SERIKALI YAMJIBU MBUNGE WA KAWE KUHUSU UJENZI WA SOKO LA TEGETA NYUKI

SERIKALI YAMJIBU MBUNGE WA KAWE KUHUSU UJENZI WA SOKO LA TEGETA NYUKI

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911


Mbunge wa Jimbo la Kawe Jijini Dar es salaam Mhe, Timoth Geoffrey Anyosisye ameishauri Serikali kukarabati Soko la Tegeta Nyuki, akisema miundombinu yake imechakaa na kusababisha wafanyabiashara pamoja na wateja kufanya shughuli zao katika mazingira magumu.

Timoth akiuliza swali bungeni jijini Dodoma leo Septemba 2, 2026, katika Kikao cha Sita Mkutano wa Nne wa Bunge la 13, Mbunge huyo alitaka kujua iwapo Serikali ina mpango wa kukarabati soko hilo ambalo ni muhimu kwa wananchi wa Manispaa ya Kinondoni, lakini kwa sasa hali yake imekuwa ikitishia ufanisi wa shughuli za kibiashara.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), amesema Serikali imeliingiza Soko la Tegeta Nyuki katika mpango wa uboreshaji wa miundombinu kupitia Awamu ya Pili ya Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DMDPII) katika mwaka wa fedha 2026/27.

Waziri huyo amesema kwa sasa mradi huo uko katika hatua ya ununuzi wa kutangaza zabuni ya kuwapata wataalam washauri watakaofanya usanifu na usimamizi wa ujenzi.

Aidha, taarifa ya tathmini ya tamko la nia imewasilishwa Benki ya Dunia kwa ajili ya kuidhinishwa, huku usanifu ukitarajiwa kukamilika Desemba 2026 ili hatua za ujenzi ziweze kuanza.
 
Back
Top Bottom