Serikali yakiri makosa kuwalazimisha Wafanyakazi wa Umma kununua laini ya simu ya TTCL

Serikali yakiri makosa kuwalazimisha Wafanyakazi wa Umma kununua laini ya simu ya TTCL


Wakati wa utawala wa awamu ya 5 chini ya Dr Magufuli, viongozi wa serikali, wakiwemo Mawaziri na wafanyakazi wa serikali walilazimishwa kununua line ya simu ya TTCL kibabe, huku wengine wakipigwa mkwara kwamba wasipokuwa na line ya TTCL watang'olewa kwenye uongozi, lengo la jambo hilo kwa akili ya viongozi wa wakati ule ilikuwa kulazimisha mtandao wa TTCL kupata wateja wengi, hata hivyo idadi ya wafanyakazi wote wa serikali ya Tanzania inakadiriwa kufikia laki 6 tu.

Nchi yenye Raia wanaotajwa kuzidi mil 60, hata ukichukua wafanyakazi wote ukawapelekea line za TTCL kwa mtutu wa bunduki mtandao huo hauwezi kuteka soko kwa idadi hiyo ya wateja, Binafsi nilipinga vibaya sana jambo hilo na nikashauri viongozi wa wakati ule kwamba, ikiwa wanataka TTCL ishamiri basi Wanaccm wote waliodaiwa kuwa wengi sana nchini Tanzania ndio walazimishwe kununua line za TTCL, pamoja na kwamba Mwenyekiti wa ccm alikuwa Magufuli huyohuyo lakini ushauri wangu hakuufuata .

Leo Waziri Nape amekiri hadharani kwamba uamuzi ule haukuwa na lolote la maana.

===

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwamba haukuwa utaratibu sahihi kuwalazimisha viongozi wa serikali kumiliki na kutumia laini za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Amesema kufanya hivyo kunaweza kusiwe na matunda yanayotarajiwa kwani kiongozi anaweza kuinunua kwa sababu amelazimishwa, lakini akatumia ya mtandao ambao yeye anaupenda.

“Huduma hizi hazilazimishwi. Ukiwalazimisha watu wachukue laini, watachukua hiyo uliyowalazimisha halafu watachukua na ile wanayoipenda,” amesema Nape na kuongeza kwamba “I don’t think if it was a good model [sidhani kama ulikuwa utaratibu mazuri.”

Nape amesema hayo akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari aliyetaka kujua wizara ina mpango gani kuhakikisha kwamba TTCL inafikisha mawasiliano vijijini ikizingatiwa kwamba Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza awatumishi wote wa serikali kuwa na laini za TTCL.

Aidha, katika mkutano huo wa kueleza mafanikio ya wizara kwa mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan iliibuliwa tena hoja ya gharama za intaneti na waziri akasema kwamba gharama zilivyo sasa zipo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria.

“… Kwa presha ya siasa tumeshuka hadi tukapitiliza kiwango kilichoiwekwa kisheria. Sasa hatuwezi kuendelea kushuka kama tunahitaji huduma bora,” amesema.

Amesema kuwa ukitaka huduma bora sharti ukubali kuigharamikia kidogo na kuwataka wananchi kuacha malalamiko, kujiona wanyongea au kudhani kwamba wanaonewa.

Hata hivyo, amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea na mazungumzo na wadau kuona namna ya kuboresha gharama hizo ili kuimarisha na kukuza matumizi ya huduma za intaneti nchini.


Pia soma: Serikali: Sio Watumishi wote wa Umma wanatakiwa kuwa na laini ya TTCL bali Viongozi wanaopewa vocha watapewa za TTCL
huyo nae ni mnafiki ana chuki binafsi na jiwe kwa kumtumbua enzi zile.
 
Hizo hizo public phones ndizo wangezitumia Makamba, Kinana na Nape "kutrepiwa".
Ukimaanisha nini kwamba nikipigiwa nikajifungie chooni secretary asisikie au na yenyewe naweza kwenda nje chini ya mti (how far though) Hivi hukusikia mambo ya Wiretap na enzi za FBI na Mafia's ?

Au unadhani kwanini wauza drugs wengi walihamia kwenye Beepers na wakipigiwa wanakimbilia kwenye public phones ?
 
