Hizi ndio akili za kijinga za maccm,hata Kama sio kukopa aina ya vipaombele vya maccm havina maana kabisa kwa mtu wa kawaida hata hao middle class ni walimu,Hawa ndio watapanda ndege? Yaani wafanyabiashara wenye viduka vya mln 5-10 ndio watapanda ndege? Zero brain kabisa Hawa jamaa,ni juzi tu hapa Tzn ni moja ya nchi zenye maskini wengi Afrika bado ccm inakomaa na miradi tembo mweupe.
Mifano ipo mingi ya kuthibitisha hoja,uwanja wa mpanda toka umejengwa enzi za Jk ndio mwaka na mwezi huu airtzn inaenda Mara moja kwa wiki,hivyo ndivyo itakuwa kwa viwanja vya Shinyanga,Tabora na Sumbawanga.Songwe airport ina miaka lakini kuna kampuni moja tu inautukia ndo itakuwa huko kwingine?.Uwekezaji haulengi kuwainua kimaisha watu wa kawaida.
Nyie maccm mnakera Sana,jengeni viwanja au miradi strategic Kama Kigoma airport au uwanja kule Njombe ungesafirisha japo maparachichi,na Kama kawaida yenu wakandarasi ni mabwana zenu wachina.Hizo pesa ni Bora mungejenga barabara mikoa husika maana kwa pesa hizo ni zaidi ya km 100 .Kwa mkoa wa Rukwa kwa mfano mungejenga barabara ya kwenda bonde la ziwa Rukwa kutoka Ntendo/Sumbawanga-muze-Kasansa-Majimoto-Inyonga, wananchi wangewashukuru Sana maana mungewarahisishia biashara na mikoa ya Tabora,Mwanza nk wakauze nafaka zao kwa bei nzuri,sasa nyie ndugu sijui mlilogwa na nani kwa sera zenu hizi za ajabu ajabu.
Ila Mimi naona maccm muendelee hivyo hivyo na miradi tembo mweupe ili watakaowachagua wapigike kweli kweli ili incase mkishinda uchaguzi huu ,ujao uwe mwepesi kwa wapinzani,ko endeleseni speed ya kujenga jenga miradi isiyo na tija kwa common raia ili wapate akili.