In other words, what is the probable cause, kitu kinachofanya atiwe shaka Bakari au Neema na siyo Mzee wa Upako au Shehe Kipozeo au Mchungaji Mama Rwakatare au Alhaji Jakaya Kikwete.
 
Nchi ipo kwenye giza nene sana
We mkuu ni hamnazo, unaamka asubuhi unaenda kugombania usafiri wa kwenda kazini unafika kazini unasubiri mda wa chai ukanywe, lanchi ukale, jioni ukagombanie usafiri urudi home, uko salama km una familia inategemea utarudi salama hawategemei hata siku moja utalipukiwa na bomu au utakuta vita njiani inaendelea, afu hayo yote hamna unaleta ushuzi wa nchi iko kwenye giza, nenda usiku baa uone giza lipo wapi watu wanakula bata, maclub yanajaa, asubuhi saa 11 wanaamsha makazini we hilo giza umeliona wapi mkuu, acha kupotosha akili finyu za wafuasi wenzio
 
unaweza kua sahihi,lakini huyo padri ni mrundi,hapo hata akipiga novena itamrudia hakuna dhulma hapo,ametendewa haki
Tanzania ndio nchi pekee dunia,mgeni anaweza kujichanganya na raia,akapata pasi na kadi ya kura akajifanya mtanzania
Hivyo vitu anavipataje kama siyo raia?
 
Kikao kile na Maaskofu hawakuzungumzia mambo kama hayo? Walikwenda kufanya nini?
 
kama wewe ni mtanzania,huwezi kushindwa kuonesha walipozikwa wazee wako,muite Helsinki nae awe mkimbizi wa kiuchumi
Uelewa finyu, waliozama na MV bukoba takribani watu 1000 na MV Spice Islander iliyoua karibu watu 200 unaweza kutuonyesha makaburi yao yako wapi, acheni ushabiki maandazi.
 
hata ukiacha hiyo, kuna watu hawakukulia makwao, wametawanyika wakiwa wadogo na hivyo hawawezi kujua mambo ya makabuli! Ni mpaka awe na shida na vitu kama hivyo. Mimi sijui makaburi ya babu/bib zangu nilikuwa wamekufa kitambo na sukulia nyumbani, nitajuaje makaburi hayo!
 
Anaandika Ansbert Ngurumo:

UTAWALA wa Rais John Magufuliumeendelea kujizolea kashfa ya kutumia “silaha ya uraia” katika kukomoa raia, kuzima sauti za wananchi na kulipiza visasi.

Zamu hii serikali imemnyang’anya uraia Padri Raymond Saba, wa Kanisa Katoliki, ambaye hadi wiki chache zilizopita alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Padri Saba ni mzaliwa wa Kigoma.

Tunazo taarifa za uhakika kuwa idara ya uhamiaji ilimchukulia hatua hiyo akiwa katibu mkuu wa TEC. Hiyo ndiyo sababu iliyozingatiwa na TEC kumwondoa katika wadhifa huo na kuteua Dk. Charles Kitima.

Maaskofu walipobadili uongozi wa juu – rais na makamu wake ambao walikuwa wanamaliza muda wao – wakamwondoa na katibu mkuu. Kwa sababu kanisa halikupiga kelele, mbele ya umma suala hili lilionekana kama mabadiliko ya kawaida tu ya uongozi, lakini kulikuwa na sababu zilizotokana na msukosuko wa serikali na vyombo vyake.

Serikali, kupitia idara ya uhamiaji, imekamata pasipoti ya Padri Saba ikimtuhumu kuwa si Mtanzania, na inamtaka athibitishe uraia wake. Miongoni mwa mambo ambayo wamekuwa wanataka afanye ni kuwaonyesha makaburi ya bibi na babu zake – jambo ambalo wamekuwa wanalifanya kwa kila wanayemtuhumu kuwa si raia.

Sababu ya serikali kumtia msukosuko padre huyo ni waraka wa kichungaji wa TEC ambao ulitolewa katika kipindi cha kwaresima mwaka huu, yeye akiwa katibu mkuu. Waraka huo, miongoni mwa mambo mengine, ulizungumzia kutetereka kwa amani ya nchi na kutaka viongozi wa nchi wajitafakari.

Serikali ilichukizwa na waraka huo, na baadhi ya viongozi wa kisiasa walijiapiza kulipiza kisasi kwa kukomoa au kuumbua baadhi ya viongozi wa dini kwa namna mbalimbali. Wapo waliozushiwa kutelekeza watoto. Wapo wanaotafutiwa kesi. Wapo wanaozuiwa kusafiri nje ya nchi. Wapo wanaopigwa kwa uraia – hasa watokao katika maeneo ya mipakani. Wengi wao wanaumia kimya kimya.

