Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Tahadhari, :-

MAMBO MUHIMU YA UHIFADHI WA RASILIMALI ZA MBUGA ZETU ZILIZOPO KWENYE MIPANGO YA UHIFADHI NA URITHI WA DUNIA, TUSIGEUZE KUWA MASUALA YA KISIASA, UHIFADHI HAINA UDUGU NA SIASA! TUELEWE HILI.
this is among very visionary comments within this very esteemed platform JF...

thank you gentleman πŸ‘ŠπŸ’ͺ
 
kwani hiyo section ilikua hakuna wakati wa wenye kiburi na jeuri walipokua mabosi wa TLS japo sifahamu inaeleza au kuhusu nini πŸ’
Ilikuwepo lakini machawa wamekuwa hawaifanyii kazi.
Wale wachache waliyojaribu kuitumia waliminywa na madikteta wa CCM, mfano Fatuma Karume alifungiwa leseni yake ya uwakili mpaka leo na Tundu Lissu alipigwa risasi 16 na kuishia kulazwa Belgium kwa karibu mwaka!
 
Tangazo batili! Serikali itajuta kumuachia Mwabukusi kuwa Rais wa TLS!
Wanasemaga hakuna mkate mgumu mbele ya Chai πŸ˜…πŸ˜€πŸ™Œ

Lakini ngoja tuone bado ni mapema sana kufanya speculation's πŸ™ŒπŸ‘
 
kwani hiyo section ilikua hakuna wakati wa wenye kiburi na jeuri walipokua mabosi wa TLS japo sifahamu inaeleza au kuhusu nini πŸ’
Kila zama na kitabu chake subiri Mwabukusi aifanyie kazi ndiyo utajua ilikuwepo au haikuwepo. Kumbuka Tundu Lissu na Fatuma Karume ni wahanga wa section hiyo na kwa sasa msitegemee kumdhuru Mwabukusi hamtabaki salama!
 
ni wahanga wa kiburi na jeuri yao usipotoshe tafadhali
 
Lakini hii siyo amri ya 'KUFUTA' Vijiji na Vitongoji.
Ni amri ya Marekebisho ya Amri ya MGAWANYO.

Kuna mtu anaweza kuinterpret hiyo notice vizuri na nini implications yake?
 
Lakini hii siyo amri ya 'KUFUTA' Vijiji na Vitongoji.
Ni amri ya Marekebisho ya Amri ya MGAWANYO.

Kuna mtu anaweza kuinterpret hiyo notice vizuri na nini implications yake?
Kwa mujibu wa serikali amri hii inafuta kata, vijiji na vitongoji na ndiyo sababu wananchi katika maeneo hayo wamesitishiwa huduma za jamii kama ujenzi na ukarabati wa shule, zahanati, barabara na huduma zingine. Pia wamehamishiwa maeneo mengine kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na pia kurekebisha au kuboresha taarifa zao katika daftari la kupiga kura.

TLS na wabobezi wengine wa sheria wamepinga hatua hiyo na kutumia kifungu hicho cha 30 wanasema hakimpi mamlaka waziri kufuta maeneo bali kurekebisha mipaka ya utawala. Kwa hiyo wanakwenda mahakamani kupinga amri hiyo.
 
Asante sana
 
Hawa wamasai tusiwachukulie poa.

Wao wanasema waliruhusu watoto wao wahamie msomera lakini wao kamwe hawatohama pale hata iweje,
Tena aliyekua anaongea anasema wao wana akili eti wahamishwe kisa eti ujenzi wa mahoteli ya kitalii? Hapana rafiki.

Wamasai ni watu jasiri sana na hua hawana maneno na mtu ukiona hadi wao wanajua wanaonewa ujue kweli umewaonea vya kutosha.

Viongozi ogopeni wananchi wanaosema wako tayari kufa, yaani hao inabidi uwape haki yao mapema kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…