Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa barabara muhimu za maeneo mbalimbali nchini zilizoharibiwa na mvua.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametoa taarifa hiyo akiwa mkoani Morogoro alikoenda kwa dharura baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kuharibu barabara inayounganisha wilaya ya Ifakara – Mlimba kwenda mkoa wa Njombe.
Ulega amesema pamoja na kiasi hicho cha fedha kilichoidhinishwa na Rais kwa ajili ya ujenzi wa dharura, mipango ya serikali ya ujenzi wa kudumu wa barabara na madaraja inaendelea kama ilivyo na haiathiriwi na mipango hii ya dharura.
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
“Nimekuja kwenu wananchi wa Morogoro – na hasa nyinyi wa Ifakara, Malinyi, Ulanga na Mlimba, kuwafikishia salamu za Rais wenu na pole zake kwa taabu hii mliyoipata. Lakini nimekuja pia na habari njema. Rais wenu, Samia Suluhu Hassan, amekubali matumizi ya zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa dharura wa barabara na madaraja yaliyoharibiwa na mvua hizi zinazoendelea, hapa kwenu na maeneo mengine ya Tanzania, ili maisha yenu yaendelee. Barabara ni uchumi. Barabara ni maisha na lazima kazi ziendelee,” amesema.
Ulega aliyelazimika kukatisha kuendelea na vikao vya Bunge vinavyoendelea mkoani Dodoma kwa ajili ya kufanya safari hiyo ya dharura, alifuatana na baadhi ya wahandisi wabobezi nchini kutoka wizarani na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili wasimamie viwango kwenye ukarabati utakaofanyika.
Kabla ya kuzungumza na wananchi wa Ifakara na viongozi waliokuwepo kwenye eneo la barabara iliyokatika, Ulega alifanya ziara kwa njia ya helikopta akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, kuona athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja mkoani humo.
Baadhi ya miundombinu ya Morogoro kama madaraja, itafaidika pia na mpango wa serikali wa ujenzi wa madaraja na barabara wa kudumu unaoendelea nchini baada ya miradi yake kuridhiwa na serikali ya Rais Samia.
Baadhi ya barabara za Morogoro zitakazofaidika na mpango huu wa serikali ni Ulanga – Namhanga ambayo imetengewa zaidi ya shilingi bilioni 6.3 na Malinyi mpaka Mto Fulua iliyotengewa shilingi bilioni 12.
Soma pia:

- Ni kwamba nchi ilikuwa na barabara nzuri muda wote mvua za El Nino ndio zimekuja kuharibu?
- Serikali huu ndio muda wa kuzibua na kujenga mitaro pamoja na kukarabati barabara mbovu, msisubiri mvua zifike muanze visingizio na maigizo
- Kutokana na kuendelea kuharibika kwa miundombinu ya barabara kwa mvua, Waziri wa TAMISEMI aagiza marekebisho kwa fedha za dharura