Msukosuko dhidi ya Padri Saba ulifikia kilele katika kipindi ambacho Mwigulu Nchemba, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, alisimamisha kazi Merlin Komba, msajili wa vyama katika wizara yake ambaye alikuwa ameagizwa na Ikulu kuandika barua za maonyo kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Barua ya serikali kwa TEC haikuvuja, lakini serikali ilikerwa na mawasiliano ya kanisa, na msimamo wa Padri Saba katika majibu ambayo kanisa lilitoa kwa maandishi, huku Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, aliyekuwa rais wa TEC akisumbuliwa na kuitwa ajieleze serikalini.

Baada ya maaskofu kubaini msukosuko na usumbufu uliokuwa unamkabili Padri Saba walimwondoa kwenye nafasi hiyo ili suala hilo lisiwe sababu ya nyongeza ya serikali kuendelea kuandama kanisa. Baadhi ya wapambe wa Rais Magufuli walichekelea alipoondolewa wakisema, “tumemkomoa.”

Serikali inaendelea kushikilia pasipoti yake kama inavyoshikilia pasopoti za wengine inaowachapa “kiboko cha uraia” kwa sababu za kisiasa.

Katika muda mfupi wa madaraka ya Rais Magufuli, suala la uraia limegeuzwa silaha ya kisiasa na linaendelea kuumiza wananchi kadhaa, hasa wanaokosoa serikali au wasiokubaliana na mambo kadhaa inayotenda.

Orodha ni ndefu lakini wengine wanaotajwa na vyombo vya habari, mbali na Padre Saba, ni hawa wafuatao:

Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship. Alitoa mahubiri makali katika Krismasi ya 2017, akaonya serikali juu ya dhuluma, hasa mauaji ya raia. Alimtaka rais atubu. Askofu Kakobe alitiwa misukosuko na polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Walipokosa jinsi ya kumtia hatiani, idara ya uhamiaji iliibua suala la uraia wake. Sasa anachunguzwa uraia.

Aidan Eyakuze mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, shirika lisilo la kiserikali ambalo limetangaza matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa umaarufu wa rais miongoni mwa wananchi umeshuka kutoka asilimia 96 (2016) hadi 54 (2018).

Wakati Twaweza walipotangaza kuwa rais alikuwa anapendwa na waanchi kwa asilimia 96 mwaka 2016, serikali haikutilia shaka uraia wa mkurugenzi wake. Ilipotangaza kushuka kwa umaarufu wake, taasisi yake ilisakamwa.

Baadhi ya vijigazeti vinavyofadhiliwa na serikali kwa ajili ya propaganda za kisiasa za CCM, vimekwenda mbali zaidi, vikamtaja kuwa ni mwanachama wa chama cha siasa (Chadema), jambo ambalo taasisi yake imekanusha. Sasa anachunguzwa uraia.

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge. Mwaka 2017 alitoa kauli kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili hatua nzuri zinazochukuliwa na serikali zizingatie misingi ya katiba badala ya kutegemea uamuzi wa mtu. Rais Magufuli ameshasema kuwa katiba mpya si ajenda yake.

Haikuchukua muda mrefu, idara ya uhamiaji ikaanza kuhoji uraia wa askofu huyo. Bado pasipoti yake imeshikiliwa. Anachunguzwa uraia.

Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alitoa taarifa kupitia simu yake kuhusu watu waliomteka usiku, wakamsafirisha usiku kucha kutoka Dar es Salaam hadi Iringa.

Kwa kuwa “watu wasiojulikana” ambao wamekuwa wanateka na kupoteza watu wanahusishwa na vyombo vya dola, yalitoka maagizo mengi ya kisiasa yakitaka kijana huyo ashughulikiwe. Serikali imemfumgulia kesi mahakamani. Amesimamishwa masomo chuoni. Anachunguzwa uraia.

Padri Saba, Askofu Kakobe, Eyakuze, na Nondo ni wazaliwa wa Kigoma. Askofu Niwemugizi ni mzaliwa wa Kagera. Orodha ya wanaoshughulikiwa “kimfumo” ni ndefu.
Hao wote uliowataja kimajina tu unajua kuwa si raia wa Tz mi naona serikali inafanya sawa tu
 
We mkuu ni hamnazo, unaamka asubuhi unaenda kugombania usafiri wa kwenda kazini unafika kazini unasubiri mda wa chai ukanywe, lanchi ukale, jioni ukagombanie usafiri urudi home, uko salama km una familia inategemea utarudi salama hawategemei hata siku moja utalipukiwa na bomu au utakuta vita njiani inaendelea, afu hayo yote hamna unaleta ushuzi wa nchi iko kwenye giza, nenda usiku baa uone giza lipo wapi watu wanakula bata, maclub yanajaa, asubuhi saa 11 wanaamsha makazini we hilo giza umeliona wapi mkuu, acha kupotosha akili finyu za wafuasi wenzio

Ok!!!
 
