Serikali yakiri makosa kuwalazimisha Wafanyakazi wa Umma kununua laini ya simu ya TTCL

NAPE....Tueleze kwanini ulikataa bunge lisioneshwe mubashara?
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia amefikia uamuzi huo ambao ni sahihi; lakini kaufikia uamuzi sahihi kwa bahati.
Maendeleo makubwa kwenye sekta hii ya mawasiliano yamekuja baada ya Serikali za awamu za awali kubadili sera ya uchumi hodhi na kukubali sera ya ushindani katika soko. Voda wanaposhindana na Tigo au Airtel ndivyo huduma na teknolojia ya kisasa inapoletwa nchini ili kuwaridhisha wateja. Serikali inapoanzisha shirika lifanye biashara ya mawasiliano kama TTCL inatakiwa iache hilo shirika lishindane na voda, tigo na Airtel. Serikali inafaidi kwa huduma, ajira pia kodi kutoka makampuni yote kwa hiyo uwanja wa biashara lazima ulingane kwa kampuni zote na ni jukumu la Serikali kusimamia sera yake hiyo. Sasa akitokea kiongozi kuagiza kwa kauli ya kiutawala kuwa wanunuzi au watumia huduma lazima watumie TTCL ni kuidhoofisha TTCL kwa kubebwa hivyo kushindwa kukomaa kwenye ushindani lakini mbaya zaidi Serikali inakuwa inapingana na sera yake na faida za ushindani katika nchi. Naona wengi hatuelewani humu pamoja na viongozi wetu. Hatujui au tumesahau tumetoka wapi na tunakwenda wapi. Tumesha sahau kuwa kuna kipindi ilitakiwa uhonge ili TTCL wakuwekee simu nyumbani au ofisini. Ile ilikuwa sera ya serikali ya uchumi hodhi kwenye mashirika ya serikali. Tumetoka huko; mkirudi tuambieni. Ningependa kuamini kuwa hilo ndilo waziri wetu mpendwa analisahihisha. La sivyo, wataalam wake wizarani na TCRA hawajampa maelezo haya ambayo nimeeleza.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…