Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema wanafunzi wa shule na vyuo pia wanatakiwa kusomea nyumbani kesho tarehe 27 na keshokutwa 28, Januari 2025, kutokana na kufungwa kwa barabara nyingi za jiji la Dar es Salaam kupisha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Barani Afrika.
Taarifa hiyo ni mwendelezo wa taarifa ya awali iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka kuhusu watumishi wa umma wa Mkoa wa Dar es Salaam kufanyia kazi nyumbani kwa siku hizo mbili.
Msigwa pia, amezitaka taasisi za sekta binafsi kufanya vivyo hivyo ili kuepuka usumbufu.