Yaani mzee Saba wa Mwanga Majengo ni mgeni? Kigoma lazima watu wafanye kitu cha tofauti ili tabia hii ikome.Ni kigoma pekee ndiko utashushwa kwenye gari pale kankoko kuulizwa kitambulisho.
 
unaweza kua sahihi,lakini huyo padri ni mrundi,hapo hata akipiga novena itamrudia hakuna dhulma hapo,ametendewa haki
Tanzania ndio nchi pekee dunia,mgeni anaweza kujichanganya na raia,akapata pasi na kadi ya kura akajifanya mtanzania
Unaongea usilo lijua.Wale tuliosoma Katubuka shule ya msingi tunaifahamu vizuri familia hii.Hata mdogo wake Alex ni padri ila hili halijamgusa.
 
Sasa huku tunakokwenda si kuzuri.

Ninakumbuka Namfua alitaka ardhi ya watawa wa kanisa Katoliki Kilacha itolewe kwa vijiji vya ujamaa.

Alisema ”ardhi itolewe kwa watu wanaozaa na kujenga taifa kuliko kuwaachia wale matasa”. Watawa walianza Novena, Namfua alipata ajali mbaya iliyisabisha kifo chake.
Maombi haya yaliyofanyika kipindi kile yafanyike na kwa huyu dhalimu aliyemjua Mungu.
 
hata ukiacha hiyo, kuna watu hawakukulia makwao, wametawanyika wakiwa wadogo na hivyo hawawezi kujua mambo ya makabuli! Ni mpaka awe na shida na vitu kama hivyo. Mimi sijui makaburi ya babu/bib zangu nilikuwa wamekufa kitambo na sukulia nyumbani, nitajuaje makaburi hayo!
Na Wewe mhamiaji haramu
 
Anaandika Ansbert Ngurumo:

UTAWALA wa Rais John Magufuliumeendelea kujizolea kashfa ya kutumia “silaha ya uraia” katika kukomoa raia, kuzima sauti za wananchi na kulipiza visasi.

Zamu hii serikali imemnyang’anya uraia Padri Raymond Saba, wa Kanisa Katoliki, ambaye hadi wiki chache zilizopita alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Padri Saba ni mzaliwa wa Kigoma.

Tunazo taarifa za uhakika kuwa idara ya uhamiaji ilimchukulia hatua hiyo akiwa katibu mkuu wa TEC. Hiyo ndiyo sababu iliyozingatiwa na TEC kumwondoa katika wadhifa huo na kuteua Dk. Charles Kitima.

Maaskofu walipobadili uongozi wa juu – rais na makamu wake ambao walikuwa wanamaliza muda wao – wakamwondoa na katibu mkuu. Kwa sababu kanisa halikupiga kelele, mbele ya umma suala hili lilionekana kama mabadiliko ya kawaida tu ya uongozi, lakini kulikuwa na sababu zilizotokana na msukosuko wa serikali na vyombo vyake.

Serikali, kupitia idara ya uhamiaji, imekamata pasipoti ya Padri Saba ikimtuhumu kuwa si Mtanzania, na inamtaka athibitishe uraia wake. Miongoni mwa mambo ambayo wamekuwa wanataka afanye ni kuwaonyesha makaburi ya bibi na babu zake – jambo ambalo wamekuwa wanalifanya kwa kila wanayemtuhumu kuwa si raia.

Sababu ya serikali kumtia msukosuko padre huyo ni waraka wa kichungaji wa TEC ambao ulitolewa katika kipindi cha kwaresima mwaka huu, yeye akiwa katibu mkuu. Waraka huo, miongoni mwa mambo mengine, ulizungumzia kutetereka kwa amani ya nchi na kutaka viongozi wa nchi wajitafakari.

Serikali ilichukizwa na waraka huo, na baadhi ya viongozi wa kisiasa walijiapiza kulipiza kisasi kwa kukomoa au kuumbua baadhi ya viongozi wa dini kwa namna mbalimbali. Wapo waliozushiwa kutelekeza watoto. Wapo wanaotafutiwa kesi. Wapo wanaozuiwa kusafiri nje ya nchi. Wapo wanaopigwa kwa uraia – hasa watokao katika maeneo ya mipakani. Wengi wao wanaumia kimya kimya.

