Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Kwahiyo Sasa hivi nikitaka kuenda wilaya ya ngorongoro nisema nataka kuenda wapi Ili nieleweke naenda wapi?

Au niseme nataka kuenda vitalu vya Dubai?
Sema nataka kwenda hifadhi ya wanyama Ngorongoro!
 
Mene Mene Tekeli na Peresi
Serikali kupitia kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinachotoa ruhusa kwa mamlaka za Serikali kufanya mgawanyo wa Halmshauri za Wilaya;

Imetoa AMRI rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024; ili kufuta baadhi ya maeneo ya kiutawala kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27 Novemba, 2024.

Amri hii rasmi sasa inafuta Kata, Vijiji na Vitongoji katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo; Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo.

Katika Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro pekee, kupitia AMRI hii, Serikali imezifuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96.

Garatwa,
Dar es Salaam, Tanzania.
20 Agosti, 2024.
View attachment 3074791
 
Masai kasomeni Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999. Tatizo mnajazwa upepo na wanasiasa uchwara na NGOs wasioishi Ngorongoro
Sheria zinazo kandamiza wananchi mnapemda kweli zifuatwe tena na vifungu kabisa mnaoneshana ila zinazo ibana serikali na watu wake wala hata hamziongelei kabisaaa hata kama zimekiukwa
 
Dogo! Haki ikitendeka hakuna mzozo. ukiona hivyo ccm waisha fanya Dili aridhi ya wananchi
Kwann wanafutiwa vijiji vyao karibu na uchaguzi? Taarifa zimehamishiwa Msomera kama mtu kaamua kuhamia Ifakara je? Taarifa zake zikoje kwani lazima Msomera?
 
Kule ni hifadhini sio makazi ya binadamu,Masai sio wa kwanza kuhamishwa kwenye Hifadhi.Imefanyija hivyo Ruaha,imefanyika hivyo kwenye migodi ya Madini na imefanyika hivyo maeneo mengine kupisha maendeleo.

Kipawa pale Hadi Leo hii watu wanadai fidia lakini Masai wanahamishwa na kulipwa Kila kitu nk nk.

Kwamba Masai ndio spesho sana au? Ngorongoro ni Mali ya Tanzania sio Masai.

Wajanja wanataka ardhi... Juu waweke hotels, chini wachimbe madini!
Bi tozo alishasema Simba na tembo hawali madini. Sasa anataka yachimbwe!
 
Wajanja wanataka ardhi... Juu waweke hotels, chini wachimbe madini!
Bi tozo alishasema Simba na tembo hawali madini. Sasa anataka yachimbwe!
Sawa hizo hoteli zipo kibao tuu humo ndani na haijawahi haribu mazingira,kama ni Madini ni sawa kabisa yanatakiwa yachimbwe maana kote kwenye Madini watu walihamishwa.

Sasa hoja ya Masai Kubisha ni nini?
 
Kule ni hifadhini sio makazi ya binadamu,Masai sio wa kwanza kuhamishwa kwenye Hifadhi.Imefanyija hivyo Ruaha,imefanyika hivyo kwenye migodi ya Madini na imefanyika hivyo maeneo mengine kupisha maendeleo.

Kipawa pale Hadi Leo hii watu wanadai fidia lakini Masai wanahamishwa na kulipwa Kila kitu nk nk.

Kwamba Masai ndio spesho sana au? Ngorongoro ni Mali ya Tanzania sio Masai.
Wamepelekwa handeni wakajengewa na kuwekewa huduma zote muhimu lakini hawaelewi ..... Ogopa Sana MTU ambae anakaa kuangalia serikali imekosea ili aseme
 
Tahadhari, :-

MAMBO MUHIMU YA UHIFADHI WA RASILIMALI ZA MBUGA ZETU ZILIZOPO KWENYE MIPANGO YA UHIFADHI NA URITHI WA DUNIA, TUSIGEUZE KUWA MASUALA YA KISIASA, UHIFADHI HAINA UDUGU NA SIASA! TUELEWE HILI.
.
--Hayati rais Mwinyi aliwahi kuwa na operation yake ya ujangili, tutafakari bila operation ile huko mbugani kungelikuwaje?
 
Section 4 ya TLS itafanya kazi labda muifute!
kwani hiyo section ilikua hakuna wakati wa wenye kiburi na jeuri walipokua mabosi wa TLS japo sifahamu inaeleza au kuhusu nini 🐒
 
Back
Top Bottom