Serikali yafafanua mgogoro wa shamba la Lokolova Vunjo

Serikali yafafanua mgogoro wa shamba la Lokolova Vunjo

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
5614511e-7380-4692-9663-e14061a3a183.jpeg
6fe62892-cd7d-492b-8de0-c7b2a53aa618.jpeg
4f297166-baf3-4511-bcf2-e0c54e8a6f41.jpeg

​

Serikali imesema kuwa Shamba la Lokolova lenye ukubwa wa ekari 2,610, lililopo eneo la Himo, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, linamilikiwa kihalali na Chama cha Ushirika cha Ufugaji na Uzalishaji Mali Limited (LOKOLOVA), kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hayo yamesemwa leo, Oktoba 30, 2026, na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, wakati akijibu Swali Na. 54 lililoulizwa na Mbunge wa Vunjo, Mhe. Enock Zadock Koola, katika Mkutano wa Tano, Kikao cha Nne cha Bunge, jijini Dodoma.

Akijibu swali hilo kuhusu msimamo wa Serikali juu ya mgogoro wa shamba hilo, Mhe. Mmuya amesema Shamba la Lokolova, linalojulikana kama Shamba Na. 70, lilitengwa kwa matumizi ya kilimo na ufugaji, kisha kupimwa na kumilikishwa kwa Chama cha Ushirika cha Ufugaji na Uzalishaji Mali Limited (LOKOLOVA).

Amesema shamba hilo lilimilishwa kwa Hati Miliki Na. 3619 kwa muda wa miaka 99 kuanzia Julai 1, 1986.

Aidha, Mhe. Mmuya ameeleza kuwa mgogoro huo unatokana na malalamiko ya wakazi wa vijiji vya Lotima na Makuyuni kuhusu kuondolewa katika eneo la shamba hilo wakati wa umilikishaji wake kwa chama hicho mwaka 1986.

Kutokana na mgogoro huo, Chama cha Ushirika cha Lokolova kilifungua Shauri la Ardhi Na. 577 la mwaka 2024 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Moshi.

Mhe. Mmuya amesema kuwa baada ya shauri hilo kusikilizwa, Mahakama iliamua kuwa Chama cha Ushirika cha Lokolova ndicho mmiliki halali wa shamba hilo na kwamba wananchi waliopo ndani ya eneo la shamba wanapaswa kuondolewa kwa mujibu wa uamuzi huo.
 
Back
Top Bottom