Msukosuko dhidi ya Padri Saba ulifikia kilele katika kipindi ambacho Mwigulu Nchemba, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, alisimamisha kazi Merlin Komba, msajili wa vyama katika wizara yake ambaye alikuwa ameagizwa na Ikulu kuandika barua za maonyo kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Barua ya serikali kwa TEC haikuvuja, lakini serikali ilikerwa na mawasiliano ya kanisa, na msimamo wa Padri Saba katika majibu ambayo kanisa lilitoa kwa maandishi, huku Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, aliyekuwa rais wa TEC akisumbuliwa na kuitwa ajieleze serikalini.

Baada ya maaskofu kubaini msukosuko na usumbufu uliokuwa unamkabili Padri Saba walimwondoa kwenye nafasi hiyo ili suala hilo lisiwe sababu ya nyongeza ya serikali kuendelea kuandama kanisa. Baadhi ya wapambe wa Rais Magufuli walichekelea alipoondolewa wakisema, “tumemkomoa.”

Serikali inaendelea kushikilia pasipoti yake kama inavyoshikilia pasopoti za wengine inaowachapa “kiboko cha uraia” kwa sababu za kisiasa.

Katika muda mfupi wa madaraka ya Rais Magufuli, suala la uraia limegeuzwa silaha ya kisiasa na linaendelea kuumiza wananchi kadhaa, hasa wanaokosoa serikali au wasiokubaliana na mambo kadhaa inayotenda.

Orodha ni ndefu lakini wengine wanaotajwa na vyombo vya habari, mbali na Padre Saba, ni hawa wafuatao:

Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship. Alitoa mahubiri makali katika Krismasi ya 2017, akaonya serikali juu ya dhuluma, hasa mauaji ya raia. Alimtaka rais atubu. Askofu Kakobe alitiwa misukosuko na polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Walipokosa jinsi ya kumtia hatiani, idara ya uhamiaji iliibua suala la uraia wake. Sasa anachunguzwa uraia.

Aidan Eyakuze mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, shirika lisilo la kiserikali ambalo limetangaza matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa umaarufu wa rais miongoni mwa wananchi umeshuka kutoka asilimia 96 (2016) hadi 54 (2018).

Wakati Twaweza walipotangaza kuwa rais alikuwa anapendwa na waanchi kwa asilimia 96 mwaka 2016, serikali haikutilia shaka uraia wa mkurugenzi wake. Ilipotangaza kushuka kwa umaarufu wake, taasisi yake ilisakamwa.

Baadhi ya vijigazeti vinavyofadhiliwa na serikali kwa ajili ya propaganda za kisiasa za CCM, vimekwenda mbali zaidi, vikamtaja kuwa ni mwanachama wa chama cha siasa (Chadema), jambo ambalo taasisi yake imekanusha. Sasa anachunguzwa uraia.

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge. Mwaka 2017 alitoa kauli kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili hatua nzuri zinazochukuliwa na serikali zizingatie misingi ya katiba badala ya kutegemea uamuzi wa mtu. Rais Magufuli ameshasema kuwa katiba mpya si ajenda yake.

Haikuchukua muda mrefu, idara ya uhamiaji ikaanza kuhoji uraia wa askofu huyo. Bado pasipoti yake imeshikiliwa. Anachunguzwa uraia.

Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alitoa taarifa kupitia simu yake kuhusu watu waliomteka usiku, wakamsafirisha usiku kucha kutoka Dar es Salaam hadi Iringa.

Kwa kuwa “watu wasiojulikana” ambao wamekuwa wanateka na kupoteza watu wanahusishwa na vyombo vya dola, yalitoka maagizo mengi ya kisiasa yakitaka kijana huyo ashughulikiwe. Serikali imemfumgulia kesi mahakamani. Amesimamishwa masomo chuoni. Anachunguzwa uraia.

Padri Saba, Askofu Kakobe, Eyakuze, na Nondo ni wazaliwa wa Kigoma. Askofu Niwemugizi ni mzaliwa wa Kagera. Orodha ya wanaoshughulikiwa “kimfumo” ni ndefu.
Ndugu hata kama unasema ukweli,cheki facts zako kwanza,kabla hujaweka bandiko,Eyakuze sio mzaliwa wa Kigoma,ni Mhaya wa Bukoba,aliyezaliwa Mwanza
 
Nyerere asili yake ni Rwanda, mzee Mwinyi Asili yake ni Comoro , mkapa kwao ni Msumbiji, kikwete Asili yake ni congo wakahamia Tabora baadae Bagamoyo, huyo wa sasa asili yake ni Burundi baadae akaja kuwa wa chato, viongozi wa Tanzania wote kwa kiwango kikubwa Asili zao si Tanzania bali ni Nchi jirani.
Nilishawahi kusikia kuwa Kikwete na mwinyi ni descendants wa kiarabu!
 
Back
Top Bottom