Serikali Yaja na Mfumo Maalum wa Kuondoa Changamoto ya Ubambikiwaji wa Bili za Maji kwa Wateja

Serikali Yaja na Mfumo Maalum wa Kuondoa Changamoto ya Ubambikiwaji wa Bili za Maji kwa Wateja

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Serikali kupitia Wizara ya Maji imeanzisha madawati ya vituo vya huduma kwa wateja kwa Mamlaka zote za Maji na Usafi wa Mazingira nchini ambapo huwa na jukumu la kupokea taarifa za huduma, maoni, ushauri na malalamiko ikiwemo bili za Maji kutoka kwa wateja na wadau mbalimbali. Baada ya malalamiko kupokelewa kupitia dawati hilo huchunguzwa na ikibainika ni kweli wahusika huchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kupewa onyo, kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi kwa mujibu wa Sheri, Kanuni, Taratibu zilizopo kwa watumishi wa Umma" - Mhe. Eng. Andrea Kundo Mathew, Naibu Waziri Wizara ya Maji

"Katika kukomesha kabisa changamoto ya ubambikiwaji wa bili za Maji kwa wananchi, Serikali imebuni mfumo ambao pamoja na mambo mengine unahusika kusimamia Ankra za Maji zinazotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini ambao unafanya kazi kwa kumshirikisha mteja wakati wa usimaji wa bili za Maji, kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) mara usomaji unapofanyika ukionyesha usomaji wa sasa, usomaji wa mwezi uliopita na kiasi cha matumizi yake ya Maji kwa mwezi husika"

"Ujumbe huo pia humtaka mteja kuhakiki usomaji huo kabla ya Ankra yake kuandaliwa na ikiwa hajaridhika au kuhitaji ufafanuzi basi huwasiliana na namba ya huduma kwa wateja kwaajili ya ufafanuzi. Serikali inaendelea na jitihada za kuharakisha matumizi ya Dira za malipo ya kabla (Pre paid water meter) ili kupunguza au kuondoa kabisa kadhia ya kubambikia wananchi bili za Maji kwani watakuwa wakilipia kadiri wanavyotumia" - Mhe. Eng. Andrea Kundo Matthew, Naibu Waziri wa Wizara ya Maji

"Nini mkakati wa Serikali kwa wanaotumia Post Paid Water Meter kujipimia matumizi ya maji wao wenyewe? Je, ni gharama gani ambayo inatumika sehemu moja na sehemu nyingine juu ya kupima?" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Serikali tayari imeingia kwenye mkakati wa kufunga Pre Paid Water Meter na mkakati unaendana sambamba na kuhakikisha kwamba Post Paid Meter (Mechanical Meters) tunaanza kuziondoa kwa hatua na kuhakikisha wananchi wote tumewafungia Pre Paid Water Meter"

"Gharama zinatofautiana, Dar inaweza kuwa Tsh 2000/Unit, Dodoma, Gairo na Tuliani inaweza kuwa tofauti. Hii inatokana na njia ya uzalishaji wa zao la Maji kama tumezalisha Maji kwa kutumia Gridi ya Taifa au Umeme wa Jua au Maji ya mserereko lazima gharama zake zitakuwa tofauti kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine" - Mhe. Eng. Andrea Kundo Mathew, Naibu Waziri Wizara ya Maji

WhatsApp Image 2024-05-28 at 17.34.24.jpeg
 
Wahuni sana hizi mamlaka. Me karibu nilisafiri mwezi mzima lakini Bill imesoma kubwa kuliko hata siku ninazokuwepo nyumbani. Inaudhi sana hii hali.
 
Wanaanza lini kufunga hizo pre paid?

Mimi ni moja ya watu waliobambikiwa na nimegoma kulipa
 
DAWASCO au DAWASA wanatubambikia bili kwa kucheza na mita zao ili nusu lita isomeke Lita moja.
Mimi Nina tank la Lita elfu tatu.
Nikilijaza hili tank kwenye mita kunasoma Lita elfu sita au unit sita.
Anayebisha anaweza kuja tukahakikisha.
Nimekwenda kuomba mita irekebishwe au inadilishwe jibu kila Mara ni hakuna mita.
Ninaishi wilaya ya kidawasa ya Kibaha.
 
Back
Top Bottom