What do you mean mfanyakazi humpi voucher akiwa kazini halafu unataka awe na vocha ya TTCL ya kuwasiliana ofisini halafu sababu vocha za TTCL hazipatikani nchi zima TTCL wanasema wameingia mkataba na Tigo Pesa kuwa kama eneo vocha za TTCL hazipo mfanyakazi wa Serikali anunue vocha kwenye Tigo Pesa !! Huyo mwajiri hajazi vocha,Hawaii Tigo pesa,halipii charge za kununua vocha halafu unataka kila mfanyakazi awe na Line ya TTCL at whose cost?

Nilipinga Magufuli humu live kuwa labda aongeze mishahara na vocha Serikali itoe
Hii ni petty issue
 
Nchi ilikua inaendeshwa na genge fulani na kwa matakwa yao binafsi .
 
Yaani uichukie ttcl kwani wewe ndiyo serikali inayolipa hizo bili za simu zinazotumika kwa viongozi wa serikali? Acheni hizo, fanyeni mambo yenu personal bila kumhusisha JPM, he did good to this country bahati mbaya wema hawaishi muda mrefu na nabii hakubaliki kwao
Ujinga utakuisha lini? Utaupenda vipi mtandao hauvuki mji?
 
Kwa hiyo watumishi wa umma kujiunga TTCL haikuwa sera ya sirikali, lilikuwa tamko.....
 
Kwa hiyo watumishi wa umma kujiunga TTCL haikuwa sera ya sirikali, lilikuwa tamko.....
Hakuna mtumishi wa serikali kwa private communication aliyeambiwa kujiunga ttcl ila provider wa serikali kwa official communications ndiyo alikuwa ttcl msipotoshe umma kwa maslahi yenu binafsi...Fanyeni deal zenu bila kutaka ku smear mad kwa wenzenu...
 
Hakuna mtumishi wa serikali kwa private communication aliyeambiwa kujiunga ttcl ila provider wa serikali kwa official communications ndiyo alikuwa ttcl msipotoshe umma kwa maslahi yenu binafsi...Fanyeni deal zenu bila kutaka ku smear mad kwa wenzenu...
Kwa hiyo hakukuwa na tamko watumishi wa umma kutakiwa kujiunga TTCL kuwaongezea wateja, wote wanaoongea hapa wewe ndo pekee unayejua.......acha ukilaza basi.
 
Kwa hiyo hakukuwa na tamko watumishi wa umma kutakiwa kujiunga TTCL kuwaongezea wateja, wote wanaoongea hapa wewe ndo pekee unayejua.......acha ukilaza basi.
Hakujawahi kuwepo...Lilete hapa kama unalo!
 
Hizo zilikuwa akili za matope
Biashara inataka ubunifu na ushindani na sio kulazimisha watu wanunue bidhaa yako

TTCL kama wangecheza karata vizuri leo Soko lao lingekuwa juu sana na ndio wangekuwa wanakodisha mpaka line za underground walizoweka Halotel zingekuwa zao
Simu za mezani ni muhimu kila sehemu hilo wangelipa nguvu na kujitangaza kwa bei poa

Shirika la Posta angalia hamna kitu

Posta ya UK Ina miaka 500 na mpaka leo wanasambaza parcel Bilioni 16 kwa mwaka yes 16b items
Nao population ni kama sisi daaa
Shirika la posta tz limekalia kuiba parcels za wateja wao, hovyo sana
 
Shirika la posta tz limekalia kuiba parcels za wateja wao, hovyo sana

Hakuna siku nimekasirika kama nilipotuma documents zangu bongo tena zingine hazina copy kabisa
Nimetrace mpaka posta Dar
Eti hawakupokea huku wanasema zimefika
Walinikera sana walifikiri kuna hela
Wametupa docs zangu bure
Huku wanasema wanilipe fidia nikawaambia ni priceless hata wakinipa millions haitarudisha hizi og

Hao ni takataka kabisa
 
Hakuna siku nimekasirika kama nilipotuma documents zangu bongo tena zingine hazina copy kabisa
Nimetrace mpaka posta Dar
Eti hawakupokea huku wanasema zimefika
Walinikera sana walifikiri kuna hela
Wametupa docs zangu bure
Huku wanasema wanilipe fidia nikawaambia ni priceless hata wakinipa millions haitarudisha hizi og

Hao ni takataka kabisa
Wale wafanyakazi wana njaa saana
Kila kitu ni kuchakura na kupotea nacho gizani
 
Back
Top Bottom